BADILI MAJI KUWA DIVAI: Jinsi Ya Kuona Fursa Katika Changamoto Unazokutana Nazo Masihani


Nimeona niseme hiki kitu, ili usije kusema kwamba sikusema.
Usije kusema kwamba sikusema kwamba fikra zako ndizo zinazalisha matokeo unayopata.
Watu wawili wanaweza kuwa wanapitia katika hali  ileile, ila mmoja akawa ameiona kama fursa ya yeye kusonga mbele. Wakati mwingine akaona kwamba ni kikwazo. Mmoja akaona kwamba ni upenyo wake wa kufanya makubwa mwingine akaona kwamba huo ndio mwisho wake na hapo hataweza kutoboa.
Ujue matatizo huwa yanafanya baadhi ya watu wanavunje rekodi na wengine kuvunjika. Sasa wewe upo upande gani? Upande wa kuvunja rekodi au kuvunjika?
Iko hivi watu wawili wanaweza kuwa wanapitia katika hali moja ila mmoja akawa amepata funzo na kulifanyia kazi na kupata matokeo makubwa na mwingiine anaweza kuona kwamba huo ndio mwisho wake wa kufanya  hicho kitu, hivyo kuishia hapo. Ndio maana nikasema kwamba matatizo huwa yanawafanya baadhi ya watu wanavunja rekodi na wengine wanavunjika.

Kuna vijana wawili ambao walilelewa baba mmoja ambaye alikuwa mlevi. Vijana hawa walikuwa wanateswa na baba yao kila alipokuwa anarudi kutoka kunywa pombe.  Walipokuwa watu wazima kijana mmoja akawa mfanyabiashara na mwingine akawa mlevi. Siku moja mwandishi wa habari alitaka kujua ni kitu gani kilimsukuma kila mmoja kuwa jinsi alivyo.
Mwandishi wa habari, alimfuata kijana yule mfanyabiashara na kumwuliza, “hivi ni kitu gani ambacho kimekusukuma na kuwa mfanyabiashara” kijana yule mfanyabiashara alijibu na kusema, “ NI BABA YANGU”. Kijana yule alijibu kwa kuendelea kusema kwamba, “nilipoona kwamba baba yangu analewa nikaona kwamba hayo sio maisha ambayo binafsi ninapaswa kuishi, niliona kwamba ninapaswa kubadili maisha ambayo ninasihi. Na hivyo nikaona kwamba ni vyema niihudumie jamii kwa kufanya kitu ambacho kitaongeza thamani kwa jamii”
Kijana yule aliendelea kwa kusema kwamba, “ nilipokuwa mdogo niliona baba yangu akipeleka pesa nyingi kwenye baa kwa ajili ya kunywa pombe, na wale wamiliki wa baa walikuwa wafanyabiashara ambao kipato chao kilikuwa kinaongezeka kila siku, kila  mwezi, na kila mwaka. Wakati sisi nyumbani tulikuwa tunakosa hata pesa ya kula, hivyo nikaona kwamba katika maisha nitapaswa kuwa mfanyabiashara ili niweze kukusanya pesa za watu wngine na kuzivuta kwangu” hivyo ndivyo alimalizia maongezi yake kijana mfanyabiashara.
Baada ya maongezi hayo mwandishi alimfuata kijana ambaye mwingine ambaye alikuwa mlevi. Mwandishi alimuuliza swali kama lile ambalo alimuuliza kiijana wa kwanza. Alimuuliza hivi, “ ni kitu gani kilikusukuma wewe kuwa mlevi”?
Kijana yule mlevi alijibu na kusema kwamba, “ NI BABA YANGU” . alisema kwamba nilipokuwa mdogo nilimwona baba yangu akiwa analewa na hivyo mpaka leo ninajua kwamba maisha ni juu ya ulevi tu hakuna kitu kingine. Alimalizia hivyo kijana mlevi.
Kwa hiyo unaweza kuona kwamba mazingira ya aina hiyo hiyo yanavyoweza kuzalisha watu wa aina tofauti tofauti. Mazingira yale yale yanaweza kumfanya mtu mmoja avunje rekodi na mwingine kuvunjika. Je, wewe upo upande gani?
Siku zote unapaswa kuwa upande wa kuvunja rekodi. Na hapa ninaenda kukupa mbinu za kukusaidia wewe kuvunja rekodi badala ya kuvunjika kwa sababu ya hicho kitu ambacho kinatokea kwenye maisha  yako.
KWANZA; KABISA KUWA MTU WAKUONA CHANYA KWENYE HASI

Ngoja nikwambie kitu rafiki yangu, nyakati ngumu kwenye maisha huwa haziishi. Ila sasa ni juu yako wewe kuona ni namna gani unazitumia nyakati hizi katika kuhakikisha kwamba unasonga mbele.
Kwa kila baya au gumu ambalo litakutokea maishani mwako, angalia ni kwa namna gani utaweza kuona fursa kwenye hilo baya ambalo unaona au kukutana nalo maishani.  Usiliangalie tatizo kama tatizo. Badala yake angalia fursa ambazo unaweza kuziona kutokana na hilo tatizo ambalo unakkutana nalo kwa wakati husika.
Hivi kwa mfano wewe mvua ikinyesha unaona. Unaona kwamba imekukwamisha kufanya mambo yako, au ndio unaona kwamba ni fursa ya wewe kufanya kitu kikubwa zaidi.

Naipenda sana hadithi ya mwalimu mmoja ambaye alikuwa anafundisha chuo. Huyu mwalimu alizoea kuona chanya kwenye kila kitu ambacho kilikuwa kinatokea maishani mwake. Sasa siku hii mvua kubwa kweli ilikuwa inayesha huku ikiwa imeammbatana na radi, ngurumo  na upepo mkali. Wanafunzi wote darasani walikuwa wamekaa kimya na wengine walidhani kwa sababu ya hali ya hewa basi inawezekana huyo mwalimu asitokee kabisa darasani. Lakini mwalimu alitokea kwa wakati na kila mwanafunzi alikuwa na shauku ya kusikia huyo mwalimu siku hiyo atasemaje? Maana walizoea kwamba kila jambo baya kwake huwa lina uzuri au ya kufanyia kazi. Lakini leo angesemaje? Maana mvua kali iliyoambatana na radi na ngurumo pamoja na upepo mkali vilikuwa vinaendelea kwa wakati huho. Hivyo kila mwanafunzi alikaa chini kwa shauku kubwa sana akitaka kusikia maneno ya mwalimu wake.
Mwalimu alipongia darasani alitabasamu sana na kisha akasema, “ tumshukuru Mungu, maana siku kama hii huwa hazijitokezi maishani”.
Mwalimu huyu hapa alikuwa ni mtu ambaye anaona chanya katika jambo ambalo ni hasi maishani. Alikuwa anaona chanya hata ambapo watu wengine wote walikuwa wanaona kwamba haiwezekani.
Je, wewe huwa unaona nini katika changamoto ambazo unakutana nazo maishani mwako?
PILI; FANYIA KAZI KILE AMBACHO UNAONA KWAMBA UNAWEZA KUBADILI KWA SASA HIVI

Kuna magumu au mambo mabaya ambayo yanaweza kuwa yanakukumba wewe au jamii. Lakini yanaaweza kuanza kupatiwa suluhisho mara moja. Na mtu wa kufanya hivyo ni wewe mwenyewe wala sio mtu mwingine.
Ebu tuseme kwamba jamii yako inapata shida ya maji. Wewe utafanyaje? Utalalamika au utasubiri serikali ije ilete maji?  Ukiangalia kwa jicho la kipekee unaweza kuona kwamba kuna kitu ambacho unaweza kubadili hapa. unaweza kutatua tatizo la watu kwa kutafuta namna ya kuwaletea maji karibu lakini pia wewe mwenyewe ukapata maji karibu. hivyo kwa kufaya hivyo ukakutakwamba umetatua tatizo na umetengeneza biashara ambayo inakuingizia kipato.
Lakini ukiona tatizo la namna hii na wewe ukawa mtu wa kulalamika, basi ni wazi kwamba tatizo hili litakuvunja badala ya kukufanya uvunje rekodi.
TATU, KUBALI KUBEBA MAJUMUKU YAKO

Ujue kitu ambacho huwa kinafanya matatizo kuwa makubwa ni kwa sababu ya watu kutokubali kubeba majukumu yao. Watuwengi huwa wanapenda kuwabebesha watu wengine majukum. Watu wanakaa sehemu wakiwa wanaamini kwamba kuna mtu ambaye yupo sehemu fulani na huyo ndiye anahusika na kuwafanya wao waweze kuwa watu wenye furaha. Huyo ndiye anahusika kuwapa afya njema na kuwapatia kila kitu.
Kuanzia leo hii, wewe ukikutana na hali au jambo ambalo unaona kwamba linakukwamisha, basi ona ni kwa namna gani wewe umesababisha hilo tatizo . ona ni kwa jinsi gani wewe umeweza kujiingiza kwenye hilo tatizo. Anza kutafuta namna ya kukutoa kwenye hilo tatizo.
Ukigundua kwamba unaangamia basia kinachofuata inakuwa ni kwamba
NNE; ANZA KUFANYIA KAZI FURSA UNAYOIONA KWENYE TATIZO

Haitoshi tu kwako kuona fursa kwenye kitu. Au kuona kitu chanya. Bali hicho kitu chanya unapaswa kukiweka katika vitendo na kuhakikisha kwamba unakifanyia kazi katika kuleta matokeo chanya.
Rafiki yangu, siku ya leo nimeona wazi kwamba ninapaswa kukushirikisha haya nilyojifunza ili na wewe uweze kunufaika na matatizo badala ya kukaa ukilalamika kwa changamoto au matatizo ambayo unakutana nayo kila siku.
Endelea kutembelea blogu hii hapa kila siku. Lakini pia
Usikose kujiunga na mfumo wetu wa makala MAALUMU KWA WATU MAALUMU ambazo huwa zinatumwa kwa baru pepe. Bonyeza hapa ili kujiunga.
Umekuwa name anayejali mafanikio yako,
Godius Rweyongeza
Unaweza kuwasiliana nami kwa 0755848391
JIUNGE NA KUNDI LA THINK BIG FOR AFRICA ili uweze kupata mafunzo zaidi ya kukufanya usonge mbele.

Soma Zaidi Hapa THINK BIG FOR AFRICA


One response to “BADILI MAJI KUWA DIVAI: Jinsi Ya Kuona Fursa Katika Changamoto Unazokutana Nazo Masihani”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X