1. Mti wowote ule mkubwa haukuanza ukiwa hivyo, ulikua taratibu mpaka kufikia ulipofikia.
Wewe pia kuwa tayari kuanza kidogo na kuendelea mbele zaidi.
2. Ukitaka kupanda ghorofa kuna njia mbili. Unaweza kupanda ngazi moja baada ya nyingine au unaweza kupanda lift.
Ila fahamu kuwa njia ya kwanza itakuimarisha na kukufanya uwe bora zaidi.
3. Ukianza kupita eneo mara ya kwanza, nyayo zako hazitaonekana. Ila ukiendelea kupita mara kwa mara njia itatengenezeka.
4. Njiti ndogo tu ya kiberiti ina uwezo wa kuwasha moto wa kuunguza msitu mkubwa. Usidharau kitu kwa udogo wake.
5. Safari ndefu ya maili elfu moja, huanza na hatua moja.
6. Ukikata mti kwa shoka, haukatiki kwa shoka la kwanza bali kwa muunganiko wa mashoka mengi unayopiga.
7. Ukitaka kuhamisha mlima, Anza kwa kuondoa jiwe moja.
8. Ukitaka kujenga ghorofa, anza kuweka jiwe moja.
9. Kuna vitu katika maisha havihitaji haraka. Huwezi kupata mtoto ndani ya mwezi mmoja kwa kuwapa mimba wanawake tisa.
10. Katika maisha, hakikisha una ndoto kubwa. Zifanyie kazi kila siku.
One response to “Chukua Mambo Haya 10 Kuhusu Namna Ya Kuanza Kidogo Na Kufikia Pakubwa”
[…] Chukua Mambo Haya 10 Kuhusu Namna Ya Kuanza Kidogo Na Kufikia Pakubwa […]