Leo ndiyo Siku Ambayo Watu Wengi Husahau Malengo Yao Ya Mwaka Na Kuanza Kuishi Kwa Mazoea


 

Leo ni tarehe 19 jnuari 2022.  Ukiangalia tangu tuuanze mwaka huu, hata hatuna siku nyingi. Ila cha kushangaza ni kwamba kuna watu ambao tayari wameshasau malengo yao.

Zimefanyika tafiti na imethibitishwa  kuwa tarehe 19 ya kila mwaka mpya, ni tarehe ambayo watu wengi huwa wanasahau malengo yao na hivyo kuendelea kuishi kimazoea.

Swali langu la kwanza kwako leo bado unayakumbuka malengo yako uliyoweka mwanzoni mwa mwaka huu? Kama huyakumbuki, basi jua wazi kuwa Kuna sehemu kuna tatizo na hizi hapa ni mbinu za kukusaidia siyo tu kuyambuka malengo yako bali kuyafikia.

SOMA ZAIDI: Lengo Lako Kuu La Mwaka 2022 Ni Lipi? Au Ndio Unamwachia Mungu🤔?

Moja, jikumbushe malengo yako kila siku. Tena ujikumbushe kwa kuyaandika chini. Fanya hivyo, asubuhi na jioni kila siku kwa siku zilizobaki mpaka ufikie lengo lako. Haufanyi hivyo tu ilimradi umefanya, badala yake unafanya hivyo kwa sababu unaukumbusha ubongo na akili yako kwamba inapaswa kuwekeza nguvu kwenye kutimiza malengo na siyo kingine.

Pili, kila siku andika chini mbinu au njia za kukusaidia wewe kufikia lengo lako. Jiulize kila siku, Ni kitu gani kimoja ambacho naweza kufanya Leo kikanisaidia kufikia lengo langu. Ukikipata, kifanyie kazi.

Tatu, ungana na timu ya watu sahihi ambayo inaweza kukusaidia wewe kufikia lengo lako.

Nne, usikimbizane na malengo mengi kwa wakati mmoja. Fanyia kazi lengo moja kwa wakati

Tano, ipangilie kila siku inayokuja kwako na itumie vizuri kuhakikisha umefikia lengo lako.

Sita, kila siku, fanya kitu kuelekea malengo yako.

Kwa leo ni hayo tu. Nakutakia kila la kheri.


6 responses to “Leo ndiyo Siku Ambayo Watu Wengi Husahau Malengo Yao Ya Mwaka Na Kuanza Kuishi Kwa Mazoea”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X