Ugunduzi mkubwa kuwahi kufanyika hapa duniani


  

Zimewahi kufanyika gunduzi nyingi sana hapa duniani. Na hata leo hii bado kuna gunduzi nyingi zinaendelea kufanyika. Hata hivyo, kuna ugunduzi mkubwa ambao ndiyo ugunduzi nambari moja kukiko ugunduzi mwingine unaoufahamu wewe. Na ugunduzi huu ni kuwa mtu anaweza kubadili maisha yake akibadili mtazamo wake.

Hii ni kauli ya James Allen ambayo aliitoa kwa kusema; ugunduzi mkubwa katika kizazi changu ni kuwa mtu anaweza kubadili maisha yake endapo akibadili mtazamo wake.

Looo! Ebu fikiria hili. Kumbe wewe unaweza kuwa na maisha bora endapo wewe utaamua kubadili mtazamo wako. Mtazamo wako wa sasa, ndio unaweza kutuonesha kesho yako ikoje. Ukibadili mtazamo wako unaweza kubadili maisha yako pia.

Uko jinsi ulivyo kutokana na jinsi unavyofikiri. Anza leo kubadili mtazamo wako.
Kuwa na mtazamo wa uwezekano. Fikiri kuwa inawezekana wewe kufikia mafanikio makubwa. Fikiri kuwa inawezekana wewe kwenda unapotaka kwenda.
Kuwa na ndoto kubwa na kuwa na mtazamo kuwa inawezekana wewe kuzifikia hizo ndoto zako.

Moja kati ya kitabu kitakachokufanya Sana kwenye kubadili mtazamo wako nabkusiendelea NDOTO ZAKO kubwa ni kitabu cha JINSI YA KUFIKIA NDOTO ZAKO pamoja na KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI.

Umekuwa nami,

GODIUS RWEYONGEZA

Hakikisha Umesubscribe kwenye Channel yangu ya youtube kwa KUBONYEZA HAPA

Jiunge na mfumo wa kupokea makala maalumu kwa njia ya barua pepe kwa KUBONYEZA HAPA

Jipatie nakala za vitabu vyangu vya kiswahili kwa KUBONYEZA HAPA

Kama ungependa kujifunza kuhusu uandishi kutoka kwangu wasiliana nami kwa 0755848391

kila la kheri

, ,

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X