Fursa Ya Wazi Ambayo Unaichezea


Kuna fursa ambazo naona wazi vijana hawazitendei haki. Na pengine wanachukulia poa hii fursa. 
Lakini pengine fursa hii wangeipata mababu wetu, basi wangefurahi sana. Au kama hao mababu wetu wangekuwa leo hii wanakuja na kuona jinsi wewe  unavyoamua kuchezea fursa hii wangekupiga Kofi. 
Fursa hii sio nyingine, Bali fursa ya mtandao wa intaneti. Mtandao umekuja na mambo mengi mazuri. Mpaka sasa hivi unakuwezesha wewe kupata elimu na kujifunza chochote kile ambacho utapenda. 
Ebu fikiria leo hii ukiamua kujifunza Kuhusu uandishi, unaweza kwa kutumia intaneti.
Leo hii ukiamua kujifunza lugha mpya. Kwa kutumia bando la bure la SUPA LA VODACOM (Zile Mb 50 za bure za asubuhi) unaweza kujifunza lugha mpya na ukaielewa kiundani.
Ukiamua kujifunza chochote kile, leo hii unaweza. 
Pengine dhambi ambayo utakuwa unafanya sasa hivi ni kutotumia mtandao huu kwa manufaa.
Kwa leo, napenda
1. Uchague Kitu kimoja ambacho utaanza kujifunza kwa kina kwa siku 66 zijazo. Maeneo ya wewe kujifunzia yapo mengi. ANZIA YOUTUBE.
Huko kuna walimu wengi, kiasi kwamba huwezi kukosa mmoja tu ambaye anakufaa wewe.
2. Jifunze hicho Kitu bila kuchoka, kwa siku 66 zijazo. Kuna baadhi ya vitu vitahitaji muda zaidi ya huo. Mfano kujifunza lugha mpya.
3. Fanyia kazi ulichojifunza. Ukijifunza Kuhusu mapishi, nenda kafanyie kazi ulichojifunza. Haitoshi tu kukusanya maarifa mengi bila kuyaweka kwenye matendo.
Godius Rweyongeza


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X