Hizi hapa ni kazi nne za fedha


Moja ya kitu ambacho watu wengi wamekuwa hawajui ni  kazi za fedha. Wengi wamekuwa wanafikiri kwamba fedha ina kazi mbili. huku wachache wakifikiri kwamba fedha ina kazi tatu na ni wachache zaidi ambao wanafikiri kwamba fedha ina kazi nne.  Hivyo leo nimeona nikuweke kwenye kundi la wachache zaidi ambao wanafahamu wazi kwamba fedha ina kazi kuu nne

 

Kazi ya kwanza ni kutumia.

Asilimia kubwa ya watu wanajua kazi hii peke yake tu. wanajua kwamba ukipokea fedha inakuwau ni ya kwako na hivyo unakuwa na mamlaka ya kuitumia jinsi utakavyo. Ila ni wazi kwamba unapoapokea fedha inakuwa sio ya kwako. maana pale unakuwa umeshikilia fedha ya muuza nguo, muda tu unapoenda kununua nguo unachukua fedha yake unamkabidhi. Unakuwa una fedha ya muuza chakula, una fedha ya mtu wa daladala, una fedha ya matibabu, mawasiliano . Na matumizii mengine, ukifanya matumizi yote haya mwisho wa siku hautabaki na kiasi chochote mfukoni na ile fedha ambayo ulikuwa unasema kwamba ni ya kwako itakuwa sio ya kwako tena. Utakuwa umewakabidhi wenye fedha na wewe kubaki bila kitu.

 

KUMBUKA: matumizi yako hayapaswi kuwa makubwa zaidi kuliko kiasi unachoingiza.

Hapo ndipo inakuja kazi ya pili ya fedha.

 

KAZI YA PILI NI KUWEKA AKIBA

Hii ndiyo kazi ya pili ya fedha. Kwamba uweke akiba ya fedha ambayo ni kwako. fedha ambayo hakuna mtu mwingine mwenye mamlaka juu yake. Fedha ambayo unaweza kusema ni ya kwangu na ikawa ni ya kwako kwelikweli. Kwenye kitabu cha TAJIRI MKUBWA WA BABILONI mwandishi anakiita kitendo hiki hapa kujjlipa mwenyewe. Hii ndio kusema kwamba utapaswa kuwa unajilipa kwa kila kiwango ambacho unapokea. Na kujilipa kunapaswa kuwa ni kuanzia asilimia kumi ya kile ambacho unapokea ila sio chini ya hapo. Ukipokea elfu kumi asilimia kumi yake ni elfu moja. hiki ni kiwango cha fedha ambacho unapaswa kuweka pembeni kama akiba. Ukifanya hivyo utakuwa  umejilipa mwenyewe.

KWA MAELEZO ZAIDI SOMA MAKALA HII:

 

Ebu fikiria tangu umeanza kuwa na akili ya kuifahamu fedha mpaka leo hii. Kama kweli ungekuwa unafuata utaratibu huu, unadhani leo hii ungekuwa na fedha kiasi gani mpaka sasa hivi? Bila shaka ungekuwa umefika mbali sana. pengine ungekuwa tayari milionea. Sasa umeujua ukweli huu leo hii, ebu hakikisha kwamba unautumia. Usisahau kuwafundisha watoto wako  elimu hii. Hizo fedha wanazopewa kwa ajili ya kununua pipi, biskuti, mandazi na BIG G, hakikisha kwamba wanaweka akiba kwanza kabla hawajanunua wanachotaka.  

 

KAZI YA TATU YA FEDHA NI KUWEKEZA

Ndio mpaka sasa hivi umeweza kuweka akiba. Sasa hivyo akiba unaitumia kufanya nini? je, akiba ni ya kula chakula? Je, akiba ni kwenda kujirusha na kula starehe? Hapana. Hii akiba tunaweza kuiita mtoto. Sasa huyu mtoto anapaswa kukuzalia watoto wengine zaidi, na watoto hao watapaswa kukuzalia watoto wengine zaidi. Akiba hii unapaswa kuiwekeza sehemu ambapo itakufanyia kazi ili kukuingizia fedha zaidi. Unaweza kuiwekeza kwenye kuanzisha biashara, au unaweza kuiwekeza kwenye hisa au hatifungani. Kwa kufanya hivi unaipa fedha nafasi ya kukufanyia kazi na kuja na fedha zaidi. Hivyo wewe mwenyewe unakuwa unazidi kujenga utajiri wako.

 

KAZI YA NNE YA FEDHA NI KUTOA

Hapa sasa ndipo linakuja suala zima la kuwasaidia wasiojeiweza na wenye uhitaji. Hii ndio kazi ya nne ya fedha.

 

Rafiki yangu, asilimia kubwa ya watu huwa hawajui kazi hizi nne za fedha, hivyo ambacho huwa wanafanya ni kupokea fedha, na kutumia tu. wengine wanajua kwamba kazi ya fedha ni kutumia na akiba, hata hivyo akiba yao hiyo huwa wanakuja kuitumia baada ya muda badala ya kuiwekeza sehemu ili iwazalishie fedha zaidi.

 

 

 


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X