Tabia Tano Unazopaswa Kujijengea Ili Ufanikiwe Mara Kumi Zaidi


Siku ya leo ninakuletea tabia Tano muhimu ambazo unapaswa kujenga ili uweze kufanikiwa mara kumi zaidi kwenye maisha.

1. Kujiamini
Kuna watu wengi  wasiojiamini. Unakuta mtu hata anashindwa kutoa hoja yake mbele ya watu kwa sababu ya kutojiamimi. Wewe jiamini.
Unapoongea na watu jiamini. Unapoongea na watu kwenye simu, jiamini. Unapokuwa unatembea njiani, jiamini.

2. Kijituma zaidi
Mafanikio makubwa siyo kitu lelemama. Unapaswa kujenga tabia ya kujituma kwenye kile unachofanya. Jitume kwenye kazi zako na zifanye kwa weredi mkubwa.

3. Kufanya vitu kwa utofauti walau mara moja kwa wiki

Kila mtu anapenda kupata matokeo ya tofauti. Ila huwezi kupata matokeo ya tofauti huku ukiwa unaendelea kufanya mambo yale yale kila siku. Lazima ujenge utaratibu wa kufanya vitu kwa namna ya utofauti, katika namna ambayo Watu wengine hawapo tayari kufanya. Kwa jinsi hiyo sasa ndivyo utakavyoweza kuzidi kusonga mbele na kufanya makubwa zaidi kwenye maisha yako.

4. Kujaribu vitu vipya
Kadiri unavyojaribu vitu vipya ndivyo unakuwa unazidi kujifunza zaidi na hivyo kupata uzoefu kwenye maeneo mbalimbali. Usiogope kujaribu. Hata Kama utajaribu kitu na baadaye ukafeli. Ukweli ni kwamba somo utakalokuwa umetoa hapo ni kubwa zaidi na litakuwa na msaada mkubwa zaidi kwenye maisha yako.

5. Kufanye kujifunza kuwe sehemu ya pili ya maisha yako. Kila mara na kila siku jifunze kitu. Jifunze kwa kusoma vitabu. Jifunze kwa makosa WANAYOFANYA watu.
Jifunze kwa mazuri wanayofanya watu.
Jifunze kwa yale mazuri wanayoongea watu ila wao wenyewe hawayafanyii kazi.

Kuna watu ni wazuri sana kwenye kuongelea vitu Kama fursa, jinsi ambavyo unaweza kutoka kimaisha ila wao wenyewe hawafanyii kazi kile wanachokiongea. Wewe ukiona mtu kaongea kitu kizuri hata kama yeye hakifanyii kazi ila unaona kuwa kitu hicho unaweza kukitumia kwenye maisha yako kitumie au kifanyie kazi kitu hicho.

Ndugu mmoja huwa anapenda sana kuongelea kuhusu  uwekezaji kwenye miti na jinsi ambavyo unaweza kutoboa maisha kupitia uwekezaji huu. Hata hivyo, yeye mwenyewe huwa hachukui hatua ya kuwekeza kwenye miti. Ni mzuri kwenye kupiga hesabu za jinsi gani unavyoweza kutengeneza mamilioni, ila yeye mahesabu hayo hayafanyii kazi.

Jifunze kwa watu wa aina hii ma fanyia kazi yale unayoyaona kutoka kwao.

Nakukumbusha tu. Kuna ofa ya kupata kitabu cha MAAJABU YA KUWEKEZA KWENYE HISA, HATIFUNGANI NA VIPANDE. Unalipia elfu nne tu kwa ajili ya kupata kitabu hiki ila utazawadiwa na vitabu vingine vitatu ambavyo ni:

1. SEKTA 11 ZA KUTENGENEZA MAMILIONI YA FEDHA TANZANIA
2. TOFAUTI 50 KATI YA MATAJIRI NA MASIKINI
3. MAAJABU YA KUWEKA AKIBA

VYOTE hivyo utapewa kwa elfu nne. Na habari mbaya ni kwamba ofa hii inaisha tarehe 15 mwezi huu. Hivyo, changamka ili uweze kupata ofa hii. Lipia sasa kwa Mpesa 0755848391 au Airtel money 0684408755 jina ni GODIUS RWEYONGEZA.

Baada ya kutuma fedha, nitumie ujumbe kwa whatsap 0755848391 ili nikutumie vitabu.

Nakushukuru sana kwa kuweza kufuatilia somo hili mpaka mwisho. Umekuwa nami rafiki yako wa ukweli Godius Rweyongeza

Hakikisha Umesubscribe kwenye Channel yangu ya youtube kwa KUBONYEZA HAPA

Jiunge na mfumo wa kupokea makala maalumu kwa njia ya barua pepe kwa KUBONYEZA HAPA

Jipatie nakala za vitabu vyangu vya kiswahili kwa KUBONYEZA HAPA

Kama ungependa kujifunza kuhusu uandishi wa vitabu kutoka kwangu wasiliana nami kwa 0755848391

Kupata nakala ngumu ya kitabu cha KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI na kitabu cha JINSI YA KUFIKIA NDOTO ZAKO basi tuma ujumbe au piga kwa 0755848391

Kujifunza namna ya kutengeneza fedha kupitia blogu tuwasiliane kwa 0755848391

Kunialika kwa ajili ya kutoa mafunzo au semina kwenye kikundi chako, taasisi, kongamano n.k. wasiliana nami kwa email: songambele.smb@gmail.com au simu 0755848391


One response to “Tabia Tano Unazopaswa Kujijengea Ili Ufanikiwe Mara Kumi Zaidi”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X