Kitu Hiki Hapa Ndicho Watu Wamekuwa Hawajui Kuhusu Fedha


 

Hongera sana kwa siku hii ya leo rafiki yangu. Leo ningependa kuongelea kuhusu fedha. Maana, ni kitu ambacho watu wengi wanaogopa kukiongelea. Mtu akionekana anaongelea sana kuhusu fedha jamii inamchukulia kuwa ni mnafiki, na mtu ambaye haweki maslahi ya watu wengine mbele. Hata hivyo ni wazi kuwa mtu ambaye anaongelea fedha LAZIMA tu atakuwa mtu anayewajali watu. kwa sababu fedha huwa haiji tu, bali ni matokeo ya THAMANI au HUDUMA ambayo mtu anatoa kwenye jamii yake. Kwa hiyo mtu anayeongelea fedha lazima atatafuta njia zaidi za kuongeza thamani kwenye jamii yake ili aweze kupata fedha zaidi. Na kadiri huduma yake inavyokuwa bora ndivyo mtu huyo anazidi kupata watu wengi zaidi ambao wanakuwa tayari kulipia na yeye anazidi kupata fedha.

Pia kadri huduma inavyowafikia wengi zaidi ndivyo mtu huyo anazidi kupata fedha.

 

Siku ya leo. Kwenye upande wa fedha ningependa ufahamu kuwa kiwango cha utajiri ambacho unapaswa kufikia ni kile ambacho wewe mwenyewe hutakuwa na uwezo wa kuhesabu fedha zako. Yaani, kama unaweza kukaa chini na kuhesabu fedha zako, basi ujue kwamba bado hujaweza kuwa tajiri hivyo endelea kuweka juhudi zaidi ili uweze kufikia hivyo viwango ambavyo fedha zako huwezi kuzihesabu.

 

Unaweza kujiuliza kuwa kama matajiri wana fedha ambazo hawawezi kuzihesabu inakuwaje sasa tunakuwa na orodha ya matajiri ambayo huwa inatolewa na majarida maarufu kama jarida la FORBES? Jibu ni kuwa hayo majarida huwa yanakadiria kiwango cha fedha cha mtu, ila huwa sio kiwango halisi. Kwa sababu ukitaka kujua kiwango halisi cha mtu. Ni lazima uuze mali zake zote kwa kupata fedha mkononi. Ambayo inakupa kiwango hicho. hata hivyo, kitu kama hicho hapo huwa hakifanyiki. Badala yake majarida haya huwa yanakadiria thamani ya mali za mtu na kuziweka katika fedha. thamani ambayo inaweza kuwa ni tofauti pale ambapo zile mali zikiuzwa.

 

Kwa hiyo rafiki yangu, leo ningependa uendelee kuweka juhudi ili kuweza kufikia kiwango cha fedha ambacho wewe mwenyewe hutakuwa na uwezo wa kukihesabu. Hapo utakuwa umeufikia utajiri.

Nakutakia siku njema.

SOMA ZAIDI; fedha inaondoa matatizo au matatizo yanaondoa fedha?

jiunge na jumuiya ya wanasongembele kwenye channel yetu ya YOUTUBE kwa  KUBONYEZA HAPA


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X