Vitu Vitatu (03)) Ambavyo Vinahitaji Kuboreshwa Kila Siku


Mwalimu Nyerere aliwahi kusema “maadui wa taifa letu ni watatu, umasikini, ujinga na maradhi.

Vitu hivi vitatu umasikini, ujinga na maradhi ni vitu ambavyo kila mtu anapaswa kujiepusha navyo kwa kipindi chote anachoishi hapa duniani.

UJINGA.  Huu ndio chanzo cha vitu vingine vyote. Ujinga huleta umasikini. Ujinga huleta pia maradhi.

Kama hauna elimu nzuri ya pesa utaishia kushika pesa na kuipoteza ila haitakaa mikononi mwako.

Kama hauna elimu nzuri ya juu ya afya utajikuta unaugua magonjwa, utajikuta afya yako inadhoofu kwa sababu tu hujajifunza.

Kwa hiyo ujinga sio jambo la kufumbia macho. Jitahidi kujifunza kila siku ili uondokane na ujinga.

Wanasema Elimu ni bahari wakimaanisha kwamba kujifunza hakuna ukomo. Usiweke ukomo kwenye kujifunza. Soma vitabu vingi kadri uwezavyo.
Hudhuria semina nyingi kadri uwezavyo.
Jifunze vitu chanya bila kuchoka

UMASIKINI: Umasikini unatokana na aina ya elimu uliyonayo na jinsi unavyochukulia mambo. Kama kichwa chako kimejaa fikra za kimasikini basi jua utapata matokeo ya kimasikini. Kijaze kichwa chako fikra za kitajiri, utshangaa sana na wewe utaanza kupata matokeo ya kitajiri.

Lakini pia ujue hakuna ukomo kwenye kupata pesa. Ukipata pesa unaweza kupata zaidi na zaidi kwa kuwasaidia watu wengi zaidi.  Hivyo kila siku komaa kuongeza thamani unayotoa ili uweze kupata matokeo bora zaidi.

MARADHI. Hakuna mtu ambaye anaweza kusema mimi nimeondokana na maradhi kwa asilimia 100. Lakini sasa, kitu muhimu ambacho mtu anapaswa kujua ni kwamba kuna vitu unaweza kuvifanya ili kuepuka maradhi.

Kwa mfano unajua kwamba kunywa maji machafu kunaweza kusababisha maradhi, hivyo utapaswa kunywa maji safi na salama. Na haufanyi hivyo mara moja, utafanya hivyo maisha yako yote.
Hivyo hivyo kwa vitu vingine vinavyohusiana na afya.

Kwa hiyo nipende kukwambia kwamba kila siku, namaanisha kila siku, jitahidi kuboresha afya yako ili iwe bora zaidi. Jitahidi kuongeza maarifa na jitahidi kutoa thamani ili uwahudumie watu kuondokana na umasikini.

Umekuwa nami,
Godius Rweyongeza
0755848391

KUPATA KITABU CHA KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI BONYEZA HAPA


One response to “Vitu Vitatu (03)) Ambavyo Vinahitaji Kuboreshwa Kila Siku”

  1. Hakika nimeipenda hiii elimu lakini nawaomba jambo Moja kuwa ingefaaa piah muwe mnatoa na nakala Kwa ujumbe wa sauti Kwani Kuna wengine hawajui kusoma kusudi kwamba elimu iwe inatufikia watu wote bila kubagua Asante Kwa elimu nzuri

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X