Kitu cha kufanya pale unapokuwa na ndoto kubwa inayohitaji pesa na wewe hauna pesa.


Mara nyingj unapokiwa unaanza maisha, lazima ndoto zako zitakuwa kubwa. Ni kubwa kiasi kwamba ukimwambia mtu atabaki kushangaa na kukakaa mdomo wazi hadi nzi wakaingia. Bila shaka unekutana na hali hii kama bado utakutana nayo. Wewe unayejua wapi unaenda na kwa nini huwezi kushangaa. Mwingine akisikia ndoto yako atakuuliza pesa utaitoa wapi ya kufanya hayo yote? Kwa haraka unapaswa kumjibu kwambabnitasambaza upendo. Ila kadri tunavyoendelea na Makala hii utaona kweli kusambaza upendo ni kitu muhimu sana. Sasa hapa chini nimekuwekea vitu vya kufanya kama hauna pesa na una mdoto kubwa.

1. Anza kufanya biashara ndogo ndogo
Mara nyingi utakuta kwamba ndoto yako inahitaji pesa ya kutosha. Na wewe unaweza ukawa kabisa hauna pesa au una kiasi kidogo kiasi hata ukianza kwa kiasi hicho hutaweza hata kufikia katikati ya ndoto zako. Katika nyakati kama hizi basi utapaswa kuchagua biashara ndogo ndogo ambazo utatoa thamani kwa watu na kupata hela. Unaweza kufanya hizi kwa muda kisha ukapata hela ya kutosha na ukaamua kuingia moja kwa moja kwenye utimizaji wa ndoto zako kubwa.

Anzia chini panda juu
Kuna usemi wa kiingereza unaosema kwamba dream big but start small. Ukimaanisha kwamba kuwa na ndoto kubwa ila kuwa tayari kuanza kidogo. Kuwa tayari kuanza na kile ulicho nacho huku unakikuza zaidi. Yaani unataka chini kuelekea juu. Vitu vidogo huwa vinatoa mambo makubwa ambayo watu hawategemei kabisa. Mbuyu ni mti mkubwa ila mbegu yake ni ndogo. Ukiiona mbegu ya mbuyu huwezi kuona uwezekano wa mbegu hiyo kutoa mti mkubwa. Lakini uwezo wake huwa unajidhirisha kadri muda unavyosogea. Na wewe utaweza kutimiza ndoto zako, ni suala la muda tu.

Jitume sana
Utahitaji kuweka nguvu katika kutimiza ndoto yako. Wafanyabiashara wengi na watu waliofikia hatua kubwa kimasisha wanasema wazi kabisa kwamba mwanzo ni mgumu. Na katika kipindi hiki lazima utapaswa kufanya kazi kwa bidii na kujituma kwa bidii kubwa. Kama unakaribisha ukawaida basi utaendelea kuwa wa kawaida ila kama umepanga kufanya vitu vya tofauti lazima uwe tayari kufanya vitu katika namna ya utofauti. Na hivyo kufanya kazi kwa bidii hakuepukiki. Katika kipindi hiki usemi wa Waziri Mkuu wa uingereza Winston Churchill  wa damu, kuteseka, machozi na damu ndipo haswa unatumika.

Kumbuka ukitoa jasho jingi sana wakati wa mazoezi utatoa damu kidogo wakati wa vita.
Ukitoa jasho jingi wakati wa ujana, utaondoa mateso yatakayokupata wakati wa uzee.

Usitarajie tu kwamba ndoto yako itatimia wewe ukiwa umelala kitandani. Katika kitabu chake cha DESTINY mwandishi T. D. JAKES anakazia msumari kwa kusema, usikae tu kwenye sofa na kusema ONE DAY YES! Ndio itakuja siku ambapo utafikia hatua kubwa lakini unapaswa kufanya kazi kwa bidii ili kufikia huko.

Kubali kuanza kuifanyia kazi ndoto yako leo. Kubali kuifanyia kazi haswa. Anza sasa hivi.

Umekuwa nami,
Godius Rweyongeza
0755848391
KUPATA KITABU CHA KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI BONYEZA HAPA

HUDUMA NYINGINE UNAZOWEZA KUPATA KWANGU HIZI HAPA
Hakikisha umesubscribe kwenye YouTube Channel Yangu Ya Youtube Kwa Kubonyeza Hapa


One response to “Kitu cha kufanya pale unapokuwa na ndoto kubwa inayohitaji pesa na wewe hauna pesa.”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X