HAKIKISHA UNAZIMA KIFAA CHAKO CHA KIELETRONIKI UNAPOENDA KULALA


 

 Rafiki yangu hongera sana kwa siku hii nyingine ya leo. Siku ya leo nina ujumbe mfupi tu kwako ambao ningependa uufahamu. Na ujumbe huu ni kuwa hakikisha unazima kifaa chako cha kieletroniki kila unapoenda kulala.

Kwenye zama hizi imekuwa ni tabia ya watu kuwa mtu anapoamka asubuhi, mpaka usiku anapoenda kulala, anakuwa amefungulia vifaa hivi vya kieletroniki. Vifaa hivi ni vizuri na tunavihitaji kwa maumizi ya yetu, ila kuna wakati wewe mwenyewe unapaswa kukizima na HASA UNAPOENDA KULALA.

Unaweza kushangaa kuwa hiki kitu kina manufaa gani kwenye mafanikio yangu. Ila  HAPA  kuna sababu kuu mbli ambazo zinapaswa kukusukuma wewe kuzima kifaa hiki

 

KWANZA ILI KUONDOA USUMBUFU pale unapokuwa umelala. Ukiwa usingizini, haupaswi kuwa unasumbuliwa na kitu chochote. Maana, muda huu ni muda wako wa kipeke ambapo mwili unakuwa unajijenga na kurudia kwenye hali nzuri. Yaani,wewe mwenyewe ni kama unakuwa unachaji mwili wako. Baada ya mizunguko na kazi za siku nzima. Haipendezi, wakati mwili unaongeza chaji wewe uwe unausumbua kwa kelele za hapa na pale au kwa kuendelea kufuataili kinachoendelea kwenye mitandao kwa kutumia hivi vifaa vya kiektroniki.

Na ni kweli unapopata usingizi mzuri, asubuhi unaamka ukiwa na nguvu na aunakuwa imara.

 

Sasa ukienda kulala na kifaa cha kieletroniki kikiwa kimewaka kuna hatari mbili, hatari ya kwanza ni wewe kushawishika kukiangalia na hasa pale kinapokuw karibu yako. Hii ni mbaya maana ule mwanga wa vifaa hivi vya kieletroniki una madhara kwenye usingizi wako

Pia, unaweza kupigiwa au kifaa hiki kinaweza kusababisha kelele, kitu ambacho bado kitaharibu mfumo wako wa usingizi.

Unaweza kujiuliza, kwa ni kuna shida gani endapo mimi nitapigiwa simu usiku. Je, kama ni dhrula na inanihitaji mimi. Ukweli ni kuwa hakuna dharula ambayo haiweze kukusubiri wewe hapo. yaani, kama kitu hakiwezi tu kukusubiri kwa huo muda mchache uliokuwa umelala, basi ni wazi pia pengine ungeweza kukikosa wakati upo macho pia.

 

Hivyo basi rafiki yangu, jizoeze kuzma vifaa hivi vya kieletronini kila unapoamka asubhi. Nikutakie siku njeam.

 

 

 

 

 


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X