Kuna kitu kimoja ambacho leo ninataka ukifahamu kuhusu utajiri na umasikini.
Kitu hiki ni kwamba maskini wapo siku zote, ila kazana usiwe mmoja wao.
Kwenye kila jamii unakuta kuna watu wachache wenye utajiri mkubwa ukilinganisha na wengine wengi.
Sasa lengo lako linapaswa kuwa ni wewe kuingia kwenye wale wachache ambao wana utajiri mkubwa.
Utajiri ni kitu ambacho unaweza kukitengeneza kwa kufuata kanuni chache tu kama
kuweka akiba
Kutunza akiba hiyo na hatimaye kuiwekeza
Kuifanya fedha ikufanyie kazi na vitu vingine vya aina hiyo
Kwa hiyo kitu cha kwanza kabisa ambacho ninataka ufahamu ni kwamba; masikini wapo siku zote. Ila chagua kutokuwa mmoja wao.
Pili, upende utajiri na ipende fedha, huwezi kupata wala kuishi na kitu ambacho hukipendi. Huwezi kupata fedha wala kuishi na utajiri kama huupendi utajiri. Upende utajiri nao utakupenda. Zipende fedha nazo zitakupenda.
Wewe si unaona hata kwa watu. Mtu unapoonesha dalili za kumpenda ndio na yeye anakupenda. Ukionesha kumchukia na mwenyewe anakuchukia pia.
Ndio maana utasikia mtu anasema, Mimi na mtu fulani huwa hatuendani. Maana yake huwa hawapatani, huwa haziivi. Hawawezi kukaa pamoja.
Sasa kama na wewe huzipendi fedha maana yake wewe na fedha hamwendani, hampatani, haziivi na hivyo huwezi kukaa pamoja na fedha (ndio maana ukizipata unazifuja kwa kuzitumia hovyo).
Kuanzia leo, anza kuzipenda fedha. Zipende zikupende.
Nashauri usome vitabu vyangu vya MAISHA NI FURSA ZITUMIE ZIKUBEBE pamoja na kitabu cha MAAJABU YA KUWEKA AKIBA
Rusha elfu 20 leo nikutumie ebooks zake leo kwa WhatsApp au barua pepe.
Rusha fedha kwa 0684408755 jina ni GODIUS RWEYONGEZA
SOMA ZAIDI:
- Vitu Vitano Ambavyo Havitabadilika Miaka Kumi Ijayo
- Ni muda Upi Sahihi Kuajiri Wafanyakazi kwenye Biashara?
- Sababu 5 Kwa Nini Haupaswi Kuomba Fedha Kwa Wazazi: Jifunze Kujitegemea na Kuwekeza Kwa Mafanikio
Umekuwa nami,
GODIUS RWEYONGEZA
Hakikisha Umesubscribe kwenye Channel yangu ya youtube kwa KUBONYEZA HAPA
Jiunge na mfumo wa kupokea makala maalumu kwa njia ya barua pepe kwa KUBONYEZA HAPA
Jipatie nakala za vitabu vyangu vya kiswahili kwa KUBONYEZA HAPA
Kama ungependa kujifunza kuhusu uandishi kutoka kwangu wasiliana nami kwa 0755848391
kila la kheri