Makala ya 600: Shukrani Kwa Wasomaji wa Songa Mbele Blog. Pongezi Kwa Godius Rweyongeza, Zawadi Kubwa Sana Kwako, Na Yajayo Yanafurahisha


Makala ya 600: Shukrani Kwa Wasomaji wa Songa Mbele Blog.
Pongezi Kwa Godius Rweyongeza, Zawadi Kubwa Sana Kwako, Na Yajayo Yanafurahisha

Leo ni siku ambapo zimefika makala 600 kwenye blogu hii. Hili ni jambo la furaha kwangu na kwa wote ambao tumekuwa kwa pamoja kwa siku zote hizi.

Tarehe 21, septemba 2016 ilikuwa siku ambapo niliandika makala ya kwanza kwenye blogu hii. Baada ya hapo nimeendelea kuandika mara kwa mara kwenye blogu hii mpaka leo hii zimefika makala 600.

1. SHUKRANI KWA WASOMAJI WA BLOGU HII
Naomba nitoe shukrani kubwa sana kwako msomaji  wa blogu hii. Kiukweli wewe ni mtu muhimu ambaye siku zote unanipa nguvu za kuendelea kuandika.

Kuna wale ambao huwa mnanitumia barua pepe na pengine mnaniandikia ujumbe mfupi au kunipigia. Kwa hakika nakubali na kuuheshimu sana mchango wenu. Hata wewe ambaye hujawahi kunitafuta usiwaze, Mimi niko kwa ajili yako. Kikubwa napenda upate maarifa makubwa ambayo ukichukua hatua basi upate matokeo makubwa.
Kuna usemi ambao nimekuwa nautumia mwaka huu ambao ni
MALENGO MAKUBWA + HATUA KUBWA = MATOKEO MAKUBWA. Hivyo nahakikisna huku unapata maarifa yatakayokufanya uweke malengo makubwa. Maarifa yatayokusukuma uchukue hatua kubwa mwisho wa siku upate matokeo makubwa sana.

HONGERA SANA KWAKO GODIUS RWEYONGEZA
Kwa siku zote hizo, makala za blogu nimekuwa nikiziandika mimi Godius Rweyongeza. Na bado nitaendelea kuandika. Kwa hiyo naomba na Mimi leo nijipongeze kwa kile ambacho nimefanya.
Mwisho naomba nikwambie bado tupo pamoja na tuendelee. Safari inaendelea.

YAJAYO YANAFURAHISHA
Yajayo yamafurahisha, Kweli yanafurahisha.
Makala bora zaidi zinazidi kuja mbeleni. Na mafunzo mengine zaidi. Vitabu vingi vinazidi kuja na bora zaidi. Kaa mkao wa kula yajayo yanafurahisha.

ZAWADI YANGU SIKU YA LEO
Sio vyema siku hii ipite tu bila ya mimi kutoa zawadi. Napenda kutoa zawadi kwa watu wangu wote wa nguvu,
Leo naomba niseme vitabu vyangu nitavigawa bure kabisa kwa wale wote ambao watasoma makala hii. Unachopaswa kufanya ni kuandaa 5000/- tu.
Baada ya hapo nitumie ujumbe mfupi kwanza kwa wasapu. Usianze kutuma pesa. Nitakuelekeza utume pesa kwenda 0742854498 jina GODIAN THEONEST. Kwa leo hatutatuma pesa kwa namba ile ya 0755848391 kwa sababu imepotea na hado sijaweza kuirudisha. Badala yake namba hiyo hapo juu itatumika.

Namba  nyingine ni   0737802316 (TTCL) na 0685763091 (AIRTEL)

Majina yake ni GODIUS RWEYONGEZA
Ukishatuma hela nitumie ujumbe wa wasapu tu kwenda namba ya Voda hiyo hapo juu.
Nitakutumia Vitabu vyoote vitano bila kuchelewa.

Gharama ya Vitabu vyote kama utanunua kimojakimoja ni 57,000/- leo unavipata kwa sh. 5,000 tu. Karibu sana

Karibu sana tuendelee kuwa pamoja.

Umekuwa nami,
Godius Rweyongeza
0755848391

KUPATA KITABU CHA KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI BONYEZA HAPA


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X