Je, kizazi kijacho cha Mabilionea wa Afrika kitatokea wapi?


Takwimu zilizotolewa na gazeti la Forbes ni kwamba karibia bilionea mmoja anatengenezwa kila baada ya dakika moja. Hii Ndio kusema kwamba fursa za kutengeneza mabilionea zaidi zinazidi kuongezeka.

Nafasi ya wewe kutengeneza ubilionea pia ipo, lakini endapo tu utaifahamu na kuiishi misingi na kanuni za kibilionea.

Sababu Tano Kwa Nini Afrika Ndiyo Eneo Pekee Unapoweza Kutengeneza Mabilioni ya Fedha Zaidi Ya Eneo Jingine Hapa Duniani

Kwa leo ninataka nikuelekeze eneo ambapo mabilionea wajao wa Afrika watatokea. Yapo maeneo 11 kama ambavyo nimeyaeleza kwenye kitabu Cha SEKTA 11 ZA KUTENGENEZA MAMILIONI YA FEDHA TANZANIA ila kwa Leo na kwa ufupi sana nataka nizungumzie eneo moja tu.

Kilimo. Afrika imebarikiwa kuwa na ardhi nzuri yenye kilimo.

Idadi ya watu Afrika inazidi kuongezeka kila siku. Na watu hawa wanahitaji kula.

Mambo mengine yanaweza kubadilika ila kula kutabaki palepale. Pengine MATUMIZI ya mtandao wa intaneti yanaweza kubadilika ila hatutaacha kula.

Idadi ya watu duniani kwa ujumla pia inazidi kuongezeka na ongezeko hili linahitaji chakula pia.

Kwa misingi hiyo basi, sisiti kusema kwamba kilimo ni mojawapo ya eneo ambalo linaenda kutengeneza mabilionea wapya Afrika. Kwenye ebook ya SEKTA 11 ZA KUTENGENEZA MAMILIONI YA FEDHA TANZANIA nimeeleza kwa kina hili.

Ila kwa hapa itoshe tu kusema kuwa kilimo Ni SEKTA muhimu sana ya kuangalia kwa jicho la pili.

Ndio maana mimi nimeshaanza harakati zangu za kuhakikisha kwamba natengeneza mabilioni yangu huku.

Mfano mzuri tu hapa Tanzania. Kuna mazingira yanayoruhusu kuzalisha karibia kila zao. Lakini cha ajabu ni kuwa unaweza kwenda supermarket na kukuta kuna mazao ya nje ya nchi yanauzwa.

Wewe kama kijana unaweza kuchagua baadhi ya mazao na kukomaa nayo, ukayazalisha kwa viwango vizuri kiasi cha kuweza hata kusafirisha nje ya nchi.

Hivyo, ukaliteka soko la ndani na nje ya nchi. Upo tayari kwa ajili ya hii safari.MAFUNZO ZAIDI


2 responses to “Je, kizazi kijacho cha Mabilionea wa Afrika kitatokea wapi?”

  1. Ahsante kwa makala yako, ila siamini kama kilimo Africa kinaweza kutengeneza bilionea ulaya sawa.

    kwanini wakulima Africa nadhani ni asilimia 70 na…haipungui 70 naamini hivyo…cha kusikitisha karibia wote ni illiterate. hiyo pekee ni sababu tosha kabisa ya kilimo Africa kamwe haiwezi kutengeneza billionea..

    Sababu nyingine kubwa ni gate keepers ambao wao ndiyo wanapanga bei..bila hilo tatizo kuondolewa kilimo Africa kitabaki kuwa ni ngazi ya matajiri wachache kuendelea kuwa mabilionea na huku wakulima wakibaki kuwa maskini wa kutupwa..

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X