Sifa mbili ambazo ukiwa nazo, basi mafanikio kwako ni suala la muda tu


Siku ya leo ningependa nikueleze sifa mbili ambazo ukiwa nazo, basi ujue kuwa mafanikio kwako litakuwa ni suala la muda tu. unajua sifa hizi ni zipi..

Sifa ya kwanza ni sifa ya kufanya kazi kwa bidii

Hakuna kitu chochote kile unachoweza kupata bila ya kufanya kazi, tena siyo tu kufanya kazi, bali kuhakikisha kwamba umefanya kazi kwa bidii na kwa kujituma.

Kama rafiki yangu haufanyi kazi kwa bidii na kwa kujituma, sichelei kusema kwamba utasubiri sana kuweza kufikia mafanikio ambayo unapenda kufikia maishani mwako

Sifa ya pili ni nidhamu

Hii ni sifa nyingine muhimu sana, nidhamu yako itakuwezesha kufanikisha mambo mengi ambayo hakuna watu wengine wanaweza kufanikisha.

Unahitaji kuwa na nidhamu kuanzia kwenye kazi yenyewe.

Nidhamu ya pesa

Nidhamu ya muda

Yaani, nidhamu kwenye kila kitu. Na kwa kuwa watu wengi hawaelewi nidhamu  ni nini, niliwahi kuandaa makala inayoonesha kuwa nidhamu ni kitu gani, naomba uiangalie ili uweze kujua nidhamu ni kitu gani. BONYEZA HAPA kuiangalia

lakini pia kuna makala ambayo niliwahi kuandaa inayoonesha aina tano za nidhamu unazopaswa kuwa nazo. BONYEZA HAPA kuisoma pia

Kama bado hujasubscribe kwenye channel yangu ya youtube basi fanya hivyo sasa hivi.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X