Ninawezaje kununua hisa na ninatakiwa kuwa na shilingi ngapi?


 

Inategemea unanunua hisa za kampuni gani.  Kuna hisa ziko juu kwa bei na nyingine ziko chini.

Hivyo kiwango kitatofautiana ila ukiwa na fedha ya hisa kumi, unaweza kununua.

Iko hivi. Tuseme wewe unapenda kununua hisa za kampuni SMB (SONGA MBELE BLOG). Hahah! Halafu, hisa za kampuni hii zinazuzwa kwa shilingi 500 kila hisa. Hii ndiyo kusema kwamba ukiwa na elfu 5 Tu unaweza kununua hisa za kampuni hii.

Na Kama utapenda kununua hisa za kampuni WIN, ambazo hisa moja inauzwa kwa shilingi elfu Saba, utatakiwa walau kuwa na elfu sabini ili uweze kununua kiwango cha chini cha hisa kumi.

Ndiyo maana inashauriwa sana wakati unachagua kununua hisa, usichague zile ambazo zina bei kubwa hasa kwa wewe unayeanza. Chagua zenye bei ndogo ila zenye mwelekeo wa kukua.

Kwa mifano yetu miwili happy juu, hisa za kampuni ya SMB, Kama zina mwelekeo wa kukua zinaweza kuwa nzuri kwa mtu anayeanza.

Najua wengi wanaposikia kuhusu hisa wanajua unapaswa kuwa na fedha kuubwa, ila ukweli ndio Kama unavyouona hapo. Hakuna mbwembwe zaidi. Ushindwe wewe tu.

Nakushauri sana, upate ebook yangu inayoitwa MAAJABU YA KUWEKEZA KWENYE HISA. kwa elfu 4 tu, itakusaieia Sana na kukupa mwongozo wa kuwekeza kwenye hisa.

JINSI YA KUNUNUA HISA

Hisa za zinazouzwa kwenye Soko la Hisa La Daressalaam huuzwa kupitia madalali, hivyo unapaswa kuingia kwenye tovuti yao na kuwaangalia madalali waliopo, Kisha kuchagua dalali mmoja utakayekuwa unamtumia. 

Unaweza kuwasiliana na dalali unayeona anakufaa ili uweze kutimiza ndoto yako ya kuwekeza.

Madalali wengi wana makao yao makuu kwenye jiji la Daressalaam, hata hivyo wengine wana mawakala mikoani na wengine wana mawakala karibia kila mkoa.

Nakushukuru sana kwa kuweza kufuatilia somo hili mpaka mwisho. Umekuwa nami rafiki yako wa ukweli Godius Rweyongeza

Hakikisha Umesubscribe kwenye Channel yangu ya youtube kwa KUBONYEZA HAPA

Jiunge na mfumo wa kupokea makala maalumu kwa njia ya barua pepe kwa KUBONYEZA HAPA

Jipatie nakala za vitabu vyangu vya kiswahili kwa KUBONYEZA HAPA

Kama ungependa kujifunza kuhusu uandishi wa vitabu kutoka kwangu wasiliana nami kwa 0755848391

Kupata nakala ngumu ya kitabu cha KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI na kitabu cha JINSI YA KUFIKIA NDOTO ZAKO basi tuma ujumbe au piga kwa 0755848391

Kujifunza namna ya kutengeneza fedha kupitia blogu tuwasiliane kwa 0755848391

Kunialika kwa ajili ya kutoa mafunzo au semina kwenye kikundi chako, taasisi, kongamano n.k. wasiliana nami kwa email: songambele.smb@gmail.com au simu 0755848391One response to “Ninawezaje kununua hisa na ninatakiwa kuwa na shilingi ngapi?”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X