Usiende Chuo Kusomea Uandishi Wa Vitabu; Badala Yake Fanya Hivi


Siku kadhaa zilizopita nilipokea simu ya mtu aliyekuwa anataka nimwambie chuo kizuri kinachonoa Waandishi Wa Vitabu.

Nilimjibu vizuri tu, ila hakuridhika na majibu yangu kwa maana yalipingana na kile alichokuwa anaamini kwa asilimia 100. Yeye alitaka kwenda chuo, asomee uandishi na apate cheti. Cheti cha nini sasa? Najua, jamii yetu imezoea kwamba ukiwa na cheti basi hapo unakuwa umefaulu na unaenda ku-win maisha.

 Baada ya siku kama tatu hivi nilipokea ujumbe huu hapa chini kutoka kwa mtu mwingine.

Nadhani huyu alinifafuta na tuliongea kwa kina kuhusu hili.

. Simshauri kwa Sasa apoteze fedha zake kwenda chuo kwenda kusomea UANDISHI. 

Kuna kozi nyingi ambazo anaweza kusoma mtandaoni tena akiwa nyumbani, na akiwa anaendelea na shughuli zake za sasa. 

Ni sawa kuingia darasani, ila kwa sasa asifanye hivyo.

Afanye yafuatayo.

1. Aanze kuandika

2. Amtafute โ€˜mentor’ wa kumsaidia.

3. Aoneshe kazi zake anazoandika aidha mtandaoni au kwa watu wake wa karibu.

4. Apokee mrejesho wa kazi zake na aufanyie kazi.

5. Atumie mrejesho anaoupata na mafunzo anayopata kuboresha uandishi wake zaidi.

Kuna mengi ila kwa sasa hayo yanatosha.

Najua ushauri huu ataupuuza. Ila walau ninachofahamu kwa sasa atapoteza muda wake kwenda kujifunza uandishi kwa ajili tu ta kupata CHETI ambacho mwisho wa siku hakitamsaidia chochote.

Ngoja nieleze kitu zaidi hapa. Waandishi hawafahamiki Kama waandishi kwa sababu wanaVYETI. Waandishi ni waandishi kwa sababu wanaandika.

Mimi siyo mwandishi kwa sababu Nina cheti; HAPANA. Sijawahi hata siku moja kuona mtu ananiuliza cheti changu cha kuwa mwandishi kipo wapi๐Ÿ˜Š๐Ÿ˜Š. 

Kitu kingine ni kwa kuwa nguvu yake kubw ipo kwenye cheti kuliko kufahamu zaidi mchakato wa kuandika na kubobea kwenye uandishi, ataweka NGUVU kwenye kupata CHETI na atapata, ila hatakuwa mwandishi mzuri. Na hicho ndiyo kuantokea pia kwenye mfumo wa elimu. Wahitimu wengi wanahitimu na vyeti vizuri ila ujuzi SIFURI kutokana na ukweli kuwa waliweka nguvu kubwa kwenye VYETI kuliko kupata ujuzi.

๐Ÿ–Š๏ธ๐Ÿ–Š๏ธ๐Ÿ–Š๏ธ๐Ÿ–Š๏ธ๐Ÿ–Š๏ธ๐Ÿ–Š๏ธ

Nashauri asome kitabu changu cha JINSI YA KUWA MWANDISHI MBOBEVU NDANI YA SIKU 30 ambacho kimeeleza kila kitu anachohitaji kujua kuhusu uandishi๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡

Au awasiliane nami kwa 0755848391


One response to “Usiende Chuo Kusomea Uandishi Wa Vitabu; Badala Yake Fanya Hivi”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X