NINAONA KITU NDANI YAKO


 

KUNA BAADHI YA WATU WALIKUWA HAWAJIELEWI KWENYE  HATUA FULANI KWENYE MAISHA. Ninaposema kwamba walikuwa wahajielewi ninamaanisha kwamba hawakuwa na kitu kikubwa cha kufanya na maisha yao. Yaani, wao walikuw wanaishi tu ilimradi wamekula, wamekunywa na kufanya kazi. maisha yao yalikuwa yakiendelea hivyo hivyo mpaka pale ambapo alitokea mtu ambaye aliona kitu kikubwa ndani yao. Mtu huyu akawa kama taa, au mwanga au akawa mtu aliyewanyanyua usingizini. Na huo ukawa ndio mwanzo wa maisha yao. Huo ukawa ndio wito mpya wa watu hawa kuanza maisha yao ya kufanya mambo ya tofauti.

 

Siandiki haya ili wewe uanze kutafuta mtu ambaye utaona kitu ndani yake na kumwambia au kumtaka aanze kuishi maisha fulani ambayo unaona yanamfaa.   

Njia nzuri ya wewe kuweza kuwabadili watu ambao ungependa wabadilike ni wewe kuanza kuishi maisha ya ndoto yako. Anza kuishi jinsi ambavyo unataka.  Ukianza kuishi maisha mbayo unataka, kuna watu ambao wataona utofauti kwenye maisha yako na wao watataka kuwa kama wewe. Na hapo ndipo utatumia  nafasi hiyo kuwaonesha njia ili na wao waweze kufanya kitu cha tofauti.

 

Binafsi ninaona kitu ndani yako. Na kitu hiki kitaanza kuonekana kwa wewe kuishi maisha ambayo siku zote umekuwa ukitaka kuishi.

 

umekuwa nami rafiki yako,

Godius Rweyongeza

PATA KITABU CHA BURE KWA KUBONYEZA HAPA


One response to “NINAONA KITU NDANI YAKO”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X