Maswali Unayopaswa kuwauliza watu waliofanikiwa


Ukikutana na mtu ambaye amefanikiwa, usitoke bure kwake. Kuwa mdadisi ili uweze kujua ni kitu gani ambacho kimeweza kumpa mafanikio makubwa.

Yafutayo ni maswali ambayo unapaswa kuwauliza watu waliofanikiwa?

1. Imekuwaje umefanikiwa wakati wengine huona siyo rahisi kufanikiwa maishani?

2. Unawezaje kuendesha miradi mikubwa wakati mimi nahangaika na miradi midogo?

3. Nini siri ya mafanikio yako?

4. Ni kitu gani kinakupa hamasa ya kuendelea zaidi?

5. Ulianza anzaje? Je, tangu unaanza maisha ulikuwa hivi?

6. Una mipango gani miaka 10 ijayo?

Usichoke kuuliza maswali. Kila unapokutana na mtu aliyefanikiwa jua kuwa kuna vitu vingi vya kujifunza kutoka kwake. Hivyo basi, kuwa tayari kumuuliza, kitu ambacho kimeweza kumfanya afanikiwe.

Hiki Kitu kitakupa nguvu zaidi wewe na kukufanya usonge mbele zaidi.

Kwanza, utaona kwamba mafanikio siyo kitu cha watu wachache. Na wewe pia unaweza kufanikiwa.

Lakini pia utaona kwamba na wewe ndoto zako zinawezekana. Kama huyu kaweza na mimi nitaweza.

Tatu, utaona kuwa unaweza kuanzia popote ulipo na bado ukatoboa kwenye maisha.

Nne, utapata ule mtazamo halisi wa kimafanikio kutoka kwa mtu aliyefanikiwa.

Mimi nakutakia kila la kheri.

1.KUMBUKA kwamba mafanikio ni haki yako ila tofauti na haki nyingine. Mafanikio hayadaiwi mahakamani. Unapaswa kupambana kuhakikisha kwamba unayapata.

2. Ukitaka kupata matokeo yasiyo ya kawaida, sharti ukubali kufanya vitu ambavyo siyo vya kawaida.

3. Ukitaka kupata matokeo ambayo hujawahi kupata, sharti ukubali kufanya vitu ambavyo hujawahi kufanya.

Kila la kheri.
Godius Rweyongeza
0755848391
Morogoro-Tz


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X