Kutoka Kwenye Ajira Mpaka Kujiajiri: HATUA 09 Za Kufuata Kutoka Kwenye Ajira Mpaka Kujiajiri


Leo nataka nikupe mwongozo muhimu ambao unaweza kuutumia katika kuanzisha biashara hasa ukiwa umeajiriwa. Ebu fikiria kwamba umeajiriwa leo hii na unataka uanzishe biashara yako ili ujiajiri.

Huu mwongozo ninaoenda kukupa hauna mfanano wake, kiufupi hakuna mtu mwingine ambaye amewahi kukwambia kitu Kama hiki, na wala hata hamna kitabu wala ebook ya kununua ambayo imefunguka kiundani kuhakikisha inakupa mwongozo sahihi kama huu.

Ukiufuata huu mwongozo utafika mbali. Ninachotaka ufahamu ni kwamba, kujiajiri siyo rahisi hata kidogo. Ndio maana watu wengi ambao wanafundisha kujiajiri wenyewe wameajiriwa.

Wengi wanaogopa sana kutoka kwenye ajira ambayo wameizoea na ambayo inawapa kipato cha uhakika kila mwishoni mwa mwezi mpaka kujiajiri na kumiliki biashara inavyoweza kujiendesha yenyewe na kuwapa kipato cha uhakika . Lakini inawezekana.

Sasa zifuatazo ni hatua za kufuata

HATUA YA KWANZA: Anza kwa kutengeneza ndoto kubwa ambayo ungependa kuifikia hapo baadaye

Hapa unapaswa kujua kwa uhakika kuwa ungependa kuwa nani hapo baadaye. Ni kweli Sasa hivi upo ajirani, ila picha yako ya hapo baadaye ni ipi. Ukiwa na maono au ndoto kubwa ni rahisi kupitia hatua nyingine zinazofuata kwa sababu tayari una ndoto kubwa ambayo inakusuma. Hii ndio picha yako na huo ndio mwongozo wako wa uhakika ambao unataka ufuate.

Sasa ebu jiulize nataka kufika wapi miaka mitano au kumi ijayo? Kaa chini ujipe muda wa kufikiri na kuandika chini ndoto yako.

Pasipo na maono watu huangamia. Kitu cha kwanza kitakachokuangamiza wewe ni kukosa ndoto kubwa. Siriazi, unahitaji ndoto kubwa.

Halafu kwa sababu nataka nikusaidie kwa ukamilifu ngoja nikwambie kitu hiki, hakikisha unajipa muda wa kuwa peke yako wa kukaa chini na kutafakari MAISHA YAKO. KAMA HUWEZI KUPATA UTULIVU KATIKA ENEO UNAPOKAA BASI TAFUTA ENEO UTAKAPOPATA UTULIVU NA KUFIKIRI KUHUSU MAISHA YAKO BILA YA  BUGHUDHIWA.

Unaweza hata kuamua kwenda kwenye hoteli na kununua maji au juisi ili tu upate mazingira tulivu yatakayokusaidia kufikiri na kujenga ndoto yako kubwa.

Hii ndio hatua ya kwanza. Ifanyie kazi hii kwanza.

HATUA YA PILI: ANZA KUWEKA AKIBA

Hiki ni kitu ambacho unapaswa kukifanyia kazi pia. Sasa tayari una ndoto kubwa ya kujiajiri hapo baadaye, Anza kujenga Tabia ya kuweka akiba. Kwa haraka wewe utahitaji kuweka akiba za aina mbili. Aina ya kwanza ni akiba  yako ya dharula. Hii ni Ile akiba ambayo inaweza kuendesha maisha yako kwa miezi isiyipungua sita endapo maisha yako yatapatwa na changamoto yoyote.

Unapaswa kuwa na aina hii ya akiba. Akiba ambayo endapo chochote kitatokea kwenye ajira yako basi utaweza kuendesha maisha yako bila hofu.

Aina ya pili ya akiba ni akiba sasa kuanzisha biashara. Nakuahauri Leo ukatengeneze akaunti yako ya benki ili uanze kuweka akiba. Kama ulikuwa hujaanza hakikisha hili suala unalipa kipaumbele kwenye maisha yako kuanzia sasa.

Kuna vitu au Tabia ambazo ulikuwa nazo kabla ya kufikiria kuanzisha biashara. Ila sasa hizi tabia unapaswa kuachana nazo. Ebu kaa chini na ufikirie juu ya tabia gani ambazo ulikuwa nazo ila siyo nzuri. Vitu kama kunywa pombe, kupoteza muda mtandaoni, kununua vitu ambavyo wewe mwenyewe huhitaji. Hivi ni vitu ambavyo utapaswa kuachana navyo.

Ngoja nikwambie kitu, hivi vitu ulikuwa unavifanya wakati umeajiriwa a kwenye ULIMWENGU wa kujiajiri vitakukwamisha sana. Yaani, huwezi kuendelea kupenda vitu vinavyokupa raha ya muda mfupi na bado ukapenda kujiajiri. KUJIAJIRI MAANA YAKE UMEAMUA KUWEKEZA MUDA WAKO, ELIMU YAKO, KATIKA BIASHARA AMBAYO UTAIKUZA KWA AJILI YA MANUFAA YA SASA NA  baadaye.

Wachezqji wa mpira wa miguu kuna vyakula hawali, kwa sababu tu ni wachezaji wa mpira wa miguu. Wengine wakila hivyo vyakula haviwadhuru ila wachezaji hawatakiwi kwa sababu wenyewe wamechagua aina fulani ya maisha. Wewe pia Kuna aina fulani ya maisha ambayo unapaswa kuishi. Kuna vitu fulani ambavyo wengine wanafanya ila kwa wewe mwenye ndoto ya kujiajiri hupaswi kuvifanya. Kwa wengine hivyo vitu ni sawa tu Ila kwako siyo sawa.

Na Kuna vitu ulikuwa hufanyi unapaswa kuanza kuvifanya, vitu kama kupenda kysoma vitabu, kutunza afya yako n.k.

Kama unataka kujiajiri haswa unapaswa kupenda kujifunza.  Kujifunza kunahusisha vitu vingi kama kusoma vitabu, kuangalia wengine wanavyofanya biashara yao na kupata funzo ambalo na wewe unaweza kulifanyia kazi kwenye biashara yako, kuwauliza wafanyabiashara wengine wanavyofanyia kazi, kuongea na wateja ili ujue wanachotaka wao.

Kiufupi unapojiajiri kujifunza kwako hakupaswi kuwa na ukomo. Mjasiriamali wa kweli huwa hana siku ya likizo. Kwake kila siku ni siku ya kujifunza kitu kipya ambacho atakifanyia kazi kwenye biashara yake.

Kupitia kujifunza utaweza kujua washindani wako wana nini na wewe kitu gani hauna. Kupitia kujifunza utapata kuona mpenyo ulipo na jinsi ambavyo unaweza kuutumia  KATIKA kuanzisha biashara mpya.

Wafanyabiashara wakubwa wote ni  wasomaji wazuri. Bill Gates anasemekana anasoma vitabu 52 kwa mwaka.
WARREN BUFFET HUWA ANATUMIA ASILIMIA 80 YA MUDA WAKE KWENYE KUSOMA. Kiukweli kwa wafanyabiashara wengi kusoma kwao ni  nguzo muhimu ya kukuza biashara zao.

Elon Musk ni bilionea mkubwa kwa sasa akiwa ni tajiri nambari moja duniani. Ila historia ya huyu jamaa ni historia yenye mafunzo makubwa ndani yake. Ameanzisha na mpaka sasa anaendesha BIASHARA ambazo hapo mwanzoni alikuwa hajui chochote kuhusu hizo biashara, ila sasa hivi anaziendesha vizuri na kwa manufaa makubwa Sana. Unajua kwa nini? Kwa sababu ya tabia yake ya kupenda kujifunza. Yaani, kujifunza hakujawahi kumwangusha mtu. Ebu na wewe kujaribu.

Hapa Sasa tunakuja kwenye kipengele kingine muhimu sana kwako. Sasa ni muda wa kujua Aina ya biashara ambayo unaenda kuanzisha. Unahitaji wazo la biashara.
Je, unapataje wazo la biashara?

Wazo lako la biashara linaweza kutokana na  ujuzi wako au taaluma yako. Tuseme kwa mfano wewe ni mwanasheria, unaweza kutumia ujuzi wako wa sheria kwa ajili na kuanzisha biashara inayoendana na ujuzi wako.

Au labda wewe ni dakatarj. Unaweza kuanzisha biashara inayoendana na ujuzi wako.

Kama una uzoefu KATIKA eneo au kitu fulani unaweza kuanzisha biashara kwenye hicho kitu pia.

Unaweza pia kutumia wazo lililopo kwa Sasa kuanzisha biashara yako. Kuna biashara ambazo watu wengine wanafanya na wewe unaweza kufanya biashara kama hiyo, Ila sasa zamu hii kwa ubora au kwa kuongeza vionjo fulani ambavyo vitakutofautisha.

Angalia vitu unavyopenda. Unapenda mpira, Kuna biashara inayoenda na hilo unavyoweza kufanya.
Unalenda muziki? Kuna biashara inayoendana na hiyo unavyoweza kufanya.

Matatizo yanayowakumba watu pia Ni biashara.
Nimeandika sana kuhusu namna unavyoweza kupata wazo la biashara, kwa kuanzia unaweza kusoma Makala hizi hapa kwenye blogu hiihii.

Lakini pia Kuna biashara au mahitani ambayo ni ya asili. Ni mahitani AMBAYO watu kwa asili wanayahitaji. Chakula, mavazi na malazi.
Nashauri pia usome ebook yangu inayoeleza SEKTA 11 ZA KUTENGENEZA MAMILIONI YA FEDHA TANZANIA. Rusha elfu tano kwa 0755848391 nikutumie ebook hii.

Sasa tayari umeshapata wazo la biashara, lakini pia kama ni mtaji tayari unao. Sasa kifuatacho ni wewe kuanzisha biashara.

Kitu muhimu ninachotaka kukwambia hapa ni kwamba umetangaza vita kubwa. Kama ni maji basi umeyavulia nguo. Sasa kifuatacho ni kuyaoga.

Ikumbukwe kwamba bado una AJIRA lakini pia una BIASHARA. Ni vitu viwili vinavyokuhitaji.

Biashara yoyote changa inakuhitaji Sana. Hivyo, utapaswa kwanza kuhakikisha kwanza unafanya kazi (AJIRA) yako vizuri. Fika ajirani kwako kwa wakati, fanya kazi kwa bidii na kwa ubora wa hali ya juu.

Halafu tumia muda wako wa ziada kufanya biashara yako. Huu unaweza kuwa ni asubuhi sana kabla hujaenda ajirani au jioni mara tu baada ya kutoka ajirani.

Ni kweli utachoka lakini sasa hiyo ndiyo gharama AMBAYO utapaswa kuilipa ili kuweza kuvifanikisha biashara yako.

Muda ule uliokuwa unatumia kuzurura mtandaoni, Sasa ni muda wa biashara yako. Muda ule uliokuwa unautumia kunywa pombe au kupiga soga na washikaji, sasa ni muda wako wa biashara.

Hiki kitu kinawezekana na ubora ni kwamba wewe siyo wa kwanza kufanya hivyo. Lakini pia ubora zaidi mimi nipo kukusaidia kwenye hili, nitahakikisha nakushika mkono mwanzo mwisho. Nashauri ujiunge na kundi langu la THINK BIG FOR AFRIKA ili tuendelee kuwa karibu sana muda wote.

HATUA YA SABA: TUNZA HESABU ZOTE ZA BIASHARA VILIVYO
Endesha biashara yako kitalaamu kuanzia siku ya kwanza. Kinachokwamisha biashara nyingi na wafanyabiashara wadogo ni kukosa mfumo mzuri wa kuwasaidia kutunza hesabu za biashara. Rafiki yangu, anza biashara yako vizuri.

Ebu chukulia kama ndio ungekuwa unaenda kuiuza biashara yako ndani ya mwaka mmoja. Na wanunuzi wa biashara yako wanahitaki kuona fedha zote zilizoingia kwenye biashara na jinsi zilivyotumika.

Na hesabu nzuri za kuanza kutunza ni hesabu za mapato na matumizi.
Ukiweza kutunza hizo kwa kuanzia, utafika mbali.

Ikumbukwe kuwa maisha ya ya kujiajiri ni tofauti kidogo na maisha ya ajira. Unapoajiriwa unakuwa chini ya bosi wako. Ila ukijiajiri wewe mwenyewe ndiye unakuwa bosi wako.

Ajirani unapaswa kuwahi kwa sababu usipowahi kuna adhabu au madhara yatatokea. Ila sasa wewe mwenyewe ndiye bosi wako mwenyewe. Ni au unafanya au hufanyi.  

Wewe mwenyewe ndiye unapaswa kujifuatilia, wewe mwenyewe ndiwe unapaswa kuhakikisha majukumu ya biashara yako yamefanyika bila kuachwa.

Jisimamie na jisukume kwa siku za kwanza kuhakikisha unafika mbali. Ukitoboa hapa, ni wazi kuwa utajiwekea historia yako ya kipekee sana

Kazi kubwa unayopaswa kupambana nayo baada ya kuanzisha biashara ni kuhakikisha inakua na inaweza kukuingizia kipato kikubwa kila mwezi ambacho ni kikubwa ni sawa au kinakaribia kile cha mshahara uliokuwa unaupokea.

Ukishafikia hii ngazi Sasa ndipo unaweza kufikiria kuacha ajira yako na kuweka nguvu kwenye biashara yako.

Hili linaweza lisiwe suala au kitu ambacho unaweza kukamilisha ndani ya muda mfupi. Ila kinawezekana. Na ndio maana tangu mwanzo nimekwambia uwe na  ndoto kubwa,  kazi yako utakuwa ni kupambana ili ufikie ndoto yako kubwa.

Rafiki yangu ngoja, nikwambie kitu. Hizi hatua zinaweza kuonekana nyingi, Ila ukweli ni kwaamba inawezekana na hiki ndio kitu ambacho nimesisitiza tangu mwanzo mpaka hapa ninapohitimisha makala hii. Rafiki yangu, inawezekana kujenga biashara na ukaisimamisha ukiwa umeajiriwa.

Karibu sana tufanye kazi kwa pamoja. Nashauri ujiunge na kundi langu la THINK BIG FOR AFRIKA. Ambapo utakuwa karibu nami na utajifunza zaidi kuhusu biashara. Jiunge na THINK BIG FOR AFRIKA kwa kuwasiliana nami kupitia 0755848391

Rasilimali nyingine unazohitaji ni:

Kitabu cha KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI (15,000) (Hardcopy &soft copy)

JINSI YA KUFIKIA NDOTO ZAKO (20,000/-) Hardcopy &soft copy)

MAAJABUYA KUWEKA AKIBA (5,000/-) soft copy

MAMBO 55 YA KUZINGATIA KABLA YA KUANZISHA BIASHARA (5,000/-) soft copy.



6 responses to “Kutoka Kwenye Ajira Mpaka Kujiajiri: HATUA 09 Za Kufuata Kutoka Kwenye Ajira Mpaka Kujiajiri”

  1. Waow!!! Hii elimu ni ya kipekee sana kwa kila mtu mwenye malengo ya kuanzisha maisha binafsi ya kujiajiri. Ubarikiwe kaka kwa kazi yako.

  2. E bhana asante kwa nondo za nguvu, upo vzr mtu wangu ubarikiwe kwa kutuonyesha njia, Ubarikiwe nitazidi kufuatilia mada mbali mbali kwa kukaa vzr zaidi, Asante kwa somo ni zuri sana, Barikiwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X