KWA siku sasa nimekuwa nikijiuliza, hivi ni mtu gani aliyesema kuwa hakuna haraka barani Afrika. Leo hii tarehe 12.4.2020 ndio nimemgundua huyu mtu aliyesema huu usemi.
Najua unajua kuwa usemi huu ndio ule usemi ambao, watu wengi huwa wanautumia kama kisingizio cha kuchelewa. mambo ya maana.
Usemi huu ndio umepelekea mpaka watu wengine kuamini kuwa waaafrika huwa wanawahi mazishi peke yake ila vitu vingine vyote wanachelewa.
Usemi huu ndio unasababisha vikao vilivyopangwa kuanza saa 10 kuanza saa 11 kwa kisingizio kuwa saa 10 ya mwafrika ndio saa 11. Sasa leo nimemjua mtu aliyesababisha haya yote. Na mimi ninaenda kumsema bila aibu ili siku nyingine ajirekebishe.
Mtu huyu ni wewe. Ndio ni wewe,
Kama wewe huwa unapanga kukutana na mtu saa 10 ila unatokea saa 11 basi wewe ndiye mhusika na sio mwingine. KWA NINI USIWAHI?
Kama wewe, huwa unaishi tu ndani ya siku bila ya kuwa na ratiba maalumu ambayo unaifuata, basi ni wazi kuwa wewe ni mmoja wa watu ambao wamesababisha falsafa hii ya HAKUNA HARAKA BARANI AFRIKA.
Sasa, basi kuanzia leo hii napenda ujirekebishe. Ndio jirekebishe kwa kufuata mambo yafuatayo.
1. Heshimu muda ambao umepanga kuwa unakutana na watu.
2. Muda mliopanga kukutana na watu ukiisha, jua kuwa umeisha. Ondoka ili uendelee na mambo mengine.
3. Kama umepanga kukutana na mtu saa 10 jioni, basi fika dakika 15 kabla.
4. Mtu huyo akichelewa, basi wewe unaweza kuongeza dakika 15. Kama ndani ya hizo dakika atakuwa hajatokea, ondoka ili uendelee na mambo yako. Kama mtu hajali muda wako, basi walau wewe jali muda wako
5. Usipange kukutana mara ya pili na mtu ambaye mara ya kwanza alishindwa kukutana na wewe kwa sababu ya kutokuwa makini na muda. Kama atahitaji kukutana na wewe mara ya pili, itabidi alipie muda wako.
6. Usiishi bila ratiba. Kila siku hakikisha una ratiba ya vitu vya msingi vya kufanya ndani ya siku hiyo. Hii itakusaidia kufika maeneo unapopaswa kuwa kwa wakati.
7. Kama unatakiwa kusafiri kutoka eneo moja kwenda jingine, basi ni bora huo muda ukauhusisha kwenye ratiba yako.
Rafiki, yangu. Muda ni mali. Muda ni rasilimali muhimu ambayo unaweza kuitumia kujijenga na kujenga maisha yako. Usipoutumia vizuri muda wako leo. Basi ipo siku utalia kwa sababu hukutumia muda wako vizuri.
Kumbuka TATIZO SI RASILIMALI ZILIZOPOTEA.
Mimi nakutakia pasaka njema sana
Umekukwa nami anayejali mafanikio yako,
GODIUS RWEYONGEZA
www.songambeleblog.blogspot.com
0755848391
MOROGORO
Kwenye kitabu changu cha KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI kuna kipengele nimezungumzia kuhusu muda. Pata nakala yako leo kwa kuwasiliana nami ili uweze kujifunza zaidi.
Unaruhusiwa kuwashirikisha wengine bila kubadili chochote
KUPATA MAKALA KAMA HIZI kwenye barua pepe yako, jaza taarifa zako
[mailerlite_form form_id=1]