Kutana Na Watu Watano Walioshindwa Karibia Kwenye Kila Kitu Na Bado Wakashinda Kwa Kishindo


 

 

Matatizo, vikwazo na changamoto humtokea karibia kila mtu kwenye maisha. Watu pekee ambao matatizo na vikwazo haviwezi kuwatokea ni wale waliolala kwenye makaburi. Ila kwa yeyote yule ambaye bado anapumua, basi matatizo na vikwazo ni kama sehemu ya maisha. Kitu kimoja cha kushangaza kuhusu matatizo, vikwazo na changamoto ni kwamba huwa vinawaimarisha baadhi ya watu na wakati huohuo huwa vinawatoa baadhi ya watu kwenye ramani. Yaani, kiufupi ni kuwa kuna baadhi ya watu huwa wanavunja rekodi baada ya kupitia matatizo, changamoto na vikwazo na kuna watu huwa wanavunjika baada ya kupitia kwenye matatizo, changamoto na vikwazo.

 

Wale ambao huwa wanvunjika basi huishia kulalamika na kusema kwamba maisha ni magumu. Ila wale ambao huwa wanavunja rekodi huwa wanajifunza kutokana na matatizo na changamoto ambazo huwa wanakutana nazo na hivyo kuzidi kuinuka na kuzidi kusonga mbele zaidi. Sasa siku ya leo nimeona nikuletee watu watano ambao walianguka na kushindwa karibia kwenye kila kitu na bado wakainuka kwa kishindo na kushinda haswa. Mtu wa tano ni muhimu sana kwako kuhakikisha unamsoma

 

 

1. STEVE JOBS

 

Huyu ni mwanzilishi mwenza wa kampuni ya Apple, kampuni ambayo inatengeneza simu za Iphone. Mwaka 1985 kwenye kampuni ya apple ulitokea mgogoro mkubwa sana kati yake na aliyekuwa mkurugenzi wa kampuni kwa wakati huo Robert Schuller. Mgogoro huo ulipelekea Steve Jobs kufukuzwa kwenye kampuni aliyoainzisha ya Apple. Hili lilikuwa ni anguko kubwa sana Kwa Steve Jobs. Yaani, kipindi hicho ni kama Steve Jobs alikuwa aemejenga nyumba, sasa baada ya nyumba kukamilika ndio akafukuzwa kwenye nyumba yake. Jobs alianza kufikiria kuhamia Ufaransa, ila baadaye aliamua kuanzisha kampuni ya NeXT. Kampuni ambayo na yenyewe miaka mitano baadaye ilikuwa bado haina mwelekeo kiasi wafanyakazi na waanzislishi wenza wakawa wanamkimbia. Lakini hayo mapigo hayakumkwamisha wala kumsimamisha Steve Jobs. Bado alisimama wima na kuendelea na safari na hapo ndipo aliamua kuuza kampuni yake ya NeXT na kurudi kwenye kampuni yake ya awali APPLE. Kilichotokea ni kwamba alianza kufanya kufanya ubunifu kwenye hiyo kampuni huku akisimamia kazi kwa ubunifu wa hali ya juu sana. Alipunguza bidhaa zilizokuwa zinauzwa kwenye hiyo kampuni kutoka arobaina na kuamuru kampuni ijikite kwenye bidhaa tano tu. Alianzisha kampeni ya Fikiri Tofauti (Think Different) ambayo ilikuwa ni kampeni muhimu sana kwenye historia ya kampuni ya APPLE.

 Baadaye akaja na ubunifu wa kifaa kidogo cha kusikiliza muziki (ipod) na baadaye Iphone. Kiufupi mtu ambaye mwaka 1985 alianguka anguko kuu, sasa alikuwa amesimama tena kwa kishindo kikubwa. mpaka kifo chake mwaka 2010 Steve Jobs alikuwa amejenga hisotoria ya kipekee sana kwenye tasnia ya mawasiliano, muziki, uuzaji wa bidhaa kupitia mtandao na mengine mengi. Mtu aliyekuwa ameanguka aliinuka tena kwa kishindo kikubwa.

 

 

2. ELON MUSK

Elon Musk ni mwanzilishi wa kampuni ya Tesla, Spacex na kampuni nyinginezo sita.kilichomtokea mtu huyu ni kwamba mwanzoni mwa mwaka 2000 alikuta watu wametengenza njama za kumwondoa kwenye cheo cha ukurugenzo mkuu wa kampuni yake. Mipango ilikuwa tayari imesukwa vizuri kiasi kwamba ilikuwa tena haiwezekani kwake kuweza kuendelea na ukurugenzi wa kampuni hiyo.

 

Kitu kama hiki kingetoke kwa watu wngine kingekuwa ni kikwazo kikubwa cha kuwasimamisha na kuwazuia kuendelea mbele. Hata hivyo, hali haikuwa hivyo kwa Elon Musk

 

Baadaye, aliweza kusimama na kuanzisha kampuni za Tesla na SpaceX. Na leo hii bado anaendelea kupambana, huku akiwa na lengo kuu moja. kuhakikisha kwamba binadamu wanakuwa na makazi kwenye sayari tofautitoafuti.

 

 

3. JACK MA

 

Mwishoni mwa miaka ya tisini kampuni za kiteknolojia zilikuwa zinapata fedha sana hasa pale zilipokuwa zinauza hisa zake kwenye soko la awali. Hata hivyo, hali hiyo iltoweka mwanzoni mwa miaka ya 2000 ambapo makampuni mengi ya kiteknolojia na mawasiliano yaliyumba. Hali kama hiyo pia ilikumta Jack Ma na kampuni yake ya Alibaba. Jack Ma alikuwa anahangaika na fedha za kuiendesha kampuni kwa kipindi kirefu. Katika kipindi hicho kuna wafanyakazi pia walitishia kumwacha na kuondoka kwenye kampuni yake. Hata hivyo, Jack Ma aliweza kusimama kwa kishindo kikubwa na kuwaambia kwamba wale ambao walikuwa wanataka kuondoka walikuwa wanaruhusiwa kuondoka ila yeye alikuwa na imani na kampuni yake na angeendelea kuipigania mpaka mwisho. Huwezi amini, hakuna aliyeondoka na Jack Ma aliisimamia kampuni yake kwa ujasiri mkubwa mpaka leo hii, kampuni yake ni moja ya kampuni kubwa sana hapa duniani.

 

 

4. 50 CENT

 

Akiwa na miaka 9 mama mzazi wake aliaga dunia na huku akiwa hamjui baba yake. Ilibidi sasa ajitose kwenye uuzaji wa madawa ya kulevya akiwa na miaka 12. Maisha yalianza kumpiga bila huruma. Ila alichokuwa anashikiria kwa wakati huo ni kwamba alikuwa anataka kuwa mwanamziki wa hiphop. Hivyo, aliendelea kuweka akiba ya fedha ambayo ingemwezesha kuingia kwenye tasnia hii ya mziki. Baadaye aliamua kuingia kwenye tasnia hii hapa, hata hivyo kuna watu walidhani kuwa alikuwa anawachora.

 

Yaani, wauza madawa ya kulevya wenzake walijua kwamba alikuwa anataka kupenyeza siri zao ili waje wakamatwe. Hivyo, waliamua kumvamia na kumpiga risasi tisa. Kitu hiki kilimfanya 50 Cent apoteze mambo mengi. Kwanza alipoteza uwezo wake wa kuimba kutokana na risasi, pili wanamziki wenzake walimkataa kwa kusema kwamba; “sisi hatuwezi kuwa na mwanamziki mwenye  visa na watu.” Na tatu label yake iliyokuwa imemsajiri ilimkataa na kukataa kutoa tungo zake alizokuwa tayari ameimba. Hivyo, kilikuwa ni kipigo juu ya kipigo.

 

Hata hivyo, 50 Cent alisimama tena baada ya kutoka hospitali na kuanza kuimba kwa shida. Baadaye aliweza kurekodi tungo kadhaa ambazo alizigawa bure kwa watu ili wazisikilize. Watu walipokuwa wanazisikiliza wakawa wamezipenda na hivyo baadaye wakawa wanazidi kuzisambaza zaidi. kitu ambacho ndicho kilikuja kumwinua 50 Cent kutoka alipokuwa.

 

5. SIXTO RODRIGUEZ

Pengine ndio siku yako ya kwanza kabisa kwako kusikia hili jina. Huyu ni mwanamziki ambaye alivunja rekodi ya kuuza miziki mingi miaka ya themanini na tisini kuliko hata akina Bob Dylan na Cat Stevens. Lakini kabla ya mauzo hayo makubwa kilichomtokea kililkuwa cha ajabu sana. Jamaa aliimba miziki mitatu ya kwanza ambayo hata haikupata umaarufu wala hakupata fedha ya kumwezesha kuendelea kuimba. Hivyo, akawa amekata tamaa akaamua kurudia kulima kijijini.

 

Kurudi kwake kwenye tasnia ya muziki ulikuwa kama muujiza. Ilitokea kwamba binti mmoja alienda kumtembelea mpenzi wake Afrika Kusini. Alipoenda huko alienda na CD zenye miziki ya Sixto Rodriguez. Kufika Afrika Kusini yeye na mpenzi wake wakaanza kuicheza hiyo miziki. Mara ghafla marafiki wa mpenzi wa huyo binti wakawa wameipenda pia hiyo miziki. Na wao wakawa wameichukua, walipoichukua na marafiki zao pia wakawa wameipenda. Yaani, ikawa miziki hiyo inasambaa kwa kasi kila kona ya Afrika Kusini. Miziki hiyo ikaingia kwenye chati za redio mbalimbali.

 

Sasa swali kubwa lililokuwa kwenye vichwa vya watu lilikuwa je, huyu mtunzi hizi tungo nzuri yuko wapi? Watu walianza kumtafuta bila mafanikio. Kila walipouliza waliambiwa aliaga dunia. Ila mwanahabari mmoja hakutaka kulichukulia hili suala kirahisi, hivyo alianzisha tovuti ya kumtafuta Sixto Rodriguez.

 

SIKU MOJA mtoto wa Sixto Rodriguez akiwa anapita mtandaoni akaona hiyo tovuti, akaamua kuandika kwamba mimi ni binti wa Sixto Rodriguez akaweka na namba yake ya simu. Baadaye, wakawasiliana ndipo ilipofahamika kuwa Sixto Rodriguez bado anaishi. Furaha na vifijo vikatawala miongoni mwa watu waliokuwa wameshaaminishwa kuwa mwanamziki huyo ameaga dunia.

 

Sasa mipango ya kumfanya afike AFRIKA KUSINI ILIFANYIKA. Ilipotangazwa kuwa Sixto Rodriguez atakuwa anaenda Afrika Kusini, watu walinunua tiketi zote zikaisha ndani ya muda kidogo sana na bado nyingine zikawa zinahitajika.

 

Huku akiwa nyumbani pamoja na binti yake, Sixto Rodriguez alitegemea labda watu ishirini au thelathini ndio wangehudhuria kwenye hiyo show yake. Ila kufika Afrika kusini mshangao wake wa kwanza ulikuwa ni kukutana na watu elfu tano waliokuwa wamefika kwenye kiwanja cha ndege kumpokea. Na isitoshe aliposhuka kwenye ndege alipigiwa makofi na vigelele kwa dakika kumi mfululizo. Kumbe Sixto Rodriguez alikuwa maarufu nchini Afrika Kusini kulinganisha na vile alivyokuwa nyumbani kwao Marekani

 

Kutokea hapo ndio aliendelea na muziki na hatimaye kufikia hatua ya kuuza albamu zake kuliko wanamziki maarufu wa kipindi hicho, akiwemo Bob Dylan

 

 


Rafiki yangu, hao ndio watu watano ambao walishindwa karibia kwenye kila kitu na bado wakashinda kwa kishindo kikubwa sana. Kuna mengi ya kujifunza kutoka kwa watu hawa ila kikubwa ni kwamba, inapotokea kwamba kwenye maisha  umeshindwa au kuanguka, basi usiuchukulie huo kama mwisho wa safari yako. Badala yake chukua somo na kisha endelea mbele. Kushindwa ni sehemu ya maisha.

 

50 Cent anasema kwamba kama unataka kufanikiwa sana kwenye maisha, basi unapaswa kushindwa mara nyingi kama ambavyo utafanikiwa. Hili linanikumbusha mwanasheria mmoja ambaye alikuwa anapenda sana kupamba mapambo ya kesi alizokuwa ameshinda ofisini kwake.

 

Siku moja aliulizwa, “inaonekana kwamba wewe huwa unashida kesi nyingi sana”. alisema kwamba hapana, ila ni hamsini kwa hamsini. Kesi nilizoshindwa na kupoteza ni sawa na zile nilizoshinda ila mimi huwa naweka mapambo ya kesi nilizoshinda ili kuwavutia watu kwangu zaidi wajue kwamba mimi ni wakili bora.

 

Rafiki yangu kwa leo naishia hapo. nikutakie kila la kheri.


Umekuwa nami rafiki yako wa ukweli Godius Rweyongez

Hakikisha Umesuscribe kwenye Channel yangu ya youtube kwa KUBONYEZA HAPA

Jiunge na mfumo wa kupokea makala maalumu kwa njia ya barua pepe kwa KUBONYEZA HAPA

Jipatie nakala za vitabu vyangu vya kiswahili kwa KUBONYEZA HAPA

Kama ungependa kujifunza kuhusu uandishi kutoka kwangu wasiliana nami kwa 0755848391

kila la kheri


One response to “Kutana Na Watu Watano Walioshindwa Karibia Kwenye Kila Kitu Na Bado Wakashinda Kwa Kishindo”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X