Aina 5 Za Nidhamu Unazopaswa Kuwa Nazo


Siku siyo nyingi sana niliakuandikia makala maalumu kukueleza maana halisi ya nidhamu. Kama hukubahatika kufuatilia makala hii basi ni muhimu kwako kuhakikisha kwamba unabonyeza HAPA ili kuifuatilia makala hii kwanza.

 

Sasa baada ya wewe kuwa umeijua maana halisi ya nidhamu, siku ya leo ningependa ufahamu aina tano za nidhamu unazopaswa kuwa nazo ili kuweza kufanikisha malengo yako na kila kitu ambacho umepanga.

Aina ya kwanza ya nidhamu unayopaswa kuwa nayo ni nidhamu ya kazi. fanya kazi unapopaswa kuifanya bila kukosa.

Pili, ni nidhamu ya fedha. Tekeleza mipango yako yote ya kifedha kama ulivyoipanga.

Tatu, ni nidhamu ya muda, heshimu sana muda wako. Maana ukiupoteza huu muda wako ujue kwamba hautakuwa na namna nyingine ambayo unaweza kuitumia kuhakikisha umeurudisha. Unaweza kupoteza vitu vingine vyote, baadaye ukaja kuvipata ila ukipoteza muda ujue kwamba hautapata kamwe.

Nne, ni nidhamu ya uwekezaji. Chagua maeneno muhimu ambayo utajikita kuwekeza na wekeza huko. Anza kuwekeza kidogo, kisha endelea kuwekeza bila kuchoka. Kumbuka haba na haba hujaza kibaba.

Tano, nidhamu ya kujifunza na kusoma. Amua kabisa kwamba ninaenda kusoma na kujifunza kila siku bila kujali kitu gani kinatokea kwenye maisha yangu. Ukijifunza utajua mengi kwenye maisha yako yatakayokusaidia wewe kuweza kuendelea kusonga mbele na hata kufanikisha mambo mengine makubwa kwenye maisha yako.

 

Nakushukuru sana kwa kuweza kusoma andiko hili mpaka mwisho. Umekuwa nami rafiki yako wa ukweli Godius Rweyongeza

Hakikisha Umesubscribe kwenye Channel yangu ya youtube kwa KUBONYEZA HAPA

Jiunge na mfumo wa kupokea makala maalumu kwa njia ya barua pepe kwa KUBONYEZA HAPA

Jipatie nakala za vitabu vyangu vya kiswahili kwa KUBONYEZA HAPA

Kama ungependa kujifunza kuhusu uandishi wa vitabu kutoka kwangu wasiliana nami kwa 0755848391

 Kupata nakala ngumu ya kitabu cha KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI na kitabu cha JINSI YA KUFIKIA NDOTO ZAKO basi tuma ujumbe au piga kwa 0755848391

Kutengenezewa blogu yako kitalaamu tuwasiliane kwa 0755848391

kila la kheri

Kunialika kwa ajili ya kutoa mafunzo au semina kwenye kikundi chako, taasisi, kongamano n.k. wasiliana nami kwa email: songambele.smb@gmail.com au simu 0755848391



One response to “Aina 5 Za Nidhamu Unazopaswa Kuwa Nazo”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X