Hongera sana rafiki kwa siku hii njema sana. Leo hii siku ya kipekee sana naomba uitumie vizuri sana.
Katika tungo yake ya Kioo; Jaguar ambaye ni mwanamziki amewahi kunukuliwa akiimba hivi
“maisha ni kama safari/ na ya kwangu ishanoa nanga. Kuna siku mbili muhimu ya kuzaliwa na ya kuzama. Yangu ya kuzaliwa nishaijua bado ya kuzama kutoka duniani”.
Katika kusema hivyo mwanamziki huyu alitaka kutwambia kwamba safari ya maisha inaanza pale unapozaliwa na hitimisho la safari hii ni pale unapoaga dunia. Mambo unayofanya kati ya siku yako ya kuzaliwa na kuaga dunia ndiyo yatakufanya uendelee kuishi milele hapa duniani au utoweke kabisa.
Soma Zaidi: NANI ATALIA UTAKAPOKUFA?
Kabla sijakwambia mambo ya kufanya, kuna swali moja ningependa ujiulize. Hivi ni kitu gani huwa kinafanya watu fulani tuwakumbuke milele na wengine kusahaulika siku chache baada ya kifo?
Hivi kwa nini mpaka leo watu kama Albert Einstein, Thomas Edison, Socrates, Seneca, John D. Rockefeller na wengine tunawakumbuka? Kwani kipindi wao wanaishi hakukuwa na watu wengine wanaishi? Sasa hawa watu walifanya nini? Hapa kuna vitu sita ambavyo vinawatofautisha watu hawa, vitakutofautisha na wewe pia.
1. TAFUTA KITU KIMOJA CHA KUFIA
Kuna vitu vingi sana ambavyo unaweza kufanya kwenye maisha yako. Kuna vingi pia vya kufanya ndani ya siku moja. Sasa utapaswa kuchagua kitu kimoja ambacho utapaswa kushughulika nayo kwa sababu huwezi kukimbizana na kila kitu. Hivyo chagua kitu ambacho unasema hata iweje, mimi nitakufa nafanya hili.
Mimi kwenye maisha yangu kuna vitu hivi vinne ambavyo nitafanya kuhakikisha vinafanikiwa kila kitu kwa wakati wake kwa wakati wake.
Kuwa mwandishi na mhamasishaji nambari moja Afrika.
kujenga chuo kikuu kikubwa barani Afrika (HARVARD OF AFRICA)
Kuwa raisi wa jamhuri ya Muungano Wa Tanzania.
Kufika kwenye sayari ya maazi na kuanzisha tawi la chuo changu huko.
Nimechagua hivi vinne. Sio lazima na wewe uwe na vinne kama mimi. Ila mimi naona kwa upande wangu naona kama sitakamilisha vitu hivi, basi nitakufa na deni kubwa sana. Na kwa sababu sipendi kufa na deni basi nitafanya kazi mchana na usiku kufikia hivi vitu. Ila hivi vitu vinne ninaweza kuviunganisha kama kitu kimoja kwa kusema, “nitafanya maisha ya watu kuwa bora zaidi nilivyoyakuta”.
Soma zaidi; Hii Ndio Njia Nitakayoitumia Kujjenga Chuo Kikuu Kikubwa Na Bora Barani Afrika (HARVARD OF AFRICA)
Hivi Ndivyo Wewe Unaweza Kuungana Na Mimi Katika Kujenga Chuo Kikuu Kikubwa Na Bora Barani Afrika
2. ANDIKA KITABU
Watu wa zamani waliamini ili uishi milele moja unapaswa kupanda mti,
Pili unapaswa kuzaa mtoto wa kiume na
Tatu unapaswa kuandika kitabu lakini Sasa hivi tunasema hivi,
Moja, kupanda miti (KUMBUKA SIO MTI MMOJA TENA)
mbili kuzaa mtoto (KUMBUKA SIO MTOTO WA KIUME TENA)
Kuandika kitabu. Mada hii tutaiongelea kwa kina siku nyingine, ila kwa leo napenda ufahamu hivi mambo unayojua wewe ni mengi sana. Hivyo usikubali kufa nayo kichwani mwako. Yaandikie kitabu.
Soma Zaidi; KITABU; KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI
3. TATUA MATATIZO YANAYOIKABILI JAMII
Jamii ina matatizo mengi sana. Mengine watu wanajua kwamba wanayo, mengine hawajui kabisa kama wanayo. Kazi yako iwe moja tu kutatua matatizo yanayoikabili jamii yako. Usiishie kulalamika unapokutana na matatizo kwenye jamii. Yatatue.
Soma Zaidi; HIZI NI KAULI MBIU MBILI MUHIMU KWA KILA MWANAMAFANIKIO
4. WAFANYIE WATU KITU AMBACHO HAWATAWEZA KUKULIPA
Huwa tunapenda tunapofanya kitu basi tulipwe. Sasa amua kuwafanyia watu kitu ambacho wewe hutadai kulipwa.
5. WAACHE WATU WAKIWA BORA ZAIDI YA ULIVYOWAKUTA
Usiwe mchonganishi. Popote pale uendapo wafanye watu waone umuhimu wako. Wafanye waione dunia kuwa ni bora zaidi.
Kuna watu wana matatizo yao ya kifamilia, kimahusiano, wengine wamepoteza biashara zao, watu wao wa muhimu. Wengine wana hofu juu ya jambo fulani ambalo linakuja. Kazi yako iwe moja tu, kusambaza upendo kwa watu wote hawa.
6. KUWA NA MAHUSIANO BORA NA MKE /MME/FAMILIA
Familia yako ni sehemu nambari moja unapopaswa kuonesha upendo wako.