Mambo Matano Ya Kufanya Unapopata Fedha Nyingi Ambazo Hukutarajia


 

 

Karibu sana rafiki yangu kwenye makala ya siku ya leo ambapo ninaenda kukuonesha mambo matano ambayo unapaswa kufanya pale unpopokea fedha nyingi kwa wakati mmoja na hasa kama fedha hii hukuitarajia.

 

1. Usikikimbilie kutumia fedha hii. Ni wazi kuwa fedha hii haikuwa kwenye bajeti yako. Hivyo, kitu kikubwa ambacho unapaswa kufanya na fedha hii sio matumizi. Badala yake unapawa kuhakikisha kwamba fedha hii unaiwekeza sehemu. Chagua eneo moja ambapo utawekeza fedha hii ili hapo baadaye iweze kululetea fedha zaidi.

 

2. Tulia na endelea kuishi kama vile hiyo fedha hajaingia. Hiki ni kitu kigumu kufanya ila ni kitu ambacho unapaswa kukifanyia mazoezi hasa kama unataka kutengeneza utajiri. Ifikie hatua ambapo fedha yako ikiingia hautateteleka wala kukimbia kuitumia, badala yake utaendelea na maisha yako kama kawaida kama vile hakuna kitu kingine kimetokea.

 

3. Iweke kwenye gerezani. Hapa unaweza kutengeneza akaunti yako ambapo wewe unaweza kuweka fedha ila hauwezi kutoa. Inaweza kuwa ni akaunti ya benki au hata akaunti ya mpesa ambayo unamiliki wewe ila namba yake ya siri haujiui, isipokuwa inajulikana kwa mtu wako wa karibu au ndugu yako. Na mtu huyu hawezi kukupa namba ya siri hii isipokuwa tu pale ambapo utakuwa umefisha kiwango kikubwa ambacho ulimwambia mwanzoni wakati unafungua hiyo akaunti. Akishathibitisha kwamba, sasa umeweza kuweka akiba, kwa kiwango ambacho kinaendana na kile kiasi ambacho ulimwambia hapo hapo awali ndipo anaweza kukupa namba ya siri ili uweze kufuangua akaunti yako,

 

4. Weka juhudi zaidi ili kupata fedha nyingine. Ni wazi kuwa fedha huwa zinakuja kwa kila mtu ila rahisi zaidi kupata fedha unapokuwa na fedha kuliko unapokuwa hauna. Maana hata mawimbi ambayo unakua unatoa kwenye dunia ni mawimbi ya kuwa na fedha. Hivyo, fedha nyingine itakuja kwako kwa kufuata hayo mawimbi.

Sasa unapopata fedha , nenda kafanye kazi ili upate fedha nyingine zaidi. nenda katoe thamani zadi. Ni kosa kusubiri utumie fedha yako iishe kabisa na ubaki bila senti, ili ukumbuke kwenda kufanya kazi. ni kosa kubwa.

 

5. Jikumbushe malengo yako na ndoto yako ili uone vitu ambavyo unaenda kufanya na hiyo fedha kama vinaendana na malengo yako pamoja na ndoto zako. kama vitu ambavyo unaenda kufanya haviendani na malengo wala ndoto zako basi ni wazi kuna sehemu kuna tatizo, na wewe unapaswa kurirekebisha hilo tatizo kabla ya kutumia hizo fedha.

 

Rafiki yangu hayo ndio mambo matano ambayo unapaswa kufanya pale unapopata fedha ambayo hukutarajia.  Hakikisha unaingia kwenye channel yangu ya youtube na kuangalia somo hili hapa chini ambalo nimekuandalia.

Umekuwa nami rafiki yako wa ukweli Godius Rweyongeza

Hakikisha Umesubscribe kwenye Channel yangu ya youtube kwa KUBONYEZA HAPA

Jiunge na mfumo wa kupokea makala maalumu kwa njia ya barua pepe kwa KUBONYEZA HAPA

Jipatie nakala za vitabu vyangu vya kiswahili kwa KUBONYEZA HAPA

Kama ungependa kujifunza kuhusu uandishi kutoka kwangu wasiliana nami kwa 0755848391

 Kupata nakala ngumu ya kitabu cha KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI basi tuma ujumbe au piga kwa 0755848391

Kutengenezewa blogu yako kitalaamu tuwasiliane kwa 0755848391

kila la kheri




One response to “Mambo Matano Ya Kufanya Unapopata Fedha Nyingi Ambazo Hukutarajia”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X