Zamani nilipokuwa nikisikia neno mwekezaji basi nilikuwa najua lazima tu mwekezaji awe ametoka nje ya nchi. Lakini sasa hivi naujua ukweli.
Na ukweli huu ni kuwa wewe na Mimi tunaweza kuwa wawekezaji pia.
Unapoanza kuzungumzia uwekezaji wengi hufikiri kuhusu gharama za uwekezaji kuwa kubwa. Wengi wanadhani ili uwe mwekezaji basi unapaswa kuwa na kiwango kikubwa cha fedha. Naweza kusema ukweli halisi ni ndiyo na hapana. Unaweza kuwa mwekezaji hata kama una kiwango kidogo cha fedha. Bado unaweza kuwa mwekezaji hata kama una kiwango kikubwa pia.
Kuna maeneo mengi ya kuwekeza kuanzia kwenye hisa, hatifungani, vipande.
Kuna uwekezaji wa kwenye ardhi, nyumba, miti n k.
Uwekezajikwenye fedha za kigeni.
Uwekezaji kwenye biashara zinazoanza.
Kitu kikubwa na muhimu sana unapoamua kuwekeza ni kuwa unapaswa kupata maarifa sahihi kuhusu uwekezaji huo unaoufanya. Usianze kuwekeza bila ya luwa ma maarifa ya kutosha kuhusu kitu unachoenda kuwekeza.ukisikia watu wanasema uwekezaji fukani ni mzuri, usikimbikilie kuwekeza kabla hujatafuta masrifa sahihi kuhusu uwekezaji huo
NB. Uwekezaji wa hisa na vipande ni uwekezaji ambao unaweza kuufanya hata kama una mtaji kidogo.
Unaweza pia kuufanya hata kwa kutumia simu yako ukiwa nyumbani kwako
3 responses to “Inawezekana Wewe Kuwa Mwekezaji”
[…] Inawezekana Wewe Kuwa Mwekezaji […]
I need the book of Joel nanauka called timiza malengo soft copy
wasiliana na mwandishi