Kitu Hiki Kimoja Huwezi Kujifunza Kwenye Vitabu


Rafiki yangu kwa siku sasa nimekuwa nakusisitiza juu ya usomaji wa vitabu. Na kitu hiki ni muhimu sana kwako ili uweze kusoga mbele kimaisha. Hata hivyo kwenye kusoma vitabu kuna kitu kimoja ambacho inaonekana kabisa bado hujakifahamu. Kitu hiki ni kwamba hutakikuta kwenye vitabu. Na kitu hiki ni KUCHUKUA HATUA.

Ujue unaweza kuwa unasoma vitabu lakini bado ukawa huchukui vitabu. Vitabu vinaweza kukwambia kwamba unapaswa kuchukua hatua za hatari lakini wewe hata ukawa kabisa huchukui hatua hizi hapa. kitu hiki kitakufanya ukwame bila kujali kwamba wewe unasoma vitabu vingapi kila siku.

Kazi kubwa inayofanywa na vitabu ni kukuweka kwenye njia sahihi. Lakini vitabu havikufanyi uitembee hiyo njia. Hivyo jukumu la kuitembea hiyo njia ya mafanikio lipo juu yako.

Kama bado hujanielewa vizuri hapa naomba uchukulie mfano wa mama na mtoto wake anayeumwa. Ni ukwelil kwamba mtoto anayeumwa anakuwa anahitaji huduma kutoka kwa mama. Kitu kikukbwa ambacho mama yake anaweza kufanya ni kuhakikisha kamba anampa mtoto wake kidonge.

Ila sasa unakuta kwamba mtoto mwenyewe anakuwa kabisa hataki hicho kidonge. Hivyo mama anamshika pua huyo mtoto na kumlazimisha kunywa dawa (pengine baada ya kuikoroga). Lakini mama akiachia pua, basi huyo mtoto anatema, hiyo dawa.

Hii ndio kusema kwamba huyu  mtoto ataendelea kuumwa hata kwama ameonja dawa kidogo. Maana suluhisho la ugonjwa sio kuweka dawa mdomoni bali ni kunywa dawa kabisa.

Sasa hiki ndicho kitu ambacho kinatokea kwako kama utasoma vitabu bila kuchukua hatua kila siku. Unakuwa sawa na mtoto anayeonja dawa na kuitema baada ya kuwa ameachiwa mdomo wake. NIKUOMBE KITU KIMOJA MUHIMU SANA KUANZIA LEO. Na kitu hiki ni KUCHUKUA HATUA JUU YA KILE UNACHOJIFUNZA KWENYE VITABU.

Nikukumbushe tu kuwa vitabu vinaweza kukuweka kwenye njia sahihi, lakini vitabu hivi havitahusika na wewe kuweza kutembea njia hii ambayo ni sahihi.
Rafiki yangu siku hiii ya leo umekuwa na mimi ambaye ninajali mafanikio yako.
Godius Rweyongeza
0755848391

,

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X