Lengo Lako Kuu La Mwaka 2022 Ni Lipi? Au Ndio Unamwachia Mungu🤔?


Jana nilienda kumtembelea mwalimu wangu wa shule ya msingi ambaye kwa sasa ni mstaafu. Kama ilivyo kawaida ya watanzania wengi, nilipofika alifungulia runinga ili tuburudike kwa kuangalia manjonjo ya kimambele.

Alifungulia channel ya Clouds na nilipoangalia tu kwenye kioo cha runinga nilikutana na swali lililosema,  *Lengo lako kuu la mwaka 2022 Ni lipi? Au ndio unamwachia Mungu🤔?*

Sikutanii, swali hili lilivuta sana umakini wangu. Kwa miaka kadhaa ambayo nimekuwa nikiongea na vijana na watu mbalimbali kuhusu maisha, wengi wamekuwa wakiishia kuniambia hawana malengo badala yake wanamwachia Mungu maana yeye ndiye kila kitu/ mweza yote/ alpha na omega.

Hawajui wanataka nini badala yake wanamwachia Mungu.
Hawana mipango ya kesho kwa kusema kwamba huwezi kupanga, mambo yajayo kwa kuwa Mungu tu ndiye anajua. Hawajifunzi hata kwa serikali inayoweka bajeti kila mwaka na  yenye mipango ya kufanyia kazi kwa mwaka mzima unaofuata. Yaani unakuta kamtu hakana malengo, kanisani hakaendi, dhambi kanafanya kila siku halafu ukikauliza lengo lake kanakwambia namwachia Mungu.???

Sasa kabla sijaendelea mbele naomba kukuuliza wewe [WEKA JINA LAKO HAPA], Lengo lako kuu la mwaka 2022 Ni lipi? Au ndio unamwachia Mungu🤔?

USIMBEBESHE MUNGU MSALABA USIO WAKE.

Ndio Mungu ndio kila kitu, lakini amekuumba wewe na mauwezo makubwa sana na bado amekupa UHURU WA KUCHAGUA mazuri na mabaya. Hivyo, jukumu la kuchagua aina ya maisha unayotaka ni la kwako.

Mungu hawezi kukuchagulia wewe kuwa masikini wala tajiri, huo ni uchaguzi unaouchagua mwenyewe kupitia maamuzi unayofanya na vitendo vyako vya kila siku. Na hata mamuzi ya mwaka 2022 iweje yapo mikononi mwako. USIMBEBESHE MUNGU MSALABA USIO WAKE.

Kwenye Biblia Mungu aliwapa uhuru wa kuchagua watoto mapacha (Esau na Yakobo). Mmoja alichagua kuwa mwindaji (mtu aliyekuwa anafanya kazi za nguvu) na mwingine alichagua kukaa nyumbani (alikuwa anafanya kazi kwa akili).

Sasa na wewe usipochagua wapi unataka kwenda, wapi unataka kufika na aina ya mtu unayetaka kuwa, utakuwa unamwangusha Mungu aliyekupa uwezo wa kipekee na shetani atakuzomea wewe!

Na hata Mungu akitaka kushusha baraka zake juu yako, atashindwa azishushie wapi kwa sababu hujaegenea popote. Wewe kwako maisha ni bora liende. Ukisukumwa unasukumika, wakienda unaenda, wakirudi unarudi, upepo wa kaskazini ukivuma unakupeperusha, wa kusini nao unakupeperusha….wewe ni bendera gazeti, mlingoti tope!

MAISHA YAKO NI WAJIBU WAKO
Maisha yako ni wajibu wako, ukishinda ni juu yako, na ukishindwa ni juu yako.

Ndiyo maana wewe unapaswa KUWEKA mipango ya wapi unataka kwenda na wapi unataka kufika. Na hapo ndipo sasa Mungu atatokea KUBARIKI KAZI ZA MIKONO YAKO.

Watu wengi wanatumia kigezo cha Mungu kama kigezo cha wao kutofanya kazi. Ndio maana wengine wanasema aliyekupa wewe ndio kaninyima mimi. Wakati wanasema hivyo Mungu anawaambia kasome Mithali 6:6-11.
Lakini pia Mungu anawasisitizia kuwa hana upendeleo bali anaibariki mikono ya mtu yeyote anayejishughulisha.

LENGO LAKO KUU LA MWAKA

Ili mwaka wako uweze kwenda vizuri, unapaswa kuwa na malengo ambayo utayafanyia kazi ndani ya mwaka huu.

Kuwa na lengo kuu moja ambalo utalifanyia kazi, kiasi kwamba mpaka mwaka huu unafika mwishoni uweze kusema kwamba kweli mwaka huu nimeweza kufanya kitu.
Kitu cha kufanya leo.
Weka lengo lako kuu la mwaka huu.
Kisha baada ya hapo andika malengo yako mengine. Hivyo, unaweza kuwa na  zaidi ya lengo moja ila lengo lako kuu la mwaka 2022 liwe moja.

Ukiwa na lengo moja kuu inakuwa rahisi kwako kuwekeza nguvu zako kwenye hilo lengo. Ukiwa na lengo kuu utakuwa tena siyo bendera hufuata upepo.

Kazi yako ya kufanya leo, andika lengo lako kuu la mwaka 2022?

Unaweza kunishirikisha lengo lako kupitia simu/WhatsApp +255755848391

Naomba nimalizie kwa kukuuliza, “Lengo lako kuu la mwaka 2022 Ni lipi? Au ndio Unamwachia Mungu🤔?”

NAKUKUMBUSHA TU!

Unaweza kupata nakala yoyote ya kitabu changu kwa elfu 3 tu. Chagua nakala unayopenda hapa (BONYEZA HAPA KUONA VITABU VYANGU)
https://www.getvalue.co/home/seller_collection/393

Kisha tuma elfu 3 ili niweze kukutumia kitabu ulicholipia.

Ukihitaji kupata vitabu vyangu vyooote kwa pamoja. Utalipia elfu 50 tu. Vipo vitabu 17.
Lipia kwa 0755848391 jina ni GODIUS RWEYONGEZA.

MWISHO WA OFA HII NI TAREHE 10  JANUARI 2022
Karibu.

GODIUS RWEYONGEZA
+255755848391
Bukoba-Tanzania
www.songambeleblog.blogspot.com


4 responses to “Lengo Lako Kuu La Mwaka 2022 Ni Lipi? Au Ndio Unamwachia Mungu🤔?”

  1. Asante sana, Kaka.

    You are great because you are doing great things.

    Continue to remind people whom they are and Almighty God will continue to shower blessings upon you.

    Barikiwa Sana Kaka.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X