Jana niliandika makala yenye vitu 9 ambavyo hupaswi kuchoka kufanya. Mmoja wa wasomaji wa amkala hiyo alinibu kwa kusema hivi
Nami nikawa nimemjibu pia kwa ujumbe huu hapa chini
Ni kweli unapokuwa unapambania ndoto kubwa watu watakuona mtu wa ajabu sana.
Watakuona kichaa, utaambiwa umechnganyikiwa na mambo mengine mengi.
Na hili linawatokea watu wote wenye ndoto kubwa.
Kuwa na ndoto kubwa ni sawa na kucheza muziki ukiwa na earphone masikioni. Wengine hawausikii huo muziki ila kwako unakuwa umenoga. Wanaokuona unacheza watakuona kichaa tu, kwa sababu muziki unaocheza kwao hauna maana.
Ndio maana Steve Jobs anasema kwamba, watu wenye kichaa cha kutosha kiasi cha kufikiri wanaweza kuibadili ndio ambao huibadili. Kuna wakati unapokuwa na ndoto kubwa, unapaswa kukubali tu kuonekana kichaa.
Nashauri sana usome kitabu changu cha JINSI YA KUFIKIA NDOTO ZAKO. Kina mengi ya kueleza kuhusu ndoto.
One response to “Kinachotokea Unapokuwa Na Ndoto Kubwa”
[…] HATUA YA KWANZA: Anza kwa kutengeneza ndoto kubwa ambayo ungependa kuifikia hapo baadaye […]