Sheria Tano Za Nguvu Zitazokusaidia Kushinda Mengi Kwenye Maisha Ya Mtaani. Zifuate Kwa Faida Yako, Zivunje Kwa Hasara Yako


 

 

 

Pengine utakuwa umesoma 48 Laws of power kitabu kilichoandikwq na Robert Greene. Kama hujawahi kukisoma, basi baada ya kumaliza Kusoma andiko hili utapaswa kukitafuta na kukisoma. 50 CENT ni  mmoja wa wasomaji wazuri na watu waliotumia kitabu hiki kwa mafanikio makubwa sana. Hata hivyo, leo hatutaongelea kitabu hiki 48 Laws Of Power badala yake tunaenda kuuongelea kuhusu sheria tano zenye nguvu zitazokusaidia kushinda  mengi kwenye maisha ya mtaani. Zifuate sheria hizi kwa faida yako, au la zivunje kwa hasara yako.

Sheria utakazojifunza hapa, zina nguvu kubwa sana. hivyo kabla hujaanza kuzisoma naomba uzitumie sheria hizi kwa ustaarabu. Lakini pia fahamu mazingira sahihi ya kutumia kila sheria, sio kila sheria inatumika kila sehemu. Na pia fahamu pi akuwa watu wengine wanaweza kuzitumia sheria hizi ili kukunasa wewe. Hivyo, jifunze kwa umakini ili usije ukaingia kwenye mtego. Sheria namba nne ni muhimu kwako kuisoma

SHERIA YA KWANZA; Kama unahitaji mtu akubaliane na wewe, mguse kidogo Kwenye mkono wake

Hakuna kitu kizuri sana ambacho nimekuwa nafuatilia na bado naendelea kufuatilia kwa umakini wa hali ya juu kama lugha ya mwili. Mwili wa binadamu huwa unaongea mengi hata kama mtu haongei maneno. kwa kumwona tu mtu, hata kama hamjaongea, unaweza kujua kwamba huyu mtu angependa kuwa karibu nami au hapendi. Unaweza kujua kwamba huyu mtu ana furaha au amechukia au ana hasira na mengine mengi, mengi , mengi sana.

Ni wazi kuwa mtu ambaye huwa anaijua lugha ya mwili, ndiye ambaye huwa anaitumia kwa manufaa yake. Kama huijui basi watu wanaoijua watanufaika kutokana na kile ambacho mwili wako unakuwa unaongea na hivyo wanaweza kuamua kukupelekesha wanavyotaka ili kupata kile wanachotaka wao. Nimekuwa nikiwafundisha watu lugha ya mwili kwa muda mrefu, ila wiki hii nimekutana na kitu kikubwa chakuongezea kwenye uelewa nilio nao mpaka sasa.

Na kitu hiki ni kwamba unapokuwa kwenye mazungumzo na mtu na unataka mtu huyo akukukubalie pointi yako basi unapaswa kumshika kwenye mkono wake taratibu. Haupaswi kumshika mtu mkono wake kwa nguvu au kwa kulazimisha na wala haupaswi kuonesha kwamba unataka kumshika mkono wake. Yaani, kitu hiki kinapaswa kutokea kama vile hata wewe hujui ulichofanya. Kwa kufanya hivi unakuwa unasababisha kutolewa kwa kemikali kama dopamine, oxytocin na serotonin ambazo huleta furaha kwa mtu.


Na hii sio kwamba ni kitu cha kutunga bali tafiti mbalimbali zimethibitisha kitu cha aina hii pia.

Kwa mfano, jarida la lugha ya lugha mwili (Journal of Non Verbal Behavior) lilitafiti na kuona kuwa mtu anapomshika mwingine mkononi taratibu katika mizunguko mtaani, anakuwa na asilimia kubwa za kusaidiwa kutatuta kitu chake kilichopotea kulinganisha na yule ambaye hajamshika mwenzake mkononi.

Lakini pia taasisi ya Haiba na Saikolojia ya jamii (SOCIETY FOR PERSONALITY AND SOCIAL PSYCHOLOGY) iligundua kuwa wahudumu wanaowashika watu mkononi taratibu wanakuwa na nafasi kubwa ya kuuza zaidi ukilinganisha na wale ambao hawawashiki watu wengine.


Sasa kabla hujatoka hapa mbio na kwenda kuwashika watu kwenye mkono naomba uzingatia yafuatayo.

·         Sio kila sehemu kwenye mkono inapaswa kushikwa taratibu kama nilivyoeleza. Ila sehemu pekee ya kushika ni hii hapa chini kwenye picha

 

·         Usilazimishe kumshika mtu ambaye yuko mbali na wewe. Mshike yule tu aliye pembeni mwako.

 

·         Usioneshe kwamba umedhamiria kufanya hivyo, yaani inapaswa kuwa kama kitu kimetokea hata bila ya wewe kujua.

 

·         Usihame eneo moja kwenda jingine ili kumshika mtu mkononi

Na ukweli wa mwisho ni kwamba inafanya kazi zaidi hasa kwa watu wa jinsia tofauti.

 

SHERIA YA PILI; Unapokuwa katika kundi ambapo kila mtu anataka kusikika, wewe ongea tararibu

 

Kuna mazingira ambapo kila mtu huwa anataka asikike yeye tu. tena watu wengine huwa huwa mpaka wanaboa. Ikiletewa mada fulani mezani, yeye ndiye anakuwa wa kwanza kuchangia. Ikiongelewa siasa, anaijua. Ikiongelewa michezo, basi yeye anazjua timu tangu zilipoanzishwa. Wakiongelewa kuhusu matembezi au vyakula, basi yeye ndiye anataka kusikika. Tena wengine wataanza kukwambia habari za, “nilikuwa na mjomba wangu alipokuwa…”/ Yaani hakosi stori kwenye kila mada.

 

Sasa kwenye mazingira kama hayo ambayo kila mtu anataka kusikika, usipaze sauti yako na wala usihangaike kuongea sana ili watu wakusikie. Ongea taratibu na kwa kujiamini, inatosha.

Unajua kwa nini?

Kama kila mtu anaongea kwa sauti ya juu na anataka kusikika, wewe ukiongea kwa sauti ya chini inakuwa ni njia ya kujitofautisha. Watu watatega masikio ili wasikie unachoongea na wengine watasogeza vichwa vyao ili wakusikie unaongea nini. kwa kufanya hivyo, utakuwa umewanasa badala ya kupiga kelele na kuongea kwa sauti ya juu ili usikike.

 

Pia, watu hawapendi kupitwa, ukiongea kwa sauti ya chini watakuwa tayari kukusikiliza ili wasipitwe. Rafiki yangu hiyo ndiyo sheria ya pili yenye nguvu sana utakayopaswa kuifanyia kaz kuanzia leo hii.

 

SHERIA YA TATU; Kuwa mtulivu

 

Mara nyingi unapokuwa unaongea na watu au mpo kwenye kikao, yule mtu ambaye huwa anaongea huwa anaangalia watu kuonesha kama wanakubaliana naye. Na mara nyingi wale ambao wapo kwenye kikao huwa wanaonesha hilo labda kwa kutikisa kichwa wanapoangaliwa, au kwa kusongeza kiti mbele kidogo au kushangaa au hata kutoonesha dalili za kuliza swali. Mnenaji au mtu anayekuwa anaongea anapokuwa anaagalia watu anakuwa atafuta kukubaliwa miongoni mwa hao watu.

 

Lakini ebu chukulia kwamba wewe umemsikiliza huyu mtu anaongea muda wote ila hujatikisa kichwa, wala kusogeza kiti n.k. Ni wazi kuwa unaeanda kuonekana kama mtu wa tofauti. Na bosi wako au mtu anayenena kwa wakati huo, atataka kujua wewe ni mtu wa aina gani. Unaweza kufanya hivi kwenye kikao ofisini kwenu wakati bosi wako anaongea.

Hiki kitu kina faida na hasara zake.

Faida zake ni kwamba, kwanza utaonekana mwenye akili kwa kufanya hivyo. Lakini baada ya kikao hicho kama ni bosi wako ataendelea kukufuatilia kuona kweli huyu mtu ana akili kama nlivyomwona? Je, ni mchapakaz? Kama utadhihirisha hilo inaweza kuwa ni nafasi nzuri ya kula vinono kwenye kampuni unayofanyia kazi. inaweza kuwa nafasi nzuri ya kukufanya utengeneze konekisheni za maana.

Kinyume chake ni sahihi pia. Mtu anaweza kuwa anaonekana anakufuatilia wewe unapoongea ila haoneshi kuwa anakubaliana na wewe wala kukataa. Watu wakipiga makofi yeye hapigia na wala wakicheka hacheki au akicheka ni kidogo tu kisha anatulia, watu wakitikisa vichwa yeye hafanyi hivyo. Mtu wa aina hii utakuta kuwa anakuwa anatafuta umakini wako, maana hata wewe baada ya maongezi ni lazima tu, utatafuta kumjua mtu wa aina hii kuona ni kitu gani kipo ndani iyake. Kwa njia hiyo utajikuta umenasa kwake.

 

Hasara yake ni kwamba kama utashindwa kudhihirisha hizo akili ulizoonesha kwenye kikao unaweza kupoteza mpaka kazi yako, ikigundulika kuwa wewe ni mzembe kazini na hutoi matokeo ambayo yanatakiwa.

Lakini kwa kuwa naamini, wewe ni mtu ambaye unatoa thamani nzuri na kuchapa kazi, basi usteteleke, ebu nenda kaifanyie kazi kanuni hii hapa, ni wazi kuwa inaenda kukupa matokeo mazuri.

 

 

SHERIA YA NNE; Jidai Kama vile kitu ambacho watu wanakupa wewe hukitaki

 

Najua mara nyingi kuna vitu unakuwa unavihitaji kwelikweli, kiasi kwamba unakuwa tayari kufanya chochote ili kupata hicho kitu. Unakuwa tayari kufanya chochote kile ili uweze kupata ajira, unakuwa tayari kufanya chochote ili uwe kwenye mahusiano na mtu fulani, unakuwa tayari kufanya chochote ili fursa fulani isikupite na kuendelea na kuendelea. Hata hivyo, hapa tunaenda kuona kitu cha tofauti na vile ulivyozoea. Na kitu hiki ni kwamba unajidai HUTAKI KILE KITU.

 

Kinaweza kuonekana kama kitu cha kijinga ila kitu chenye nguvu sana. na kinaweza kuonekana kama hakiwezekani hasa kama wewe una uhitaji, ila ni kitu ambacho kinawezekana vizuri tu na kitakupa matokeo mazuri. Najaribu kukufikiria eti kwa mfano unaenda kwenye usaili na kazi hiyo unaihitaji sana halafu eti UJIDAI HUITAKI! Hahah, ngoja kwanza nikupe stori.

 

Bernie Mardoff ni mmoja wa watu kwenye historia hii ya dunia kuwahi kutengeneza mradi feki (PONZI SCHEME) na ambao umeweza kudumu kwa mrefu kuliko miradi mingine feki iliyowahi kutengenezwa. Pia ni mradi feki pekee kuwahi kukusanya fedha nyingi kuliko miradi mingine feki ililyowahi kuanzishwa. Bernie Mardoff alikusanya dola bilioni 64. Sasa aliwezaje kujenga mradi mkubwa na feki wenye fedha nyingi kiasi hicho, ilikuwa hivi.

 

Huu ulikuwa ni mradi wa kuwasaidia watu kuwekeza. Si watu wote wanaweza kuwekeza wao kama wao bila kuhitaji msaada. Hivyo, watu wengine huwa wanatafuta msaada wa watu wabobevu ili waweze kuwasaidia kuwekeza na hasa kwenye soko la hisa. Kwa hiyo, watu wanakuwa wanakupa fedha unawekeza, inapopatikana faida basi wewe unagawia faida wahusikakulingana na uwekezaji wao. Sasa na mradi wa Bernie Mardoff ulikuwa hivi hivi. Watu walikuwa wanampa fedha kwa ajili ya kuwekeza, ila kiufupi hizo fedha alikuwa haziwekezi sehemu yoyote. Badala yake alikuwa anaenda kula bata na kununua vitu vingine vya kwake. Lakini watu walikuwa wanaendelea kuja zaidi kwake ili awasaidie kuwekeza. Na alikuwa anapokea fedha za vishimba. Wachezaji wa mpira maarufu, wanamziki wenye majina yao, mabilionea, wamiliki wa timu za mpira wa kikapu na miguu n.k.Sasa alikuwa anawezaje kufanya hili hapa na wakati mradi wake ulikuwa feki? Je, kama alikuwa hawekezi fedha za kuwapa watu wengine endapo watazihitaji alikuwa anazipata wapi? Na je, gawio lao alikuwa analitoa wapi?

 

Yeye, alikuwa anajifanya hahitaji watu wapya kuwekeza naye. Yaani, kiufupi mpaka umpe fedha zako akusaidia kuwekeza ilikuwa ni vigumu sana. sana tu. kitu hiki kinaweza kuonekana cha kushangaza ukizingatia kwamba yeye alikuwa hawezekezi fedha, hivyo angehitaji watu zaidi waje kwake ili apate fedha ya kusaidia kulipa gawio na kuwalipa wale ambao walikuwa wanataka fedha zao zote. Ila hali haikuwa hivyo kwake, ili akusaidie kuwekeza fedha zako ulipaswa kuwa na konekisheni kubwa ya watu watakaokusaidia ili umfikie.

 

Lakini hata kama ungekuwa na konekisheni kubwa, bado  ulipokuwa unaenda kwake alikuwa hakukubalii kirahisi. Kwa mfano, mtu ameenda na dola milioni tano. Yeye alikuwa anakataa kuwa hawezi kupokea hicho kiasi na isitoshe nafasi zimejaa. Kwa hiyo kilichokuwa kinafuata watu wanaanza kumshawishi Bernie Mardoff ili awasaidie kuwekeza badala ya yeye kuwashawishi watu ili wampe fedha. Mtu aliyeenda na dola milioni tano alikuwa anarudi anajichanga mpaka anafikia labda dola milioni 15. Hapo ndio mardoff ndio alikuwa anakufikiria na hata bado alipokuwa anapokea fedha zako alikuwa anakwambia kwamba anakusaidia na usimwambia mtu. Hahah!

 

Watu waliokuwa wanawekeza kupitia kwake muda wote walikuwa wanapata faida, hivyo wakawa wanasambaza habari kwa wengine (japo waliambiwa wasimwambie mtu).  Kwa hiyo jamaa akawa anazidi kupata watu wengine zaidi. hivyo, ndivyo alikuwa anafanya Bernie Mardoff.

Kikubwa ninachotaka ujifunze kutoka kwake ni KUTOONESHA KWAMBA WEWE UNAKIHITAJI KITU hata kama unakihitaji sana, sana. kwenye hadithi hii fupi unaona wazi kuwa Benrie ndiye alikuwa anawahitaji watu ili kupata fedha. Maana alikuwa hawekezi hizo fedha wakati huohuo atakiwa kutoa gawio na kuna wengine watarudia kuchukua fedha zao zote. Kilichokuwa kinamfanya apate fedha zaidi ni kujifanya hazihitaji.

 

Sasa hii unawezaje kuitumia kwenye maisha yako ya kila siku.  Je, kwa mfano huo namaanisha kwamba na wewe uwe Bernie Mardoff anayefuata? Hapana! Ila napenda ufahamu kuwa unapaswa kupunguza hisia zako hata kama kitu unakihitaji sana. kadiri unavyoonesha kwamba kitu hukihitaji ndivyo watu watakuwa tayari kukushawishi ili wakupe zaidi.

 

Tuchukulie mfano mdogo. Tuseme kwamba leo hii ukiingia benki na kumwabia mkurugenzi hapo akuangalizie salio lako kwenye akaunti yako. Mkurugenzi akaangali na kukuta milioni mia tatu! Unaweza kuwa umeingia benki ukiwa mtu wa kawaida ila hicho kitendo cha wewe kuonekana una hizo fedha zote kutakuinua juu kidogo. na hata ukiomba mkopo ni rahisi kupewa maana tayari unaonekana kwamba wewe hata huwezi kuwa na shida ya kulipa. Japo inawezekana fedha hizo nikawa nimekupopesha mimi kwa muda ili ulingishie. Hahah

 

Achana na hizo mlioni mia tatu! Ebu turudi kabisa mpaka mtaani kwako. tuseme kwamba wewe unauza karanga. Utaitumiaje kanuni hii ya kujifanya hutaki kitu wakati unakitaka?

tuseme kwamba, wikendi hii umeenda sehemu kujirusha kidogo. na huko ukamkuta rafiki yako ambaye unajua kweli anazo fedha na ungehitaji kupata fedha kutoka kwake. Utafanyeje?

 

Unachoweza kufanya kwanza kabisa ni kuhakikisha kwamba wewe ndiye unahusika na kila kitu pale. Unalipia kila kitu bila kuteteleka (hapa nachukulia kwamba umeuza karanga na umepata walau elfu hamsini au laki). Na fanya ionekane kwamba fedha kwako sio tatizo. Baada ya muda, unaweza hata kuongelea gari lako la kisasa uliloacha nje. Au unaweza kuongelea kuhusu dereva wako au jinsi alivyochelewa kuja kukuchukua n.k. maneno na matendo yako yote yataonesha kwamba wewe sio mwenye njaa, kinyume kabisa na kile ulichodhamiria. Sasa huyo rafiki yako lazima tu atataka kujua unafanya kazi gani sasa hivi? Wewe unaweza kujibu tu kitu chochote ambacho utaona kwamba kinaweza kukujengea heshima pale na ambacho unaona kwamba kinaingiza fedha nyingi. Labda tuseme kwamba umesema, “ninamliki kampuni ya kuchimba madini”. Halafu umetulia.

Sasa huyu rafiki yako atataka kujua zaidi na atahitaji kuhoji zaidi. atakuuliza tena, “madini aina gani ambayo unachimba, unauza wapi? Kiufupi hapa yatajitokeza maswali mengi.

Wewe sasa utajibu, “kiufupi haya ni maelezo marefu, ila nina watu tunachimba dhahabu hapo Mererani na kuuza kwa wazungu, na hata hapa nimekuja kupumzika baada ya kutoka Afrika kusini”. Hahah, kumbe wewe mwenyewe Afrika kusini yenyewe unaisikia redioni tu!

 

Hapo kiufupi umeshatega mtego mzuri tu. mpaka hapo wewe utakuwa umeshakuwa Bernie Mardoff. Sasa hapo ndio utasikia anasema, aiseeh, na mimi unapaswa kunifanyia mchongo, ili na mimi nianze biashara ya madini. Hapo sasa unapaswa kujidai kama vile hujasikia vile. Unachukua bia yako na kunywa kidogo, kisha sasa ndio unakuja kumwambia.

 

Ni kweli nimewasaidia wengi. kwa kuwa wewe ni rafiki yangu nitakusaidia pia, ila utapaswa kulipa milioni kumi ili kila kitu kikamilishwe haraka.

Hivyo tu, na kwa vile ulishaonesha kwamba wewe fedha unazo. Huyu mtu atakuwa tayari kutoa hiyo fedha kwako ili umuunganishe.

 

Sijui umenielewa. Jitahidi sasa kuwa mtaarabu, usije ukaitumia hii siri kuiba fedha za watu. badala yake itumie kwenye vitu ambavyo vinafaa. Ningeweza kuendelea kukupa mifano zaidi, ila naishia hapa ili tuendelee na pointi nyingine. Kumbuka unaweza kuitumia kanuni hii kwenye biashara, kwenye mahusiano, kwenye michezo n.k yaani kila sehemu. Lakini pia kuwa makini watu wasije wakaitumia kwako ukajikuta kwamba umeingia kwenye biashara au kujihusisha na vitu ambavyo sio. Kuna watu wameuziwa viwanja feki kwa sababu walikuwa na haraka badala ya kututlia na KUJIDAI KAMA HAWATAKI.

 

Nimewahi kushuhudia watu wanatoka mjini na kuja vijijini na kuwashawishi watu kuwa watakuwa wanatoa mikopo kwa wamama wa vijijini, kisha wanawaambia hao wamama wachange fedha kiasi fulani (labda milioni moja) ili waweze kupewa kiasi kikkubwa zaidi (labda milioni kumi). Wamama wanajichanga na kufikisha h iyo fedha, mwisho wa siku wanaishia kutapeliwa. Hiyo yote ni kwa sababu hawakutaka KUJIDAI HAWATAKI HICHO KITU.

 

Ukijidai hutaki hicho wahusika watakushawishi wewe badala yaw ewe kuwashawishi.

 

SHERIA YA TANO; KAMA HAMUWEZI KUWA MARAFIKI, AFADHALI MUWE MAADUI.

 

Kuna watu wa aina mbili ambao huwa tunawaongelea maishani. Tunaowapenda na wale tunaowachukia. Ila kama mtu yuko katikati (humpendi wala humchukii), hutawezi kamwe kumwongelea.

 

Kwa hiyo, kuna wakati kama utaona imeshindikana kujenga urafiki na mtu basi utatakiwa tu kuweka nafasi ya kuonesha kuwa  kuna uadui. Mtu huyo atakuongelea zaidi wewe unapokuwa adui yako kuliko ambavyo angekuongelea kama usingekuwa adui yake.

 


One response to “Sheria Tano Za Nguvu Zitazokusaidia Kushinda Mengi Kwenye Maisha Ya Mtaani. Zifuate Kwa Faida Yako, Zivunje Kwa Hasara Yako”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X