Unawezaje Kupata Wazo La Biashara La Kipekee?


Unachohitaji sana wewe, siyo wazo la kipekee ambalo halijawahi kufanyika. Unachihitaji ni kUchagua kitu kimoja na kuhakikisha kwamba unashughulika na hicho.

Angalia jamii yako ina tatizo gani kisha tatua hilo tatizo. Ebu fikiria kuhusu sehemu unapopata huduma mtaani kwako. ebu fikiria juu ya supermarket yoyote mjini kwako. au fikiria kuhusu basi ambalo huwa unatumia kusafiri, hawa jamaa hawa hawakuwa wa kwanza kuingia kwenye soko.

Kitu kikubwa ni kwamba walifanya uamuzi wa kwamba tunaenda kuzalisha bidhaa na kutatua tatizo ambalo linawakumba watu. Basi. Hawakuwa wagunduzi wa hicho kitu, hawakuwa waanzilishi wala wa kwanza kufanya hicho kitu.

Ebu kwa mfano fikiria kampuni inayotengeneza redio. Haikugundua hiyo redio. Na walikuwa wanajua kwamba kuna redio nyingine huko mitaani zinauzwa. Hawakukaa na kuanza kufikiri juu ya wazo gani jipya na la kipekee waje nalo.

Kitu pekee walichokuwa na uhakika nacho ni kwamba, kila mtu anahitaji redio na watu wananunua redio mara zore. Hivyo, ngoja na sisi tutengeneze moja na kuiuza.

Hivyo, huhitaji kuwa wa kwanza kwenye soko. Wanunuaji wanapoenda kununua hawanunui kwa sababu mtu au kampuni ili kuwa ya kwanza kutengeneza bidhaa husika.

Bali wenyewe wananunua kwa sababu,

  • Wana tatizo na
  • Wameona bidhaa ambayo inatatua tatizo lao

Hivyo. Badala ya wewe kuanzakufuta wazo ambalo halijawahi kufanyika hapa duniani, fanya hivi:

  • Angalia tatizo walilonalo watu
  • Tengeneza bidhaa inayoweza kutatua hilo tatizo lao
  • Ilete mbele ya wahusika.

Acha kulisubiria wazo la kipekee. Ukisubiria wazo la aina hii, utakufa ukiwa bado unasubiri.

Kila la kheri

Godius Rweyongeza

0755848391

SOMA ZAIDI


One response to “Unawezaje Kupata Wazo La Biashara La Kipekee?”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X