Hatua muhimu ambazo wazo lako litapitia kabla ya kuonekana kwenye uhalisia


Niseme, nisiseme! Wazo linazaliwa, linakua na muda mwingine kuzeeka mpaka kufa!

Kwa hiyo wazo ni kama mtoto, linabebwa kama mimba. Hiki ni kipindi ambacho linakuwa kichwani mwa mtu. Linazaliwa hapa ni pale ambapo linaanza kufanyiwa kazi, linakua, hapa ni pale linapozidi kufanyiwa kazi na kuzidi kuleta matokeo kwa aliyekuwa na wazo na jamii, wazo linazeeka na hata kufa (hapa ni pale ambapo linakuwa halijafanyiwa kazi kikamilifu).

Wanaume kama nawaona vile mnavyoguna, eti unajiuliza kwa hiyo na sisi wanaume tunabeba mimba? Naomba nieleweke tu kwamba mimba yenyewe ni ya wazo siyo mimba ya mtoto, hapo vipi.

Mwanamke anapokuwa na mimba ya mtoto kuna vitu anapaswa kufanya ili mimba hiyo isitoke wala kuharibika. Mtoto anapozaliwa anaangaliwa kwa umakini, analelewa, analishwa na kupewa vitu vyote vya muhimu. Endapo vitu hivi vitu vyote vitatolewa bila shida yoyote, unakuwa ni uhakika kwamba LAZIMA TU mtoto atakua. Na ni kweli anakua, lakini endapo vitu fulani havitazingatiwa, basi ndio mtoto ataaza kupata utapiamlo, au magonjwa mengine.

Sasa kitu kikubwa cha wewe kufanya ni kwamba, ukiwa na wazo la biashara, hakikisha unakimbizana kulifanyia kazi.

Ukianza kulifanyia kazi ng’ang’ana nalo mpaka likue au ulifanikishe.

Ukishalikuza, hakikisha unakuwa mbunifu ili liendelee kukua zaidi au kuenea maeneo mengine, la sivyo litakufa.

PATA KITABU CHA BURE

Umekuwa nami rafiki yako wa ukweli

Godius Rweyongeza

+255755848391/ Morogoro-Tanzania


One response to “Hatua muhimu ambazo wazo lako litapitia kabla ya kuonekana kwenye uhalisia”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X