JITUME KWA FAIDA YAKO


 

Katika kazi yoyote ile unayofanya jenga utaratibu wa kujituma na kufanya kazi kwa bidii. Hata kama kazi hiyo siyo yako. Unapojituma humnufaishi mtu yeyote, unakuwa unajinufaisha mwenyewe.

Hata kama kazi umelipwa fanya zaidi ya vile unavyolipwa. Usiangalie manufaa ya muda mfupi badala yake angalia manufaa ya muda mrefu. Hivyo jitume zaidi kwa manufaa yako.

Kiufupi;
kama umeajiriwa, jitume kwa manufaa yako.
Kama unaimba, jitume kwa manufaa yako.
Kama unaandika, jitume kwa manufaa yako.
Kama unajitolea, jitume kwa manufaa yako.
Kama una kipaji Cha kucheza mpira, jitume kwa manufaa yako.

Kama huwezi kujituma, Kama huwezi kufanya kazi zaidi ya vile unavyolipwa, ni bora tu usiifanye hiyo kazi.

Kila la kheri.

SOMA ZAIDI: Jinsi Kufanya Kazi Kwa Bidii Kunabyoweza Kukukutanisha Na Wafalme

FANYA KAZI KWA BIDII

UKITAKA KUFANIKIWA NENDA KAUZE VYOTE ULIVYONAVYO


2 responses to “JITUME KWA FAIDA YAKO”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X