Siku 100 Za Kwanza Za Mwaka 2020 Zimeisha: Mambo 100 Unayoweza Kufanyia Kazi Kwa Siku 266 Zilizobaki


 

Tarehe 1.1.2020 dunia nzima ilishangilia mwaka mpya. Shangwe kutoka kila kona ya dunia zilitawala. Kuna watu siku iliyotangulia tarehe 1 hawakulala wakiusubiri mwaka mpya ufike. Kuna watu walikuwa na mipango mikubwa sana ya kufanya mwanzoni mwa  mwaka huu. Kuna watu ambao siku ya mwaka mpya ilipofika walijiambia kwamba haiwezi kupita hivi hivi tu, lazima nifanye kitu na kweli siku hiyo walifanya kufanya kitu. Leo hii hii ni siku ya 100 tangu mwaka huu uanze, swali langu kwako ni je, ile mipango yako ya mwaka huu bado unayo? Je, malengo yako yako wapi au ndio tayari umeshapotezea kapuni. Kama umeyapoteza maana yake tayari mpaka sasa hivi unaishi maisha ya kawaida sana.

 

Leo nimekuandalia vitu 100 ambavyo utaanza kufanyia kazi kuanzia leo hii kwa siku266 zijazo.

 

1. kwa siku hizi 266 zilibaki hakikisha unafanya kitu cha tofauti. Huwezi kupata mafanikio kwa kufanya kitu ambacho kila mu anafanya. Japo kwa kufanya hivyo hutakosea, lakini hutapata matokeo makubwa. ila ukifanya kitu cha tofauti utakosea na nafasi yako kufanikiwa itakuwa ni kubwa.

2.   tenga muda wa kujifunza na kuchukua hatua kwa kile ambaho unajifunza. Fahamu kwamba kama bado unapumua una mambo mengi ya kujifunza

3. walau kila wiki, ongeza watu kwenye mzunguko wako. Toa dakika chache uwapigie watu ambao umekuwa unaogopa kuwapigia na uanzishe uhusiano mpya na hao watu

4. mtu akifanya kitu kizuri msifie. Usisubir mpaka siku atakapoaga dunia ili uje uanze kusema kwamba alikuwa ni mtu  mzuri. Haitsaidia, maana atakuwa hakusikii.

5. mtu akikosea samehe. Unafanya hivyo sio kumridhisha yeye, bali kwa manufaa yako mwenyewe.

6. shukuru kwa yote. Mvua ikinyesha shukuru, jua likiwaka shukuru pia.

7. fahamu kuwa kuna vitu vipo ndani ya uwezo wako na kuna vitu ambavyo vipo nje ya uwezo wako. Shughulika sana na vile ambavyo vipo ndani ya uwezo kisha achana na vile ambavyo vipo nje ya uwezo wako.

8.  ndugu zako ni watu muhimu sana. kila siku ishi nao kama vile ndio siku ya mwisho. Hivyo kama kuna kitu ambacho ungependa kuwafanyia, kifanye leo.kama kuna kitu ungependa kuwambia, kiseme leo

9. kama kuna mtu unampenda mwambie, kama kuna tabia unapenda kuanza kuiishi, anza kuiishi, kama kuna kitu ungependa kujifunza anza kujifunza na kama kunakitu ungependa kuanzisha basi kianzishe..

10. kama mwaka huu utapaswa kusahau, basi sahau vitu vingine ila usisahau malengo yako

11. malengo huwa hayafanikishwi ndani ya siku moja,bali ni hatua moja inayojengwa juu ya hatua nyingine

12. fahamu kwamba safari ya maili elfu  moja huanza na hatua moja

13. usianze siku yako kama myama na kumaliza siku yako kama myama.

13. usiendeshe maisha yako kama myama, maisha haya yana kanuni zake. Na kanuni hizi hazibadiliki.

14. ukiwa na kusudi kubwa la maisha hakuna kitu ambacho kinaweza kukuzuia. Ukiwa huna kusudi lolote, kila kitu kitakuzuia hata kama ni ukungu.

15. ukiamka asubuhi soma kitabu, mchana soma kitabu, jioni soma kitabu

16. leo hii ingia google na uandike jina lako. Kama kile kitakachotokea utakuwa hukipendi basi azimia kukibadili ili jina lako liweze kuonekana kwa sura ya tofauti watu wanapolitafuta google.

17. kama unataka kubadili dunia, anza kwa kutandika kitanda chako. Huwezi kubadili dunia wakati unashindwa kutumia vizuri mazingira ambayo yamekuzunguka.

18. ukikutana na mtu, usimwache kama ulivyomkuta. Azimia kwamba lazima utamwinua kidogo na kumfanya awe  bora zaidi ya ulivyo mkuta

19. badili zawadi zako ambazo umekuwa unatoa. Zamu hii ukitaka kutoa zawadi basi mununulie mtu kitabu na umtumie.

20 Soma kitabu cha Kutoka Sifuri Mpaka Kileleni

21. kama kuna mtu ambaye ungependa abadilike, usimlazimishe kufanya hivyo. Wewe kwanza kuwa chachu ya mabadiliko hayo na yeye ataona  mfano na kufuata. Kumbuka kwamba penye mwanga hakuna giza.

22. usiwe mtu wa kufikiri kwa uhaba. Ni dhambi kufikiri kwamba fulani akifanikiwa basi mafanikio yako atakuwa ameyachukua. Utajiri, fedha na mafanikio vipo vya kutosha kwa kila mtu ambaye anavihitaji.

23. ukiona mtu ana gari zuri, mbariki mtu huyo, ukiona mtu ana familia nzuri mbariki huyo mtu na familia yake, ukiona mtu amesoma na anajua vitu mbariki hyo mtu na vitu vyake. Huwezi kupata kitu ambacho unakilaani.

24.ukiona vyaelea jua kabisa kwamba vimeundwa.na wewe ukitaka vielee, basi viunde.

[mailerlite_form form_id=1]

25. maisha yakikupa limau, wewe tengeneza juisi ya limau

26. fahamu kuwa mjinga wakarne ya 21 sio yule ambaye hajui kusoma na kuandika, bali mjinga wa karne ya 21 ni yule ambaye anajua kusomana kuandika ila HASOMI

27. kuwa basi mbunifu kwenye vitu ambavyo unafanya na kuviongezea thamani

28. fahamu kuwa ule usemi wa mababu zetu walikuwa wanafanya hivi umepitwa na wakati. Sasa hivi tupo kwenye zama nyingine, wao walifanya walivyokuwa wanafanya, sasa hivi tunafanya kivingine.

29. kuwa mtu ambaye anafunguka na kuwa tayari kupokea mawazo mapya. Ukiendelea kushikilia mawazo yako bila kubadilika, ni wazi kuwa utaendela kupata matokeo ambayo umekuwa unapata.

30. Soma JINSI YA KUIBUA UBUNIFU ULIO NDANI YAKO kilichoandikwa na Godius Rweyongeza

31. kama kuna ujuzi unapaswa kujifunza basi jifunze kuandika, unenaji (public speaking) na mauzo na masoko (sales and marketing)

32. kwa kitu chochote kile ambacho kinatoka mikononi mwako,au kitu ambacho akili yako inahusika, au miguu yako inagusa basi hakikisha kimefanyika kwa viwango vikubwa

33. chagua walau kitu kimoja ambacho utajifunza mtandaoni kwa siku hizi zilizobaki na kukielwa kiundani. Kinaweza kuwa ni lugha mpya, ujuzi, n.k

34. amua kutumia mitandao ya kijamii kwa manufaa yako kuanzia leo hii.

35. usiingiie mtandaoni asubuhi unapoamka. Huu ni muda wako wa kutumia akili yako kwa mambo makubwa na yanayohitaji akili kubwa.

36. nunua notebook ndogo ambayo utakuwa unaandika mawazo yanayokujia kila siku. Mawazo huwa yanakuja na kupotea, usikubali wazo lako lipotee kwasababu hauna sehemu nzuri ya kulweka.

37. ukitaka kulipwa mara 2 zaidi ongeza viwango vyako mara 3 zaidi

38. maisha yakiwa magumu fahamu kuwa huo sio mwisho wa dunia bali mwanzo mpya.

39. Ukikutana na changamoto,basi jua hicho hilo ni tuta na safari inaendelea.

40. Soma kitabu cha NYUMA YA USHINDI kuna kushindwa, kushindwa, kushindwa

41. ukianguka, simama, ukianguka basi angukia mbele, ukianguka basi toka na kitu chini ila usikubali  kuishia hapo.

42. kama huwezi kupaa basi kimbia, kama huwezi kukimbia wewe tembea, kama huwzi kutembea tambaa. Kwa vyovyote vile usikubali kuwa vile vile wakati wote.

43. ukiona umeanza kusema kwamba bora ya jana. Basi ujue wazi kwamba kuna kitu hufanyi vizuri. Maana kila siku inapaswa kua bora zaidi ya ilivyokuwa jana

44.ukiona watu hawakuchangamkii, juwa wewe huwachamgkii unapata ulichotoa. Ukitaka tabasamu, toa tabasamu kwanza.

45. dunia hii inaendeshwa kwa kanuni za asili. Na moja ya kanuni hizo ni kuwa utavuna ulichopanda

46. kanuni nyingine inasema kwamba, kila kitu kitaendelea kuwa kwenye mwendo wake mpaka pale nguvu ya ziada itakapotokea.

47. kanuni nyingine inasema kwamba, kitu kinapokuwa kwenye hali yake ya kawaida na na moja vitu vinavyokiweka kitu hicho kwenye hali yake ya kawaida vikabadilishwa. Ukawaida wake utabadilika ili kuendan na mabadiko mapya. Hiki kinawakuta watu wengi sana kwenye fedha. Kuna watu hali yao ya kaiwaida linapokuja suala la fedha ni kupokea malaki. Saa inapotokea akaingiza mamilioni basi anajikuta hatulii mpaka hayo mamilioni yaishe ili arudi kwenye hali yake ya kawaida ya akuingiza malaki yake.

48. kanuni nyingine inasema kwamba viungo vya mwili ambavyo huwa vinatumika huwa vinaimarika zaidi wakati vile ambavyo huwa havitumiki  huwa vinakufa na kupotea. Vivyo hivyo kwa kipaji na uwezo wako. Ukitaka kupoteza kipaji chako, usikitumie. Ukita kiwe bora zaidi, kitumie zaidi. Kipaji hakitumiki kikaisha, kadri unavyokitumia ndivyo unavyopata zaidi.

 

49.  Mtu akikutukana, mchukulie kama mtoto mdogo, kisha endelea na maisha yako.

50. tembelea www.songambele.co.tz kila siku

51. hakikisha unaowapenda wote wanajua kuwa unawapenda.

52. ukiwa na watu sikilza zaidi ya unavyoongea.

53. ule usemi wa hakuna haraka barani mwisho wake sekunde iliyopita. kuanzia sasa hivi anza kufahamu kuwa kuna haraka barani afrika

54. ukipanga kukutana na mtu basi mwambie muda  ambao utakutana naye. Akichelewa kwa dakika 15 unaruhusiwa kuondoka maana mtu hyo ameenda kinyume na makubaliano.

55. kama unataka kufika mbali acha na kuhangaika kuwaridhsha watu. kama unataka kuishia hapo ulipo basi mridhishe kila mtu.

56. usilipe ubaya kwa ubaya. Ubaya unalipwa kwa wema na

57. andika orodha ya vitu 101 ambavyo utafanya kabla hujafa. Na anza kuvifanyia kazi

58. soma vitabu vinavyozungumzia fedha walau 8 kwa miezi liyobaki

[mailerlite_form form_id=2]

59. jifunze namna ya kutengeneza fedha, kutunza fedha na kufanya fedha ikufanyie kazi zaidi.

60. SOMA KITABU CHA JINSI YA KUFIKIA NDOTO ZAKO kilichoandikwa na Godius Rweyongeza

61. kama unafanya kitu ambacho kinahusisha watu, wape lengo lako mapema. Na waambie waiwasilishe kazi hiyo kabla ya tarehe husika. La sivyo utaumia bure ukisubiri mpaka tarehe ya mwisho.

62. weka fedha ya kutumia kwa ajili ya sherehe au kujirusha, sio siku ya sikukuu unatumia akiba yako.

63. walau mara moja kwa mwezi  ungana na watu ambao watakuhamisha ili upige hatua zaidi.

64. huhitaji kuwa na jina ili kuanza, unahitaji kuanza ili kuwa na jina. Huhitaji kuwa na fedha ili kuanza, unahitaji kuanza ili kuwa na fedha

65. watu walio wengi hawawezi kukuzuia. Mvua kubwa haiwezi kukuzuia, ni wewe tu unayeweza kujizuia.

66. kama watu milioni wamekosea juu ya jambo fulani, WAMEKOSEA TU. wingi wa watu huwa haufanyi kitu kuwa sahihi.

67. unapogundua kuwa una nguvu kubwa ndani yako, maisha yanaanza. Wewe hapo una nguvu yakuponya magonjwa, una nguvu ya kuvuta utajiri na nguvu ya kukufanya mkuu.

68. watu wapo tayari kukusaidia kama utakuwa muwazi na kuwaeleza kilicho ndani yako

69. fanya mazoezi sana huko nyuma ya pazia. Ila ukija kuonekana mbele ya watu ionekane  kama vile ulizaliwa unajua kila kitu.

69. usifanye na kutimiza majukumu yako kwa sababu kuna mtu ambaye muda wote anakuangalia na kukufatilia. Jijege katika namna ambayo unaweza kufanya kazi kwa viwango vile vile akiwepo msimamizi na asipokuwepo.

70. soma kitabu changu cha MITAJI 8 ILIYOKUZUNGUKA NA JINSI YA KUITUMIA

71. sema kidogo, fanya sana. matendo yako yaongee zaidi ya maneno yako.

72.usisubiri kupata ruhusa ili uanze, anza na ikitokea umekosa utaomba msamaha. Ila usipokosea utaendelea mbele. Ni boa kuomba msamaha kuliko kuomba ruhusa.

 

73. kuna watu ambao kama hutawafuatilila, basi kazi yako hawataifanya kabisa au  wataifaya chini ya kiwango. Wajue watu wa namna hii na weka mpango wa kuwafuatilia.

74. hakikisha mwaka huu umeanzisha biashara hata kama itaonekana ni ya kijinga. Kwa namna hii utaweza kupata chanzo kingine cha kipato mwaka huu.

75. unapokuwa na lengo kubwa na lenye umuhimu, usipoteze muda wako kwenye mambo madogo madogo.

76. kuwa mtu ambaye yupo tayari kupokea fursa mpya. kumbuka kwamba fursa huwa haziji kwa kupiga kelele. Wala haziji zikiwa na mhuri wa FURSA.

SOMA ZAIDI: MAiSHA NI FURSA: ZITUMIE ZIKUBEBE. Zipuuze Zikukikimbie

77. kama mpaka sasa hivi, hujaanza. Kuna vitu vitatu ambavyo unaweza kufanya

Moja anza na kile ulichonacho

Fanya kinachowezekana

Mwisho wa siku utajikuta unafanya yasiyowekana

78. jisikilize wewe zaidi ya unavyowasikiliz watu wengine

79 . ifanye kazi yako kwa ubora sana, ithamini na waambie watu wakulipe kwa kazi hiyo ambayo unayoifanya. Usipowaambia hakuna mtu ambaye atajua hilo.

80.  SOMA MAMBO 55 YA KUZINGATIA KABLA YA KUANZISHA BIASHARA

81. teknlojia inabadilika kwa kasi sana. hivyo kuwa na muda wa kujifunza kuhusu mabadiliko yanayotokana na teknolojia walau mara mbili kila wiki.

ANGALIA: JINSI YA KUDANDIA TEKNOLOJIA MPYA

82. kuwa na mipango ya muda mrefu, itakuepusha na kelele za muda mfupi

83. kabla hujaanza kukimbia kutafuta nje  ya hapo ulipo, hakikisha umenzia hapohapo ulipo. Kuna vitu vingi vizuri vipo hapo ulipo. Siku zote watu huwa wanaona vitu vya mbali yao kuwa ni vizuri wakati walipo kuna vizuri zaidi.

84. siku zote tafuta kuwainua watu wengine

85. siku zote utapata kile ambacho unatafuta.  

87. mafanikio yatakuja ila sio ndani ya siku moja, utakutana  kwanza na changamoto, utakwama. Lakini ukionesha kwamba unayahitaji mafanikio kama ambavyo unahitaji kupumua, yatakuja tu.

88. kama hujiamini wewe mwenyewe, usitegemee kwamba kutakuwa na mtu wa kukuamini.

89. kama unataka kujenga ghorofa anza kuweka tofali moja

90. soma kitabu cha TATIZO SI RASILIMALI ZILIZOPOTEA

91. watu wapo tayari kukusaidia kama utaanza kujisaidia. Wanasaidia anayejisaidia

92. fedha haiendi kwa watu ambao wanaitaka, fedha inaaenda kwa watu ambao wanafaamu kanuni za fedha na kuziishi. Hivyo wekeza kwenye kujifunza kanuni hizi za fedha.

94. Usijilinganishe na watu wengine, jlinganishe na wewe wa leo na yule wa jana au mwaka jana.

95.kadri unavyokutana na watu wengi ambao wanakukataa ndivyo unakutana na wengi wanaokukubali.

96.  mwaka mpya sio lazima uanze tarehe moja, mwaka mpya unaanza siu ile unapoweka malengo yako na kuanza kuyafanyia kazi

97. Soma kitabu cha THE SECRET OF THE MILLIONAIRES MIND

98. soma kitabu cha sapiens: a brief history of humankind

99. kuwa na kitu ambacho kila siku utakifanya hata kwa udogo bila kukosa, labda kuamka mapema kila siku, kuandika kila siku kama mimi, kuandika kwenye diary yako kila siku mambo muhimu uliyojifunza kwa siku hiyo, kufanya mazoezi, kuadaa chakula bora n.k.

Kikubwa ni kwamba uwe na kitu kimmoja ambacho unaweza kujivunia kwamba unakifanya kila siku kwa siku 266 zilizobaki.

100. ANZA KUANDIKA KITABU CHAKO.

 

 

Rafikiyangu kwa kumalizia ni kwamba kila kitu huanzia sifuri. Lakini huwa hakibaki kikiwa hapo hapo kwenye sifuri. Mtoto huanza na miaka sifuri hukua na kufikisha miaka 70 mpaka 100.

Gwiji wa mpira unayemwona kuna siku alikuwa hajui kitu kwenye mpira (alikuwa sifuri) ila leo hii ni mtaalmu mzuri wa mpira. Kampuni lolote kubwa ulalolifahamu ni kwamba lilianzia sifuri mpaka leo hii umeweza kulifahamu. Wewe pia unaweza kuanzia sifuri na kufanya makubwa maishani mwako.

Kinachowawamisha watu wengi wasianze safari kwenye maisha yao ni kwamba wanasubiri pale watakapokuwa wamekuwa na makubwa. na kinachotokea ni kwamba makubwa haya huwa hayatokei. Ukitaka kupata  makubwa unaanza na kile ulichonacho, unafanya kinachowezekana na mwisho wa siku unakuwa na uwezo wakufanya yasiyowezekana

 

Mimi nakutakia kila la kheri

Makala nyingine zinazoenda na hii

Mambo 20 Ya Kufanyia Kazi Kwa Siku 340 Zilizobaki Mwaka Huu Kuisha.

IKO WAPI MOTISHA YA JANUARI MOSI?

 

Umekuwa nami

Godius Rweyongeza

0755848391-Morogoro


One response to “Siku 100 Za Kwanza Za Mwaka 2020 Zimeisha: Mambo 100 Unayoweza Kufanyia Kazi Kwa Siku 266 Zilizobaki”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X