Jinsi Ya Kuutumia Muda Ulioupata Ndani Ya Kipindi Hiki Cha Korona Kwa Manufaa. Mambo Sita (06) Ya Kufanya Katika Kipindi Hiki Ambayo Hujaambiwa Na Mtu Yeyote


Habari ya siku hii ya kipekee sana rafiki yangu. Hongera sana kwa kupata siku hii nyingine, kiukweli hakikisha kuwa siku hii unaitumia vizuri kwa ajili kufanya vitu vya toafuti.

 

Dunia nzima sasa hivi inapitia katika kipindi ambacho shughuli nyingi za kiuchumi zimefungwa. Hivyo kitu hiki kufanya watu wengi kuwa majumbani kwao bila majukumu ya kikazi ya kila siku. Kuna sekta chache tu ambazo kazi zake zinaendeelea ila sekta nyingine kama sekta ya elimu, michezo na burudani, usafiri zimefungwa au kazi zinaendelea ila sio kama ilivyozoeleka.

 

sasa kama kazi nyiingi zimefungwa ndio kusema kwamba kuna watu wengi ambao wapo nyumbani kwa ajili ya mapumziko ila hawajui ni kitu gani cha kufanya. Hivyo leo hii nimeona nikuletee mambo sita ambayo unaweza kufanya ndani ya kipindi hiki hapa, yakawa yenye manufaa makubwa sana kwako, leo hii na siku nyingine zijazo.

1. JIFUNGIE KUSOMA

Hiki sio kipinidi cha kuangalia na kufuatilia kila aina ya tamthiliya. Bali ni kipindi ambacho unapaswa kujinoa na kuongeza maarifa yako mara mbili mpaka mara tatu zaidi ya hapo awali. Katika kipindi hapa chagua vitabu ambavyo utasoma na kujifunza kwa kina. Soma vitabu kuhusu biashara, fedha na uchumi maendelea binafsi au vitabu vinavyohusiana na kazi yako.

Yaani, ukiutumia  muda huu vizuri, ni wazi kuwa baada ya kipindi hiki kuisha basi utakuwa umeongeza maarifa yako mara dufu. Na kanuni ya malipo iko wazi, inasema kuwa ukitaka kulipwa mara mbili zaidi basi ongeza maarifa yako mara tatu zaidi. Hivyo kaa ukifahamu kuwa maarifa haya yatakusaidia hata kama sio kwa haraka, ila ni ukweli kuwa maarifa haya utakayopata ndani ya kipindi hiki hayapotea hata kidogo.

 

2. FANYA KITU AMBACHO KWA SIKU SASA UMEKUWA UNAHAIRISHA

Je, ni kitu gani ambacho ulikuwa ukipanga kukifanyia kazi kwa siku nyingi ila ukawa unahairisha kwa sababu ya kukosa muda? Sasa zamu hii ndio unapaswa kukifanyia kazi bila kukosa. Kitumie kipindi hiki hapa kufanya kitu cha aina hii.

Je, ulikuwa unapanga kuandika kitabu ila hukuwahi kufanya hivyo? Je, ulikuwa unapanga kufanya mazoezi huku ukihairisha? Sasa utumie muda huu kufanya kitu cha aina hiyo

 

3. JIFUNZE UJUZI AMBAO  HAUKUWA NAO

Kitumie kipindi hiki kuwekeza kwenye ujuzi mmoja tu ambao utakusaidia kwa siku nyingi huko mbeleni. Jifunze ujuzi ambao  hakuna mtu ambaye anaweza kukuibia ujuzi huo.

Hiki ni kipindi ambacho kifurushi chako cha intanenti unapaswa kukitumia vizuri. Sio kwa kufuatilia watu wangapi wanapatwa na korona,bali kwa kufuatilia  na kujifunza ujuzi mmoja tu muhimu kwako. kama hujui ni ujuzi gani unaweza kujifunza, basi hapa ninakuwekea sehemu ya kuanzia. Kwanza ni kuandika, unenaji (public speaking) na masoko na mauzo ( sales and marketing). Chagua ujuzi mmoja hapo, kisha anza kuufanyia kazi mara moja

 

4. FUNGUA BLOGU

Hik ni kipindi ambacho unapaswa kufungua blogu yako na kuanza kurindima mtandaoni. Labda unaweza kuwa unajiuliza, kwa nini kufungua blogu? Iko hivi. Tunaishi kwenye zama ambazo zimebaadilika sana. Yaani, kwenye zama za sasa hivi, mtu akitaka kitu hata haanzi kujiuliza maswali mawili au matatu. Anachofanya ni moja kwa moja kuingia mtandaoni na kutafuta hiccho kitu. Na huku ndipo anategemea kukutana na majibu ya swali lake.  Sasa ni mtu gani ana majibu yake, NI WEWE HAPO?

Sasa kama wewe hujaweka kazi yako mtandaoni, ni wazi kwamba hata iweje, mtu huyu hataweza kukufahamu. Ila kama upo mtandoni basi ni rahisi kukupata. Na ninaposema uwe mtandoni simaanishi kwamba uwe kwenye  whatsapp au facebook. namaanisha uwe na blogu yako.

 

Blogu ni sehemu pekee ambayo unaweza kuimiliki mtandaoni. Hii mitandao mingine ya kijamii ni vijiwe, ila ni vijiwe vya kisasa (kidigitali). Ni kawaida kuwa tukienda kwenye vijiwe vya mtaani huwa mwisho wa siku tunarudi nyumbani. Kitu kama hiki pia, kinatokea mtandaoni. Unapoenda kwenye mitandao ya kijamii (vijiwe), mwisho wa siku utapaswa kurudia nyumbani. Na utapaswa kuwakaribisha watu wengine kuja nyumbani kwako.

 

Sasa swali nyumbani kwako mtandaoni ni sehemu gani? Hapa sasa ndio ninakwambia kuwa BLOGU NDIO NYUMBANI KWAKO. Wala sio kwenye kikasha cha kupokea jumbe (INBOX).

Je, umeshafungua blogu yako?

Chukua hatua leo. Kama unahitaji msaada wa haraka wa kufungua blogu nitumie ujumbe kwenda 0755848391. Nitakutengenezea blogu ya kitaalamu kwa elfu 30 na kukushika mkono kwa wiki mbili za mwazo ambazo utaanza kuitumia.

 

4.  ANDIKA KITABU/ IMBA WIMBO WAKO/ TOA IGIZO LAKO

Hiki ni kipindi ambapo unapata utulivu mkubwa sana. kama umewahi kuwa na mpango wa kuandika kitabu, basi huu ndio muda wa wewe kuhakikisha kwamba kitabu chako sasa unakileta kwenye uhalisia.

 

Kama umewahi kuwa na mpango wakuimba wimbo, basi kitumie kipindi hiki hapa kutoa tungo yako hiyo.

 

Kama umewahi kufikiri juu ya kuandaa igizo, basi kipindi hiki hapa ni kipindi ambapo igizo lako unapaswa kuliandaa vizuri sana. yaani kwa vyovyote vile, hakikisha kile kitu ambacho kwa siku nyingi sasa umekuwa na mpango wa kufanya unakifanyia kazi kweli kweli.

 

5.  HAKIKISHA UNAPATA VITU VITATU AMBAVYO UTAVIFANYIA KAZI MARA TU BAADA YA UGONJWA KUISHA

Ugonjwa huu ukiisha maisha yataendelea kama kawaida. Lakini hatutarudi nyuma. Mambo yatabadilika kidogo. sasa baada ya ugonjwa kuisha wewe utafanya nini ili kuweza kuwasaidia watu wengine. Utafanyaje ili kutatua matatizo mengine ya kijamii ambayo yatajiotkeza. Utafanyaje ili kuongeza kipato chako?

 

Haya ni maswali ambayo unapawa kuyapatia majibu yako sasa hivi na kuweka mpango ambao utaufanyia kazi mara moja.

 

Bila shaka umeona ni wapi ambapo unaweza kutumia muda wako vizuri ndani ya kipindi hiki hapa. nikusihi sana uutumie muda huu kwa manufaa sana. itakuwa ajabu kubwa sana baada ya kipindi hiki kuisha, wewe pia ukawa hauna kitu cha maana ambacho unaweza kuonesha kwa watu kuwa umeweza kufanya ndani ya kipindi hiki hapa. kiukweli, kiukweli utakuwa umeutumia muda wako vibaya.

kila la kheri

makala nyingine zinazoendana na hii:

Vikwazo Kama Hiki Hapa Huwa Vinatokea Kukuimarisha Sio Kukuangusha


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X