Sababu Tano Kwa Nini Afrika Ndiyo Eneo Pekee Unapoweza Kutengeneza Mabilioni ya Fedha Zaidi Ya Eneo Jingine Hapa Duniani


 

Kabla ya julai 2016, nilikuwa napenda sana kufuatilia taarifa ya habari. Na mara kwa mara nilipokuwa nikisikiliza taarifa ya habari nilisikia  wakitangaza kuwa kuna watu wamekamatwa wakijaribu kuingia Ulaya kinyume na utaratibu au pengine walisema kuna maelfu wameaga dunia baharini  wakati wanavuka kuingia Ulaya. Wote hawa walikuwa wanaenda huko ili kutafuta maisha mazuri au kutafuta zilipo fursa na fedha. Kiufupi walikuwa wanaenda huko ili wapate maisha mazuri.

Lakini ukweli ni kuwa Afrika ndipo kuna fedha na wala hupaswi kuhangaika kuzitafuta kwingineko. Zifuatazo ni sababu tano kwa nini, ukisoma andiko hili mpaka mwisho, utakutana na sababu ya nyongeza kama zawadi yangu kwako siju ya leo.

1. MATATIZO YA AFRIKA NI MAKUBWA KULIKO ENEO JINGINE HAPA DUNIANI
Afrika ina matatizo makubwa yanayohitaji suluhisho kuliko ENEO JINGINE HAPA DUNIANI. Na matatizo siku zote ndiyo yamebeba fedha. Ukiweza kutatua MATATIZO YA WATU, haohao watu uliowasaidia kutatua MATATIZO YAO, watakuwa tayari kukulipa ili waendelee kupata suluhisho la matatizo yao. Hakuna sehemu nyingine unapoweza kukuta matatizo kama yaliyo Afrika.

2. IDADI YA WATU INAZIDI KUONGEZEKA KILA SIKU
Idadi ya watu Afrika inazidi kuongezeka kila kukicha. Kwa sasa Afrika ina zaidi ya watu bilioni 1.2 na idadi hii inategemewa kuongezeka mpaka bilioni 1.7 kufikia 2030. Idadi hii inahitaji huduma za kijamii ambazo bado hazijafika kila sehemu. Hii Ni fursa ya kutumia kama unataka kutengeneza mamilioni na hata mabilioni. Hakuna sehemu nyingine ya dunia utaenda ukakuta huduma za kijamii zinahitajika kama Afrika.

Sambamba na hilo kadiri idadi ya watu inavyoongezeka, kutatokea matatizo mapya na haya matatizo mapya yatahitaji suluhisho pia. Hiki kitu kwa vyovyote kinanifanya nijue waziwazi kuwa Afrika ndiyo sehemu unapoweza kutengeneza fedha kuliko ENEO JINGINE. Fedha zako wanazo hao watu bilioni 1.2. 

 Unaweza kupenda kitabu changu cha SEKTA 12 ZA KUTENGENEZA MABILIONI YA FEDHA TANZANIA. Wasiliana Nami kwa 0755848391 kukipata.

3. UNAWAJUA WAAFRIKA KULIKO UNAVYOWAJUA WENGINE
Hakuna watu unawajua kiundani Kama WAAFRIKA wenzako. Umekua nao, umecheza nao, umekula nao. Umewasikiliza mara nyingi wakiwa wanalalamika, hivyo haya yote yanafanya iwe rahisi kuanzisha kitu kitakachowasaidia WAAFRIKA KULIKO unavyoweza kuanzisha kitu kikagusa maisha ya watu sehemu nyingine utakapohamia.

4. SOKO LA AFRIKA HALIJAFURIKA
Maeneo mengine nje ya Afrika yamefurika bidhaa za kila aina kiasi kwamba ukianzisha kitu, kitachukua muda kuifikia nafasi ya kwanza au nafasi ya pili. Au kinaweza kisifikie viwango hivyo. Hata hivyo, kwa kuwa soko la Afrika halijafurika, ukianzisha biashara au ukigundua kitu, uwezekano wa kitu hicho kuwa namba 1 au 2 upo njenje.

5. NI SEHEMU PEKEE UNAPOWEZA KUANZIA SIFURI MPAKA MAFANIKIO MAKUBWA
Uwepo wa rasilimali nyingi barani Afrika unaifanya Afrika iwe sehemu pekee unapoweza kuanza kitu kwa gharama ndogo sana, au hata ukaanzia sifuri mpaka ukafikia mafanikio makubwa.

Wakati washindani wako watakuwa wanakuja kuchukua malighafi hapa Afrika, wewe utakuwa unachukua hapa na kuzitumia pale.

Sababu ya Nyongeza

6. WATU WENGINE WANAKIMBIA NCHI ZAO KUJA AFRIKA PIA
Kuna watu wengi wanaokimbia sehemu nyingine kuja Afrika kuanzisha maisha. Sasa iweje wewe ukimbie huku kuelekea eneo jingine?

Hizo hapo ndizo Sababu Tano Kwa Nini Afrika Ndiyo Eneo Pekee Unapoweza Kutengeneza Mabilioni ya Fedha Zaidi Ya Eneo Jingine Hapa Duniani. Wakati naandika makala hii nimekumbuka hadithi ya mtu aliyeuza shamba la almasi kwenda kutafuta almasi. Nikaona kuwa kuikimbia Afrika ni sawa na kukimbia sehemu ilipo almasi ili kwenda kutafuta Almasi. Unaweza kujifunza zaidi kuhusu mtu huyu aliyeuza shamba la almasi kwenda kutafuta almasi HAPA

NakNakushukuru sana kwa kuweza kusoma andiko hili mpaka mwisho. Umekuwa nami rafiki yako wa ukweli Godius Rweyongeza

Hakikisha Umesubscribe kwenye Channel yangu ya youtube kwa KUBONYEZA HAPA

Jiunge na mfumo wa kupokea makala maalumu kwa njia ya barua pepe kwa KUBONYEZA HAPA

Jipatie nakala za vitabu vyangu vya kiswahili kwa KUBONYEZA HAPA

Kama ungependa kujifunza kuhusu uandishi wa vitabu kutoka kwangu wasiliana nami kwa 0755848391

 Kupata nakala ngumu ya kitabu cha KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI na kitabu cha JINSI YA KUFIKIA NDOTO ZAKO basi tuma ujumbe au piga kwa 0755848391

Kutengenezewa blogu yako kitalaamu tuwasiliane kwa 0755848391

kila la kheri

Kunialika kwa ajili ya kutoa mafunzo au semina kwenye kikundi chako, taasisi, kongamano n.k. wasiliana nami kwa email: songambele.smb@gmail.com au simu 0755848391


One response to “Sababu Tano Kwa Nini Afrika Ndiyo Eneo Pekee Unapoweza Kutengeneza Mabilioni ya Fedha Zaidi Ya Eneo Jingine Hapa Duniani”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X