Hiki Ni Kitu Kimoja Ambacho Ninakijua Kuhusu Wewe


Rafiki kuna kitu kimoja nakijua kuhusu wewe hapo. unaweza kujiuiliza kuwa ni mtu gani huyu alikwambia siri zangu. naomba tu, utulie kwanza nikwambie kitu hiki.

 

Kitu hiki ni kuwa wewe walau una kitu ambacho unaweza kutoa kwa watu ili kuwafanya watu wengine wawe na maisha bora zaidi. Inawezekana kitu hiki sio kikubwa lakini unacho.

Kitu hiki kinaweza kuwa ni kipaji chako

Unaweza kuwa ni ujuzi wako

Kinawezakuwa ni kitu ambacho ambacho umekuwa ukikifuatilia kwa muda mrefu na sasa umekijua kiundani ila kuna watu ambao wangependa kujifunza pia kutoka kwako.

 

Hivyo nikusihi kuanzia leo, uanzishe utaratibu wa kuangalia namna ambavyo unaweza kufanya maisha ya watu kuwa bora zaidi kupitia kitu hicho ambacho unajua. Kupitia kitu hicho ambacho unaweza kukitumia kufanya maisha ya watu wengine kuwa bora zaidi.

Kama una kipaji cha kuimba basi maana yake unapaswa kuanza kuimba ili watu wengine waburudike kwa sababu umetumia vyema kipaji chako

Kama  una kipaji cha kutangaza, maana yake unapaswa kukitumia vyema kutangaza mambo ya msingi ili watu waweze kunufaika na hicho kipaji chako.

Kama una kipaji cha kushauri, kitumie vyema kwa manufaa ya watu wengine.

Kama una kipaji cha kushawishi basi kitumie pia kwa manufaa.

Ni wazi kuwa kila mtu walau ana kitu. Hata kama sio kikubwa. Lakini hiki kitu kikitumika kwa manufaa, basi ni wazi kuwa kitawanufaisha walio wengi.

 


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X