Huu Ndio Muda Ambao Unapaswa Kufanikiwa Kwa Viwango Vikubwa Sana


 

Rafiki yangu hongera sana kwa siku hii ya kipekee sana.  Sku ya leo nilipenda tu nikueleze kuwa kuna muda ambao wewe hapo unapaswaa kufanikiwa kwa viwango vikubwa. Na muda huu ni pale ambapo unkuwa hauna kitu chochote kile cha kupoteza.

Kama ndio kwanza unaanza na hauna vitu vingi ambavyo unaweza kusema kwamba utapoteza basi usiogope kitu chochote. Weka kazi, fanya kila unachoweza kwa bidii na jitume ili kupata matokeo makubwa.

Hata hivyo, si hauna kitu cha kupoteza. Sasa unaogopa nini? haupaswi kuogopa kumpigia simu mtu na kumwambia mtu anunue bidhaa yako, kwa sababu hauna kitu cha kupoteza. haupaswi kuogopa kuanzisha biashara mpya au kuwekeza maana hauna kitu cha kupoteza.

Kwa chochote kile, usiogope, maana hauna kitu chochote kile cha kupoteza.

Umekuwa nami,

Godius Rweyongeza

Jiunge nami youtube kwa KUBONYEZA HAPA

Pata vitabu vyangu kwa KUBONYEZA HAPA

Kupata makala maalumu kwa watu maalumu basi BONYEZA HAPA

 


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X