Mambo 20 Ya Kufanya Kwa Siku 340 Zilizobaki Kabla Mwaka Huu Kuisha


Siku ya leo sitaki niandike sana, ila hapa kuna mambo 20 ambayo unapaswa kufanya kwa siku 340 zilizobaki ili kuufanya mwaka huu kuwa mwaka wa mafanikio makubwa sana.

1. Hakikisha unakuwa na notebook ambapo kila siku utaangalia mwenendo wako. huku utaandika mambo yako unayofanya kila siku. Hii pia itakupa urahisi wa kujifanyia tathimini kila mwisho wa mwezi.

2.  Walau mara moja kwa wiki fanya kitu ambacho unaogopa kufanya.

3. Anzisha biashara ambayo umekuwa unafikiri kwa siku nyingi sana kuanzisha ila hujawahi kuanzisha.

3. Soma kitabu cha KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI (hard copy)

4. Angalia video ya uzinduzi wa iphone mwaka 2007 ya Steve Jobs.

5. Washukuru watu ambao wanakusaidia kusonga mbele. Hata kama ni kwa hatua chache.

6.  Tembelea Songambele blog kila siku. (www.songambeleblog.blogspot.com

7. Soma  kitabu cha YUSUFU, NINA NDOTO cha Edius Katamugora.

8. Tembelea youtube channel ya GODIUS RWEYONGEZA kujifunza masomo mbalimbali. https://youtu.be/ZK5iBKkIdp0

9. Usipitishe siku bila kusikikiza muziki unaoupenda.

10. Tumia kanuni ya pomodoro kwenye kazi zako za kila siku.

11. Usianze siku yako kwa kutumia simu na wala usimalize siku yako kwa kutumia simu. Anza na malengo yako, maliza na malengo yako.

12. Nenda kwenye channel Ya LAZARO SAMWELI uangalie video zake kila siku.

13. Wafanye wengine wafanikiwe badala ya kutaka, ufanikiwe peke yako.

14. Angalia video ya STEVE JOBS akiwa chuo kikuu cha Stanford.

15. Weka biashara yako mtandaoni.

16. Tabasamu, tabasamu. Ebu tabasamu sasa hivi.

17. Usizuie vitu vinavyotokea kwa asili kutokea. Mfano usizuie kucheka pale unapopaswa kucheka.

18. Tembelea website ya Jacob Mushi.

19. Soma, kitabu cha Deo Kessy Cha Ongea Lugha Yako.

20. Jiandikie barua mara moja kwa mwezi kujipongeza kwa hatua ambazo umefanya ndani ya mwezi husika. Kwenye barua hiyo jiambie vitu ambavyo utapaswa kufanya ili ufanikiwe zaidi. Najua hujawahi kufanya hivi ila ukifanya hivi mwezi huu, utashangaa. Naomba kwenye hili  hapa ukimaliza kulifanya nitafute kwa namba yangu uniambie umejisikiaje baada ya kujiandikie barua.

NA KUMBUKA HAPA NAMAANISHA BARUA YA KUANDIKA KWA MKONO!!

21. Hudhuria walau semina moja kila mwezi. Semina ambayo itakufundisha kitu ukichokuwa hujui.

22. Kuwa tayari kulipa gharama, kuna gharama saba utapaswa kulipa mwaka huu ili ufanikiwe. Gharama hizi zote utazikuta kwenye kitabu cha TIMIZA NDOTO ZAKO. (Kama tayari umesubscribe kwenye channel ya GODIUS RWEYONGEZA) nitumie screen shot ikionesha umefanya hivyo ili nikupe zawadi ya kitabu hiki bure badala ya 5,000 ambayo ni gharama yake ya kawaida. Hii zawadi inadumu kwa maasa 6 tu kutoka sasa. Mwisho ni saa tisa mchana.

 Usisahau pia kushare na wengine walau wawili unaowapenda.

Ni mimi ninayejali mafanikio yako.
Godius Rweyongeza

Whatsapp namba yangu ni hii hapa; 0755848391
Barua pepe; songambele.smb@gmail.com


One response to “Mambo 20 Ya Kufanya Kwa Siku 340 Zilizobaki Kabla Mwaka Huu Kuisha”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X