Nakumbuka nikiwa kidato Cha tano nilitamka kauli ambayo mpaka leo hii imekuwa mwongozo mkubwa kwangu; nilisema kwamba; kwa vyovyote vile kazi yoyote ile nitakayoifanya maishani mwangu nitahakikisha naifanya kwa ubora na watu nitakaokuwa nawahudumia watafurahia.
Kipindi hicho nilikuwa na ndoto za kuja kuwa daktari wa binadamu au mwalimu. Si unajua ukisoma PCB unakuwa na mikogo za kujiita daktari. Muda mwingine mpaka kwenye daftari unaandika jina lako kwa kutanguliza neno Dr.
Siku mkienda maabara na labcoat ndio kabisa unapost mpaka mtandaoni ukisema, Dr. In action hahah.
Baada ya kumaliza kidato cha sita nilianza kusoma vitabu vya mafanikio na kitu kimoja nilichokuja kugundua ni kuwa ninlikuwa nataka kuwa daktari kwa sababu tu ya kuutaka mshahara mkubwa,uliokuwa ukisemwa na watu na nilitaka kuwa mwalimu kwa sababu iliaminika kuwa ni rahisi kupata ajira kama mwalimu (mshahara siyo mkubwa ila uhakika wa ajira ni mkubwa). Sasa hapa nikagundua kuwa ukiwa mtu makini unaweza kutengeneza mshahara mkubwa hata kama siyo daktari, nikaamua sasa kwa dhati kuwa ninaenda kuwa tajiri maishani mwangu. Na hata baada ya kuingia chuo na kuhitimu niliweka mkakati ambao ndio nimeufanyia kazi naamini utaweza kukusaidia wewe. Kwa hiyo Kama upo chuoni na una mpango wa kujiariri; fanya hivi
1. Acha cheti chako kiozee chuoni
Kwa mfumo wa elimu ya Tanzania, watu wengi wanathamini sana vyeti kiasi kwamba mtu akishahitimu anaanza kuzunguka huku na kule na kule cheti. Elimu yenyewe hii kikawaida imekuandaa kuhakikisha kwamba mara tu baada ya kumaliza chuo unaanza kutafuta ajira mtaani, ikitokea tu hujaajiriwa basi utaanza kulalamika, utapata msongo na hata unaweza kujiua.
Sasa, ninachotaka nikwambie wewe unayetaka kujiajiri ni kwamba soma kwa bidii, faulu ila mara tu baada ya chuo, sahau kuhusu cheti chako. Tena kiache hicho cheti chako kiozee chuoni. Wewe nenda mtaani, utafute kitu ambacho utaanza kufanya na upambane na hicho. nasema hivyo maksudi kwa sababu endapo utaanza kuhanganaika na cheti mara tu baada ya kuhitimu, utajikuta kwamba unajiingiza kwenye mtego wa kuajriwa na kuanza kukimbilia kuitafuta ajira, hivyo hatua ya kwanza kabisa ya kufanya kama unataka kujiajiri mara tu baada ya kuhitimu chuo ni kuhakikisha kwamba unaachana na cheti chako na kukiacha kiozee hukohuko chuoni.
Cheti kitakulemaza na kukusahaulisha ndoto zako za kujiajiri.
2. Noa kipaji chako
Hakikisha kwamba unanoa kipaji chako na kukiendeleza kwa umakini wa hali ya juu. Tatizo la watu wengi ni kwamba wanafikiri kuwa kipaji hakifai na wala hakilipi hapa bongo, ila sasa tatizo watu wanaokwambia kuwa kipaji hakilipi hapa bongo wenyewe hawajawahi hata kunoa wala kutumia kipaji chao maishani mwao. Utakuta mtu anakwambia kwamba kipaji hakikilipi bongo ila yeye hajawahi hata siku moja kutumia kipaji cha kwake. Na hata hajui kipaji chake ni kipi.
Wewe jifunze kwa watu ambao wanatumia vipaji vyao. Kipaji kinalipa asikudanganye vitu. Kinachofanya vipaji vya watu visiwalipe ni kwa sababu wanavifanyia kazi kikawaida, hawavipi thamani wao wenyewe, wanaibiwa na wasimamizi wao na mengineyo mengi. Kama umeamua kwa dhati kwamba unaenda kunoa kipaji chako na kukifanyia kazi bila kurudi nyuma, basi kasome kitabu cha KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI kina mengi ya kukusaidia wewe kuweza kunoa na kunufaika na kipaji chako. Wasiliana na 0755848391 ili kupata nakala yak oleo.
3. Anza kuwashirikisha watu maarifa yako uliyojifunza chuoni
Mpaka sasa hivi kuna vitu vingi ambavyo umejifunza chuoni. Unaweza kuanza kutumia vitu hivyo mara moja kwenye maisha yako kwa kuwasaidia watu wengine. Kuna vitu unavyojua, ila sasa kuna watu wengine ambao haawajui kabisa hivyo vitu na hivyo na wangependa kujua hivyo vitu. Kwa hiyo kujifunza kwako chuoni kuwe tiketi ya kuwasaidia watu. anza kuwasidia watu kwa kuwapa maarifa kulingana na kile kitu ambacho umejifunza. Kuna vitu ambavyo wewe unajua na unaviona vya kawaida, ila wengine wanavihitaji sana hivyo vitu.
4. Fungua blogu
Kutokana na ukweli kuwa una maarifa uliyonayo kutoka na kile ulichojifunza chuoni, na kwa kuwa tumeshakubaliana kuwa utaanza kuwashirikisha watu wengine maarifa kutokana na kile ulichojifunza chuoni, hivyo kifuatacho ni wewe kufungua blogu na kuhakikisha kwamba haya maarifa yako unayaaweka sehemu sahihi mtandaoni. Ukianza kuwashirikisha watu maarifa haya, utajikuta kwamba
- Wewe mwenyewe unaongeza maarifa zaidi kwenye vile vitu ulivyokuwa unajua
- Unaanza kujenga timu ya watu wanaokuamini
- Unaanza kupata mrejesho kutoka kwa wasomaji wako
- Unapata kipato cha kuendesha maisha yako n.k.
Kama shida yako kwenye kufungua blogu ni kuandika, unaweza hata kupata kozi ya uandishi. Wasiliana nami kwa 0755848391 ili niweze kukusaidia
5. chagua kitu kimoja ambacho utakufanyia kazi kwa muda mrefu bila kuacha
Chagua kitu kimoja ambacho unaenda kukifanyia kazi kwa muda mrefu bila kuacha, kitu hicho unaweza ukawa umeanza kukifanya bila ya malipo, ila kadiri utakavyokuwa unaenda utakuwa unazidi kukiboresha ili kiweze kukuingizia fedha. Kinaweza kuwa ni kipaji chako ambacho umeshanoa, kinaweza kuwa ni ujuzi wako au elimu yako ambayo unaitumia sasa hivi kwa manufaa kuwasaidia watu wengine. Inaweza kuwa ni biashara ambayo umefungua au kitu kingine. kifanye hiki kitu na usichoke kukifanya mpaka pale kitakapokupa matokeo unayotaka.
Kumbuka tu kuwa unaweza kupata chochote unachotaka kama utaamua na utadhamiria kweli kuhakikisha kwamba unaweka juhudi na kazi zaidi.
PATA KITABU CHA BURE
Umekuwa nami rafiki yako wa ukweli
Godius Rweyongeza
+255755848391/ Morogoro-Tanzania
2 responses to “Kama upo chuoni na una mpango wa kujiariri; fanya hivi. Mwongozo kujiajiri baada ya kumaliza chuo”
[…] Soma Zaidi: Kama upo chuoni na una mpango wa kujiariri; fanya hivi. Mwongozo kujiajiri baada ya kumaliza chuo […]
[…] SOMA ZAIDI: Kama upo chuoni na una mpango wa kujiariri; fanya hivi. Mwongozo kujiajiri baada ya kumaliza chuo […]