Ushauri Kwa Kijana Ambaye Anaanza Maisha Na Angependa Kufanya Kitu Anachopenda Ila Hajui Pa Kuanzia


 

Mara nyingi huwa unakuta kwamba, kijana anapoenda kusoma chuo,  anasoma kitu ambacho wazazi wake au walezi wake wameona kwamba kinafaa kwake. Hivyo, hata anapoenda kufanya kazi, anaenda kufanya kazi ambayo haitaki.

 

Lakini kwenye zama hizi hapa, ni rahisi sana kwa kijana kufanya kazi ambayo anataka hata kama chuo kasomea kitu ambacho walikuwa hataki. Unaweza kuwa unajiuliza hii inawezekanaje? Hii inawezekana kutokana na ukweli kwamba, unaweza kujifunza vitu vingi sana kwa njia ya mtandao ambavyo unaweza kufanyia kazi.

 ANGALIA VIDEO HII: Maeneo Mawili Ya Kupata Shahada Mtandaoni Bure Kabisa

Na njia mojawapo ya kufanya kazi ambayo unaipenda ni kujiajiri kwa kuanzisha biashara hata kama biashara hiyo itaonekana ni ya kijinga. Hii itakupa nafasi ya kujifunza mambo mengi sana ambayo utaweza kuyafanyia kazi kwenye maisha yako ya kila siku na hata kwenye biashara yako ijayo.

 

Ukiona kwamba biashara hiyo ya kijinga uliyoanzisha haikufai, bado unakuwa una uhuru wa kuiacha na kuanzisha biashara nyingine. Kitu kikubwa ni kwamba utajifunza kitu kutoka kwenye biashara hiyo ambacho utakifanyia kazi kwenye biashara nyingine au kwenye kazi nyingine ambayo utakuwa unafanya. Na kitu kikukbwa zaidi ni kwamba unaweza kuanza na biashara ya kijinga mwanzoni ila baadae ukahamia kwenye biashara kubwa na nzuri baada ya kupata mtaji na pengine hii ikawa ile ambayo unaipenda.

 SOMA ZAIDI: Makosa Matano Ya Kuepuka Wakati Unaanzisha Biashara

Unaweza ukawa unajiuliza, hivi kweli kuanzisha biashara inaweza kuwa ni njia bora ya mimi kufanya kitu ambacho ninakipenda? Jibu linaweza kuwa ni ndio na hapana. Kuanzisha biashara inaweza kuwa sio njia bora zaidi ila kulinganisha na njia nyingine ambazo zipo basi yenyewe ni bora zaidi. hakuna sehemu nyingine ambapo unaweza kupata nafasi ya kufanya kitu unachopenda kama kwenye biashara. kwenye ajira utapaswa kufanya kazi ambayo umeamuriwa kufanya, haijalishi unaipenda au huipendi.

 

Unaweza ukawa unajiuliza, sasa itakuwaje maana mimi nimehitimu chuo na nina shahada, astashahada n.k? Watu watanionaje endapo nitaenda kufanya kuanzisha ya mtaji mdogo?

Vizuri na hongera kwa kisomo chako. Kumbuka kwamba mwanzoni anza na biashara ambayo inaweza kuonekana ya kijinga. Lengo la biashara hii ni kwamba ikuingizie kipato, lakini pia upate kujifunza kitu kikukbwa kutoka kwenye hii biashara.

Kitu kimoja ambacho ninaweza kukwambia ni kwamba kama mpaka sasa hivi hauna fedha, basi wewe hapo hauna kitu cha kuogopa kufanya hata kama umehitimu chuo. Huwezi kuingia hotelini na kulipa chakula kwa shahada, huwezi kuingia kwenye daladala na kulipa nauli kwa shahada, huwezi kulipa kodi ya nyumba kwa shahada. Fedha ndio inalipa vitu hivi, amua kufanya biashara ya kijinga na ukue kisha kusongambele au acha.

Ningependa kumalizia makala ya leo kwa mfano wa kijana mmoja aliyekuwa amehitimu chuo kikuu cha HAVARD. Kijana huyu alikuwa anapenda sana magari kiasi kwamba alikuwa anayachora kila siku kwenye notebook yake. Hata hivyo,  aliendelea kufanya kazi ambayo alikuwa haipendi. Kazi ya benki kwa sababu tu baba yake alimwambia afanye hiyo kazi.

 

Kwa maneno hayo basi, nakuachia uwanja ili uweze kufanya maamuzi sahihi wewe mwenyewe.  Kila la kheri

 

Kwa ushauri, tutumie ujumbe kwenda songambele.smb@gmail.com nasi tutakujibu

hakikisha umejiunga na mfumo wetu rasmi wa kupokea makala maalumu kwa watu maalumu kwa kufuata maelekezo ya chini hapa

MAKALA ZINAZOENDANA NA HII: WANAOSHEREHEKEA KUHITIMU CHUO, TUWAAMBIE UKWELI AU TUWAACHE MPAKA WAFUMUE NYWELE ZAO ZA GRADUATION?

Vitabu Vitano Ambavyo Kila Muhitimu Wa Chuo Kikuu Anapaswa Kuanza Kusoma Mara Moja

Kama Ningekuwa Wewe Ningefanya Hivi

Ni mimi anayejali mafanikio yako,
GODIUS RWEYONGEZA

KUWA MIONGONI MWA WATU AMBAO WANAPOKEA MAKALA MAALUMU KWA WATU MAALUMU KWA KUBONYEZA HAPA

SUBSCRIBE KWENYE CHANNEL YANGU YA YOUTUBE HAPA


JIUNGE NAMI KWENYE NURU ANGAZA


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X