LIPA GHARAMA
Ili kweza kufikia mafanikio makubwa kwenye kutimiza ndoto zako basi moja ya kitu ambacho utapaswa kufanya ni kulipa gharama. Hii haijalishi kwamba wewe ni ndoto yako ni kuwa baba bora au mama bora, au iwe ni kufikia viwango vya juu katika mchezo fulani. Kwa vyovyote vile gharama bado haitaepukiki
Na hapa ninapozungumzia gharama kinachokuja kwenye akili yako basi kinaweza kuwa ni kulipa pesa peke yake. Japo kwa vitu vingi gharama unazopaswa kulipa ni gharama ya pesa ila kwako wewe kuweza kufikia ndoto zako utahitaji kulipa zaidi ya gharama ya pesa. Kuna nyakati utapaswa kulipa gharama za pesa peke yake. Pia kuna nyakati ambapo utapaswa kulipa gharama ya pesa pamoja na vitu vingjne na hizi gharama nyingine ndizo ningependa uzifahamu siku hii ya leo.
1. gharama ya muda
2. gharama ya kujifunza
3. gharama ya kuachamna na baadhi ya vitu. Kuna baadhi ya vitu ambavyo unavipenda sasa hivi. Utahitaji kuachana navyo ili tu uweke muda wako na nguvu zako kwenye kutimiza ndoto zako na malengo yako ya muda mrefu.
4.gharama ya kufanya kazi kwa bidii. Kumbuka kwamba kuna kufanya kazi na pia kuna kufanya kazi kwa bidii. Hi ndio kusema kwamba utapaswa kufanya kazi zaidi ya uluvyozoea. Utapaswa kuweka juhudi zaidi ya vile ambavyo umezoea na uta[aswa kufanya kazi masaa mengi zaidi ya ulivyozoea.
5. gharama ya kujifunza
6. gharama ya pesa yenyewe.
Baada ya kuzijua gharama ambazo utapaswa kulipa ili kuweza kufikia ndoto zako hapa una vitu ambavyo utapaswa kuvifahamu katika kutimiza ndoto zako.
1.Kila ndoto yako uliyonayo leo hii itatimia ila unapaswa kuwa tayari kulipa gharama
2. sehemu pekee ambapo unaweza kunywa na kula kabla ya kulipa gharama ni kwenye mgahawa au hotelini. Ila kwenye maisha na kutimiza ndoto zako basi utapaswa kulipa gharama kwanza kabla kupata kile ambacho unakitaka
3. ukiona watu waliofanikiwa kimaisha unapaswa kujua kwamba watu hawa walilipa gharama kuweza kufika hapo walipofika. Na wewe unapaswa kuwa tayari kulipa gharama ili kuweza kufika hapo walipofika au kwenda zaidi ya hapo.
4. kadri ndoto yako inavyokuwa kubwa ndivyo unapaswa kulipa gharama kubwa Zaidi.
5. lipa gharama mapema. Kuna usemi kwamba muda mzuri wa kupanda mti ulikuwa ni miaka kumi iliyopita ila muda mzuri zaidi wa kupanda miti ni leoo hii. Vivyo hivyo kwenye kutimiza ndoto zako. Muda mzuri wa wewe kutimiza ndoto zako ulikuwa ni miaka kumi iliyopita ila muda mzuri izaidi wa wewe kutimiza ndoto zako ni leo hii.
6. unaruhhusiwa kuchukua njia za mkato kwenye kutimiza ndoto zako ila fahamu kwamba hazitakufikisha kwenye mafanikio unayotaka na wala hazitakufanya upate mafanikio ya kudumu.
7. utapaswa kufanya kazi yako vizuri zaidi kiasi kwamba kama kuna mtu ambaye anafanya kitu kama cha kwako aje kwako kujifunza namna kinavyofanyika. Na wakati yeye anajifunza kwako wewe unakuwa unachukua hatua zaidi kufanya vizuri zaidi..
8. ili uweza kufikia ndoto zako utapaswa kutoa pia sadaka. Kwanza ufahamu kwamba kila kitu ambacho umewahi kufikia maishani kuna sadaka ambayo uliitoa. Iwe unaona umetoa sadaka au la! Hakuna kitu cha bure na wala dunia haijawahi kufanya hivyo.
Kama kweli umejitoa kuhakikisha kwamba unafanikisha ndoto zako na kufikia viwango vikkubwa maishani mwako basi unapaswa kufahamu gharama ambazo utapaswa kulipa ili kuwea kufika huko uendapo. NAKUKUMBUSHA TU. Kila kitu ambacho unataka leo hii kina gharama yake ambayo utapaswa kulipa. Je, upo tayari kuilipa?
Umekuwa nami,
Godius Rweyongeza
0755848391
KUPATA MAKALA MAALUM KWA WATU MAALUM KILA WIKI BONYEZA HAPA