Wanawake Watano Walioshindwa Karibia Kwenye Kila Kitu Na Bado Wakashinda Kwa Kishindokuna usemi wa wahenga wetu wanaosema kuwa kukatika kwa jamvi sio mwisho wa mazungumzo. Jamvi linaweza kukatika na bado mazungumzo yakaendelea, tena vizuri tu.

Sasa leo, natakata niongee nawe kuhusu hili suala na hasa wewe mwanamke.
Leo nimekuandalia Makala maalumu, huku nikitaka uchukue masomo makubwa kutoka kwa wanawake walioanguka na bado wakainuka na kushinda kwa kishindo kikubwa. Lakini pia nataka nikwambie kwamba, ewe mwanamke, inawezekana.

Makala za mwanzo zinazohusiana na hii ni Kutana Na Watu Watano Walioshindwa Karibia Kwenye Kila Kitu Na Bado Wakashinda Kwa Kishindo

Sasa acha tuanze hivi:

 1. OPRAH WINFREY (67)
  Huyu ni mwanamke mwenye ushawishi mkubwa na hasa kwenye zama hizi. Historia yake ina mengi ya kusikitisha kuhamasisha. Alibakwa akiwa na umri wa miaka 9 tena na ndugu yake. na Kisha akapata mimba akiwa na umri wa miaka 14. alijifungua na mwane akaaga dunia ndani ya wiki mbili.
  kitu hiki kilimfanya Oprah aone kama vile maisha siyo fair hata kidogo. Hivyo akawa kama amekata tamaa na kuona hakuna usalama na hasa unapokuwa umezungukwa na wanaume.
  Lakini baadqye aliamua kuachana na hayo mawazo. Akaona kuwa inawezekana kufanya makubwa.
  akaingia kwenye sekta ya utangazaji na kuwa maarufu.
  ewe mwanamke, usikubali kuonekana wa kawaida. hata kama unapitia changamoto, fahamu kuwa changamoto zipo na huwa zinatokea kwenye maisha. Ila inawezekana wewe kuwa na maisha zaidi ya hayo.

SOMA ZAIDI: BADILI MAJI KUWA DIVAI: Jinsi Ya Kuona Fursa Katika Changamoto Unazokutana Nazo Masihani

 1. JK. ROWLING
  Huyu ni mwandishi maarufu wa vitabu hasa vya watoto.
  Mwaka 1995 ndio aliandika kitabu Cha Harry Potter. Kitabu hiki kilikataliwa na wachapaji 12 tofauti.
  Mchapaji mmoja tu ndiye aliyekikubali na hata baada ya kukikubali alimwambia Rowling kwamba utafute kazi nyingine maana, hutaweza kupata maisha mazuri kupitia uandishi wa aina hii.

Ila hali ilikuwa tofauti baada ya kitabu kuchapwa. kiliuza nakala nyingi mpaka kufikia mwaka 2004, Rowling akawa bilionea wa Kwanza kupata ubilionea kupitia uandishi.

Na mpaka leo hii yeye bado ni mwandishu anayelipwa sana duniani.

 1. BARBARA CORCORAN

Huyu mwanamama anaeleza jinsi alivyoolewa na mme wake. Wakawa wamefungua kampuni na baadaye wakaachana, chanzo kikubwa kikiwa ni mme wake kumpenda karani wa kampuni yao.

walivyoachana huyu mwanamama aliondoka ka asilimia 49 ya kampuni yake. Aliondoka wafanyakazi baadhi na hela dola elfu moja.

wakati wakaachana mme wake alimwambia kuwa hutaweza kutoboa bila ya mimi.

hicho kitu kilimpa hasira na akaamua kuwa kwa vyovyote vile lazima tu atoboe. na kweli alitoboa. aliweza kugeuza dola elfu moja kuwa mabilioni ya fedha.
kitabu chake cha SHARK TALES kinaeleza alivyobadili hiyo dola elfu moja kuwa mabilioni.

 1. HELLEN KELLER
  Huyu alipata upofu akiwa na umri wa miezi 19 tu.
  Ila maisha yake alivyoyaishi alifanya makubwa kiasi kwamba dunia nzima inamkumbuka mpaka leo hii.

Alikuwa mtu wa Kwanza mwenye ukipofu kupata shahada.
alikuwa mkufunzi
alikuwa mwandishi wa vitabu, kutaja ila machache.

 1. ARIANNA HUFFINGTON

Huyu mwanamama ni mwandishi wa vitabu na mwanzilishi wa jarida la HUFFINGTON post.
Kitabu chake cha pili kilikataliwa na wachapaji 36 kabla ya kuchapwa.

kwa sasa ameandika vitabu 15.

Rafiki yangu, hao ndio wanawake watano wa nguvu, chukua somo kwa mmoja wao na lifanyie kazi.

Kila la kheri.
Ni mimi rafiki yako wa ukweli
Godius Rweyongeza (Songambele)
0755848391
Morogoro-Tz
Wewe ni zaidi ya ulivyo

NB. Ofa vitabu vyangu kwa bei ya ofa: kwa punguzo la nusu bei kipindi ndani ya siku hizi mbili tu. Yaani, leo na kesho. Hii ni ofa ya siku ya wanawake.

Chagua kitabu hapa. Ofa hii inahusu vitabu vya softcopy tu.


One response to “Wanawake Watano Walioshindwa Karibia Kwenye Kila Kitu Na Bado Wakashinda Kwa Kishindo”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X