Kwa Nini Mpaka Sasa hivi huanzishi biashara yako?


Ngoja kwanza! Si ulisema mwaka 2020 kwamba utaanzisha biashara? Ilikuwaje? Nakumbuka mwaka 2021 ulisema ndio mwaka wako wa kufanya makubwa! Uliishia wapi? Mbona hilo wazo lako la kuanzisha biashara unarudia kulisema kila mwaka huku ukiwa huchukui hatua?

Siku ya leo nataka nikudadavulie vitu vinavyokuzuia wewe kuanzisha biashara yako mwaka hadi mwaka na hatua unazoweza kuchukua.

MOJA: MSHAHARA

Mshahara unaondelea kuupokea kila mwezi unaona kwamba utaendelea kuwepo mwaka hadi mwaka, hivyo huoni haja ya kuanzisha biashara au chanzo kingine cha kipato.

Ninachotaka ufahamu ni kwamba, mambo yanabadilika kila siku. Ajira yako ya leo, inaweza isiwepo kesho. Hivyo basi ni muhimu sana uanzishe biashara.
Kuna sababu nyingi kwa nini unapaswa kuanzisha biashara, mojawapo ikiwa ni pamoja ni kujitengenezea uhuru wako mwenyewe.

Na uhuru huu unaweza kuupata zaidi kwenye biashara yako utakayoanzisha.

SOMA ZAIDI: USHAURI: Jinsi ya kuanzisha Biashara Ukiwa Umeajiriwa Bila Bosi Wako Kujua

PILI: UOGA

Najua, umekuwa unaogopa kwa muda sasa, hivi nikianzisha biashara, itakuwaje?

Ninachotaka ufahamu ni kuwa watu ambao wewe unawaogopa, wao pia kuna vitu vyao wanaogopa na pengine wanakuogopa wewe. Usikwamishe ndoto zako kwa sababu ya watu waliokuzunguka au hofu ya watu.

TATU: HUTAKI KULIPA GHARAMA

Biashara siyo kitu cha mchezo mchezo. Ukianzisha biashara kuna vitu ulikuwa unafanya, utapaswa kuachana navyo na kuna vitu ulikuwa hufanyi utapaswa kufanya.
Ulikuwa husomi wala kujifunza utapaswa kuanza kusoma na kujifunza.
Ulikuwa hutaki kuongea na watu, utapaswa kuwapigia wateja na kuongea nao vizuri ili waweze kuja kwako kununua zaidi.

Kuwa tayari kulipa gharama maana mtaka cha uvunguni sharti ainame. Ukitaka kula vinono, sharti ukubali kulipa gharama kwanza.

NNE: UNASUBIRI MPAKA UWE NA MTAJI WA KUTOSHA.

Yaani, nadhani hiki ndicho kilipaswa kuwa kigezo nambari kwako.

Kila siku na kila mwaka unaendelea kusema kwamba unazichanga, sijui utaendelea kuzichanga mpaka lini.

Unasubiri mpaka uwe na mtaji wa milioni 200 ndio uanzishe biashara si ndio?

Kwa nini usianze sasa hivi kwa kutumia huo mtaji ulio nao. Una mitaji mingi sana imekuzunguka, unaijua?

Ebu rusha elfu mbili tu leo, nikurushie ebook inayozungumzia MITAJI 8 ILIYOKUZUNGUKA NA JINSI YA KUITUMIA.

Changamka sasa rusha kwa 0684 408 755 jina ni GODIUS RWEYONGEZA. Hii ni bei ya ofa

TANO: UNAOGOPA KUSHINDWA

Najua kuwa ukianzisha biashara, lazima tu watu wengi watajua kuwa umeanzisha biashara.

Na hasa watu wako wa karibu. Ndugu, jamaa na marafiki. Sasa unachoogopa ni endapo biashara ikifeli itakuwaje?

Si unajua huwa hatupendi kuonekana tumeshindwa, badala yake tunapenda kuonekana tunashinda kwa kila kitu?

Ninachotaka nikwambie ni kuwa japo biashara haina guarantee kuwa itafanikiwa kwa asilimia 💯. Ila utajifunza sana kwenye kuanzisha na kukuza biashara kuliko unavyoweza kujifunza sehemu yoyote.

Hata biashara ikifeli, bado somo utakaloondoka nalo hapo ni kubwa kuliko unavyoweza kufikiri.

Hata hivyo, kufeli ni sehemu ya maisha.  Nyuma ya ushindi wowote ule Kuna kushindwa, kushindwa, kushindwa. Usiogope SONGAMBELE

Tulipokuwa wadogo, tulijaribu vitu vingi sana na kufeli kwenye vitu vingi pia. mfano kwenye kutembea tu, mtoto anajaribu mara nyingi sana kutembea huku akianguka na kuinuka.

Hakuna mtu ambaye huwa anamcheka mtoto kwa sababu eti anaanguka. ila sote huwa tunajua kwamba kadiri anavyoanguka ndivyo anakuwa anakaribia kwenye ushindi. kwa hiyo kuanguka kwako, ni sehemu tu ya kuelekea kwenye ushindi.

Kupata kitabu hiki wasiliana na 0755848391 sasa

SITA: UMEZUNGUKWA NA WATU WENGI AMBAO HAWANA MTAZAMO WA KIBIASHARA

Ukizungukwa na watu ambao hawana mtazamo wa kibiashara, hata kama unapenda biashara kiasi gani, usitegemee kuanzisha biashara.

Watakukatisha tamaa na wataongea vitu ambavyo mwisho wa siku vitakufanya ushindwe kwenda hatua ya ziada na kuanzisha biashara.

Kama unataka kuanzisha biashara, ungana na timu ya watu sahihi.

SABA: KUNA WATU UNAWATEGEMEA

Una wazazi, mjomba au ndugu unayemtegemea akupe kila kitu. Hivyo, unadhani kila kitu kitaendelea kuwa hivyo maisha yako yote.

Unadhani, ataendelea kukulipia bili ya umeme na wewe unachaji simu yako tu ili uchati.

Unadhani ataendelea kukupa chumba cha kulala maisha yako yote, milele na milele, Amina.

Funguka. Itumie hiyo kama fursa, kwa kuwa una mtu ambaye anaweza kukusaidia basi tayari una sehemu ya kusimamia.

Kuna watu wanakutamani ila wewe hujui tu. Wengi wanatamani wangekuwa kama wewe, shauri yako!

NANE: UNADHANI UMEZEEKA SANA AU BADO KIJANA SANA

Kitu kingine unafikiri labda umri wako bado sana kiasi kwamba huwezi kuanzisha biashara, na pengine labda unadhani kuwa umri wako umeenda sana.

Nakumbuka niliwahi kuongea na kijana wa miaka 35 tu, akawa ananiambia umri wake umeshaenda, hawezi tena kufanikiwa.

Kama wewe unadhani umri wako bado sana unakosea . Unapaswa kuanza ukiwa bado na nguvu kama kijana.

Vipi ukiambiwa Warren Buffet alianza kuwekeza akiwa na umri wa miaka 11? Na bado leo hii anasema kwamba anaona alichelewa kuanza. Siyo kwamba muda wako bado, Anza sasa hivi.

Kama unadhani umri wako umepita. Unakosea pia. Vipi ukiambiwa aliyeanzisha KFC aliianzisha baada ya kustaafu?

Siyo kwamba muda umeenda; muda mzuri wa kupanda mti ulikuwa miaka 20 iliyopita muda mzuri zaidi wa kupanda miti ni sasa.

Pichani ni Cornel Sanders aliyeanzisha mgahawa wa KFC akiwa na umri wa miaka 65

TISA: MAJUKUMU YA SASA YANAKUBANA

Unasema kwamba majukumu ya sasa yanakubanabsana kiasi huwezi kuanzisha biashara. Na ni ukweli kuwa biashara inahitaji muda pia.

Wewe kwa upande wako unaweza kuona upo sawa, ila mimi naona tatizo hapo. Kwa nini? Kwa sababu japo biashara mwanzoni itakuhitaji sana, ila mwisho wa siku lengo la biashara ni kutupa uhuru.

Maana yake kama kweli uko siriazi kufanya biashara inapaswa baada ya muda upate uhuru, biashara ijiendeshe yenyewe, wewe upate uhuru na muda wa kufanya mengine.

Najua kwako hili ni gumu kumeza kwa sababu hujawahi kuona washikaji zako wakifanya hivyo. Ila huoni walau hata kwa bosi wako?

Sasa hata kama upo bize hakikisha unaanzisha biashara, anza na biashara hata za mtandaoni, soma ebook ya MITAJI 8 ILIYOKUZUNGUKA NA JINSI YA KUITUMIA

Kama unaona upo bize na huwezi kuanza biashara. Nashauri pia ujiunge na programu yetu ya mafunzo zaidi ambapo utapata nafasi ya kuwa karibu na mimi kwa mwaka mzima. Nitakusaidia na kukushika mkono mpaka uanzishe na kuendesha biashara kwa muda ziada. BONYEZA HAPA kujiunga.

kupata mafunzo zaidi BONYEZA HAPA

KUMI: HUPATI RUHUSA KUTOKA KWENU

Pengine labda ndugu zako wa karibu hawataki kabisa kusikia habari za wewe kuanzisha biashara. Kama mazingira yako ndiyo haya

Basi utapaswa kukaa nao na kuongea nao kwa kina kuhusiana na biashara. Walekeze kwa nini unataka kuanzisha biashara. Waeleze ndoto zako kubwa ulizonazo kuhusu biashara.

Ongea nao, bwana bro au sista, iko hivi, mimi siku zote hizi unaniona hapa, nina ndoto kubwa za kuanzisha biashara, najua kweli kuwa biashara siyo kitu ambacho unapenda ila mimi binafsi ni kitu ambacho naona kwamba napenda na ninaona naweza kusaidia watu na familia kupitia hapo…

Kama kuna uoga au hofu ambayo wanayo iongelee kwenye maongezi yako na namna ambavyo utaweza kufanya biashara yako bila ya kuwasababishia hiyo hofu.

Ikiendelea kushindikana pengine unaweza kutakiwa kutoka nyumbani, kama upo nyumbani kwenu lakini.

KUMI NA MOJA: HUNA MTAJI FEDHA

Pengine labda kinachokukwamisha wewe kuanzisha biashara yako ni kukosa mtaji fedha.

Kama shida yako ni mtaji fedha, basi utapaswa kuanza utaratibu wa kuweka akiba. Weka akiba kutokana na kipato chako cha sasa.

Kama huna kazi kabisa, basi kuanzia leo unapaswa kufunguka. Tafuta kazi au kitu chochote kile cha kuuza kuanzia leo. Angali akwenye jamii yako ni kitu gani ambacho unaweza kuanza kuuza. Lakini pia unapaswa kujua ni mtaji kiasi gani ambao unauhitaji.

Nashauri sana, sana uhakikishe umesoma ebook ya MITAJI 8 ILIYOKUZUNGUKA NA JINSI YA KUITUMIA itakusaidia hata kama huna mtaji upate sehemu ya kuanzia. Kupata ebook hii Tuma elfu 5 sasa hivi kwenda 0684 408 755 jina ni GODIUS RWEYONGEZA ili kupata ebook hii

umekuwa nami GODIUS RWEYONGEZA

0755848391

[block rendering halted]


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X