KIPAJI NI DHAHABU: Jinsi Ya Kukigundua, Kukinoa Na Kutumia Kipaji Chako Kwa Manufaa


Nakumbuka mwaka 2013 nilikutana na vijana wenzangu ambao walikuwa kwenye mjadala mkali kuhusiana na Messi, Ronaldo na Neymar. Kwenye mjadala huu walikuwa wakijadili kuhusiana na uwezo wa wachezaji hawa, huku wengine wakisema kwamba Messi na Neymar wana kipaji ila Ronaldo akiwa anatumia nguvu.

Nadhani kama wewe ni mpenzi wa soka, mijadala kama hii utakuwa unaifahamu ambavyo huwa inatokea sana. Na jinsi ambavyo huwa inateka umakini wa watu.

Kwenye mijadala kama hii watu huwa wanatoa hoja zao kwa nguvu kuonesha kwamba mchezaji fulani ni mzuri na ana kipaji kuliko mwingine.

Mijadala mingine ya aina hii huwa ni mijadala ya wasanii, ambapo huwa wanalinganishwa wasanii wawili. Umewahi kushiriki mjadala kama huo?

Hivi kwanza wewe mwenyewe unakijua kipaji chako?

Mjadala kama huu ndio ulinifanya nitafakari na kujiuliza hivi mimi mwenyewe nina kipaji gani? Je, hawa wanaozungumzia kipaji cha Messi, Neymar na Ronaldo wanajua vipaji vyao? Ukiwauliza wewe una kipaji gani wanaweza kukujibu? Na tokea hapo nikaianza safari ya kujitafuta ili niweze kujua kipaji changu. Maswali kama kipaji ni nini? Hivi ni kweli kila mtu amezaliwa na kipaji au kuna baadhi ya watu wachache tu ambao wamebarikiwa ndio walizaliwa na kipaji? Kipaji ni kitu cha kuzaliwa nacho au unaweza kukipata ukubwani?

Safari hiyo tu imenifunza mengi ambayo unaenda kukutana nayo kwenye ebook hii hapa ya kipekee.

Kila Mtu Kazaliwa Na Kipaji Ila Hapaswi Kulinganishwa Na Mwingine

Nakummbuka Albert Einstein aliwahi kunukuliwa akisema kwamba kila mtu ni gwiji, ila tatizo ni pale ambapo unamhukumu samaki kwa uwezo wake wa kupaa.

Hapo ndipo nilipogundua kumbe mimi na wewe tuna vipaji, ila sasa kipaji changu hakiwezi kufananishwa wala kulinganishwa na wewe.

Ni wazi kuwa kwa vyovyote vile samaki hawezi kuwa gwiji kwenye somo la kupanda mti, kupaa wala kukimbia. Yeye uwezo wake mkubwa upo kwenye kuogelea na huko lazima atafanya vizuri tu.

Sasa hivyo hivyo kwa kipaji chako. Hakiwezi kulinganishwa na mtu mwingine, unacho wewe na ni kwa ajili yako tu. Hakuna mtu mwingine ambaye anaweza kuwa na kipaji kama cha kwako.

Mgawanyo Wa Kitabu

Kwenye ebook hii hapa nimeeleza kipaji kwa kina hasa ili hata kama ebook hii anaisoma mtoto wa miaka sita aweze kunielewa kuhusiana na kipaji.

Kwenye sura ya kwanza nimeanza kwa kueleza kwamba kipaji ni kitu gani? Ambapo nimeeleza dhana nzima ya kipaji na jinsi kinavyofanya kazi.

Kwenye sura ya pili nimeeleza namna ambavyo unaweza kugundua kipaji chako. Je, unajiuliza ni kwa namna gani ambavyo unaweza kugundua hicho kipaji chako? Basi nenda moja kwa moja kwenye sura ya pili.

Kwenye sura ya tatu nimeonesha mbinu unazoweza kutumia kwenye kunoa na kuendeleza kipaji chako. Hapa utakutana na mbinu za kukusaidia wewe kuweza kupeleka kipaji chako mbali. Na kwenye sura ya nne tutaona kwa nini watu hawathamini vipaji vyao.

Kwenye sura ya tano tutaona mbinu zitakusaidia wewe kutengeneza fedha kwa kutumia kipaji chako.

Tunaishi kwenye ulimwengu wa intaneti. Na hapa tutaingia kwenye sura ya sita ambapo tutaona namna ambavyo unaweza kupeleka kipaji chako kwenye mtandao na kunufaika na inatenti.

Kwenye sura ya saba  tutaona kipaji na elimu. Kwa nini elimu inapewa kipaumbele zaidi kuliko kipaji na je, kuna ulazima wowote wa kuendeleza kipaji chako au ukomae tu na elimu?

Uko tayari kwa ajili ya safari hii ya kipekee? Basi wacha tuianze kama ifuatavyo.

Kupata YALIYOMO YA EBOOK HII BONYEZA HAPA

Mafunzo haya yapo kwenye ebook ambayo unaweza kuipata kwa elfu 5 tu. kuipata ebook hakikisha kwamba lipie elfu 5 kwa  0684 408 755 jina ni GODIUS RWEYONGEZA. ukishalipia utanitaarifu kwa namba hiyohiyo ili niweze kukutumia hiyo ebook.

Kupata YALIYOMO YA EBOOK HII BONYEZA HAPA


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X