Ok vizuri.
Inawezekana kuanzisha biashara ukiwa umeajiriwa.
Kwanza, unapaswa kujua aina ya biashara ambayo ungepsnda kuanzisha.
Pili, unapaswa kujua na ratiba yako ya kazi. Hii itakusaidia kupangilia muda wa mwajiriwa wako na muda wa kufanya biashara yako.
Tatu, unapaswa kuhakikisha kwamba unafanya kazi zako kuajiriwa kwa nguvu na weredi mkubwa. Usifanye kazi ya ajira hovyo, muda wa kazi ya ajira utumie kuifanya.
Nne, fahamu unapoamua kuanzisha biashara ukiwa umeajiriwa unapaswa kujitoa sana. Inahitaji ujitoe na upate muda wa kufanya kazi yako ya ajira na biashara yako. Nyakati nyingine utakuwa umechoka ila UTAPASWA kujilazimiaha. Utajikosesha raha na starehe nyingi ulizokuwa unapata. Hayo yote kwa ajili ya biashara yako.
Muhimu sana katika kuifanya biashara yako isijulikane ni kutoanzisha biashara ambayo utakuwa unaifanyia ofisini kwa bosi wako; kama kuuza vitu kwa wafanyakazi wenzako. Ikiwezekana, hata wafanyakazi wenzako wasijue kuwa umeanzisha biashara maana wanaweza kuwa watu wa kwanza kukuchongea. Unaweza kuanzisha biashara mbali kidogo na ajira yako ilipo, ila unapoweza kufika kwa haraka.
Kila la kheri
One response to “USHAURI: Jinsi Ya Kuanzisha Biashara Ukiwa Umeajiriwa Bila Bosi Wako Kujua”
[…] Na uhuru huu unaweza kuupata zaidi kwenye biashara yako utakayoanzisha. […]