Hivi ukisikia mtu anasema mtu fulani ana nidhamu au hana nidhamu anakuwa anamaanisha nini? Je, wewe una una nidhamu? Au ndio ulishasahau mambo ya kuwa na nidhamu tangu ulipohitimu shule? Siku ya leo naomba ufahamu kwamba nidhamu, ni pale unapoamua kufanya kitu kwa utaratibu fulani na ukakifanya bila kuacha.
Umeamua kuwa kila siku utaamka alfajiri saa 11, na unahakikisha unafanya hivyo bila kujali siku hiyo inanyesha au ni jua kali, hiyo ndiyo nidhamu.
Umepanga kuweka akiba ya kiasi fulani cha fedha kila unapopata mshahara, unakiweka bila kujali mwezi huo una matumizi na mambo mengi yanayohitaji fedha au la!
Umeamua kufanya mazoezi kwa dakika kadhaa kila siku au kila wikendi, unafanya hivyo bila kujali siku hiyo una wageni au upo ugenini.
Orodha inayoonesha vitu vya aina hii inaweza kuwa nyingi sana ila walau msingi mkubwa wa nidhanu ndiyo huo.
Nikukumbusha tena; nidhamu, ni pale unapoamua kufanya kitu kwa utaratibu fulani na ukakifanya bila kuacha bila kujali kitu gani kinatokea au kimetokea.
Kazi ya kufanya siku ya leo.
Chagua kitu kimoja hata kama ni kidogo sana (hata kama ni kuweka akiba ya shilingi 100 kola siku). Kisha azimia kukifanya kila siku au kila wiki bila kuacha. Na ukifanye kweli kwa mwaka mmoja ujao.
Nakutakia kila la kheri.
SOMA ZAIDI:
Viashiria Vitano (05) Vitakavyokufanya Uendelee Kuwa Maskini Maisha Yako Yote
Nakushukuru Sana kwa kuweza kusoma andiko hili mpaka mwisho. Umekuwa nami rafiki yako wa ukweli Godius Rweyongeza
Hakikisha Umesubscribe kwenye Channel yangu ya youtube kwa KUBONYEZA HAPA
Jiunge na mfumo wa kupokea makala maalumu kwa njia ya barua pepe kwa KUBONYEZA HAPA
Jipatie nakala za vitabu vyangu vya kiswahili kwa KUBONYEZA HAPA
Kama ungependa kujifunza kuhusu uandishi kutoka kwangu wasiliana nami kwa 0755848391
Kupata nakala ngumu ya kitabu cha KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI na kitabu cha JINSI YA KUFIKIA NDOTO ZAKO basi tuma ujumbe au piga kwa 0755848391
Kutengenezewa blogu yako kitalaamu tuwasiliane kwa 0755848391
kila la kheri
One response to “Hii Ndiyo Maana Halisi Ya Nidhamu”
[…] Yaani, nidhamu kwenye kila kitu. Na kwa kuwa watu wengi hawaelewi nidhamu ni nini, niliwahi kuandaa makala inayoonesha kuwa nidhamu ni kitu gani, naomba uiangalie ili uweze kujua nidhamu ni kitu gani. BONYEZA HAPA kuiangalia […]