Ninahitaji Watu 10 Nami Nitawafanya Kuwa Waandishi Wabobevu Ndani Ya Siku 30


Mwishoni mwa mwaka 2019 nilianzisha darasa maalumu la kufundisha uandishi. Ambapo katika darasa hili nilikuwa nafundisha mbinu za kiuandishi kwa mtu ambaye hajawahi kuandika kabisa au ambaye tayari ameanza kuandika ila hajaweza kubobea na kujenga nidhamu inayostahili katika uandishi. Katika darasa hili tulijifunza mbinu mbalimbali za kiuandishi na kila kitu unachohitaji kujua kuhusu uandishi.

Kwa mara ya kwanza kabisa darasa hili tuliliendesha kwa siku 66, mara ya pili darasa hili tulikuja kuliendesha kwa siku 30 tu. Waliojifunza mbinu za kiuandishi kwenye darasa hili sasa hivi ni waandishi wazuri sana.

Tokea hapo darasa hili limekuwa endelevu, kila mwaka likiendeshwa mara mbili au mara tatu na sasa kwa mwaka huu 2022, darasa hili litaanza tarehe 16,Machi 2022. Hii ni private writing class ukiwa na mimi hapa Godius Rweyongeza na kwenye darasa hili nitakupa mbinu za kiuandishi ambazo hakuna kitabu, mwalimu au sehemu yoyote ile unaweza kuzipata.

 

Kwenye darasa hili hapa unaenda

  • Kujifunza kila kitu kuhusu uandishi
  • Utaanza kuandika (kumbuka sio tu utajifunza kuandika, ila utaanza kuandika, mfumo wa darasa hili umelenga kukufanya uandike badala ya kujifunza tu, na kuna mbinu ya kukusukuma wewe kuandika badala ya kuishia kujifunza maarifa peke yake)
  • Utapata msaada wa karibu kutoka kwangu wa kiuandishi kwa siku 30 mfululizo. Ndio maana nasema, nahitaji watu watu kumi tu, ambao nitawafanya kuwa waandishi wabobevu ndani ya siku 30 zijazo.

Sambamba na hayo kwenye kozi hii

👉Nitakusaidia UANDIKE kitabu chako na kitakamilika ndani ya siku 30.
👉Nitakusimamia na kusoma kazi zako unazoandika kila siku na kukuelekeza namna bora ya kuziboresha

👉Nitakufungulia blogu ya bure.
👉Utajifunza mengi kutokana na yale wanayoandika wenzako na maoni nitakayokuwa natoa kuhusu kazi za wenzako.
👉Utapata kitabu Cha JINSI YA KUWA MWANDISHI MBOBEVU NDANI YA SIKU 30 bure.
👉Utapata jarida lenye hatua 15 za kufuata ili kuandika magazetini.
👉Utapata mafunzo ya audio zaidi ya 10. Yakiwemo mahojiano na waandishi wakubwa hapa nchini.

👉Utaungana na waandishi wengine wanaoandika na kujifunza mengi kutoka kwao.

Nafasi kwenye darasa hili ni 10 tu. Hivyo, kama unataka kuhudhuria darasa hili, sharti uwahi kujihakikishia nafasi yako kabla hazijaisha.

 

Unaweza kujiuliza kwa nini watu kumi na kwa nini siku 30 tu?

Naomba sasa usogeze kiti chako karibu ili nikwambie nini kinaendelea. 

Kwanza nahitaji watu kumi ambao kwangu itakuwa rahisi kuwasimamia na kufuatilia mwenendo wa kila mmoja ndani ya hizo siku 30. Ningeweza kusema watu 100, ila sasa kuwafuatilia watu 100 wote kila siku kwa siku 30 ni ngumu. Ndiyo maana nasema hii ni private masterclass na kila anayejiunga na darasa hili hapa ni V.V.I.P

 

Sasa ngoja nikujibu kwa nini nimechagua siku 30 na sio siku tano au kumi au 60 au 100.

Moja ya lengo muhimu kabisa tutalifanyia kazi kwenye darasa hili hapa ni kuhakikisha kwamba unajenga tabia ya kuandika. Yaani, unaufanya uandishi unakuwa sehemu ya pili ya maisha yako.

Sasa kulingana na utafiti uliofanyika kwenye moja ya chuo kikuu Marekani, tabia mpya huwa inajengwa ndani ya siku 66. Hizi ni siku ambazo unajenga tabia mpya kiasi inafikia hatua ya wewe kufanya kile kitu kama sehemu ya pili ya maisha yako. Hata hivyo utafiti huu unasema kwamba sio kwamba tabia inajengeka siku ya mwisho, yaani siku ya 66. Kipindi hiki cha siku 66 kimegawanyika katika vipengele vitatu.

Kuna siku 22 za kwanza, zipo siku 22 za pili na siku 22 za tatu. Siku za 22 kwanza huwa ni za kuachana na tabia ya zamani.

Siku 22 zinazofuata huwa ni za kujenga misingi ya tabia mpya na siku 22 za mwisho huwa ni za kuimarisha tabia mpya.

 

Sasa kitu kimoja cha kushangaza ni kwamba kuna watu ambao huwa wanawahi kushika tabia mpya mapema na kuna wale ambao huwa wanachelewa. Wanaoshika tabia  mapema huwa inawachukua siku 21 au 22 tu. Ndio maana vitabu vingi vya hamasa utakuta vimeandika kuwa inachukua siku 21 kujenga tabia mpya. Ila kwa utafiti binafsi nilioufanya kwenye suala la uandishi tu. siku 30 zinatosha kabisa kumfanya mtu ambaye hajawahi hata kuandika sentensi kuwa mbobevu. Ndio maana leo hii ninasema kwamba, ninahitaji watu KUMI, nami nitawafanya kuwa waandishi wabobevu ndani ya siku 30. 

 

Sisi kwenye darasa letu tutakuwa na kitu cha tofauti. Badala ya kutumia siku 66 zilizogwanyika kwenye siku 22-22-22 tutatumia 30 zilizogawanyika kwenye siku 10-10-10..

Yaani, tutakuwa na siku 10 za mwanzo. Hizi zitakuwa za kujenga tabia ya kuandika. Baadae tutakuwa na siku 11 za pili. Hapa sasa tutaingia ndani kabisa kwenye misingi na saikolojia ya uandishi yenyewe.

 Na hatimaye tutakuwa na siku 11 za mwisho, hizi zitakuwa za kuandika andiko linalojiuza lenyewe. Ndio namaanisha andiko linalojiiuza.

 

Sasa kwa yeyote atayehudhuria darasa hili atapata kwanza kitabu changu kinachohusu uandishi., sambamba na yote niliyosema hapo juu 

Atapata mwongozo wa uandishi (huu ni muhimu sana hasa kwa mtu anayeanza na hajawahi kuandika)

 

Darasa hili litaendeeshwa kwa njia ya whatasap na ili uhudhurie darasa hili hapa utapaswa kulipia laki mbili (200,000) tu. Nikuhakikishie kuwa hiki ni kiasi kidogo sana, sana kulinganisha na kile unachoenda kujifunza kwenye darasa hili hapa. na fedha hii hapa bado una uwezo kuipata wakati wowote wakati darasa linaendelea au baada ya darasa kuisha endapo utaona kwamba hujanufaika na darasa hili. Ndio namaanisha kwamba fedha yako yote utaipata, endapo hutaridhika na darasa au kupata thamani inayoendana na laki mbili baada ya kuwa umehudhuria darasa hili hapa.

Na utaratibu wa kulipa ni kama ifuatavyo; utatuma fedha kwa 0755848391 jina ni GODIUS RWEYONGEZA, kisha baada ya hapo utanitaarifu ili niweze kukuunga kwenye kundi.

Ukilipia leo

  • Utapata kitabu cha JINSI YA KUWA MWANDISHI MBOBEVU PAPO HAPO
  • UTAFUNGULIWA BLOGU YAKO LEO
  • UTAPATA JARIDA LENYE HATUA 15 ZA KUFUATA ILI KUANDIKA MAGAZETINI leoleo
  • Tutapanga ratiba kwa pamoja ya mimi na wewe kuongea kwa dakika 15 kwa njia ya simu. Hii ni muhimu kwani itanisaidia kujua nini hasa lengo lako kwenye hizi siku 30 na tutakuwa tukifanya kazi kuhakikisha kwamba linakamilika.
  • Lakini pia utapata Audio 3 Za mwanzo.(HAYA YOTE UNAYAPATA KABLA DARASA HALIJAANZA NA HAPO NDIO KWANZA UNAKUWA BADO HATA HUJAPATA ASILIMIA 10 KILE KITAKACHOKUWA KWENYE KOZI
  • Nitakutumia na mwongozo wa uandishi

 

 Kwa mwaka huu darasa linaanza tarehe 16, machi. Na litadumu kwa siku 30.

 

Chukua hatua sasa uthibitishe ushiriki wako kwa kulipia laki mbili (200,000/-) kwenda namba 0755848391 JINA ni Godius Rweyongeza. 

 

Baada ya hapo nitumie ujumbe kunitaarifu kwa namba hiyohiyo.

 Ikumbukwe nafasi ni kumi tu! Zikiisha hakutakuwa na nafasi ya ziada.

 

Njoo ujifunze uandishi kutoka kwangu, nakuhakishia unaenda kujifunza ujuzi wa kipekee sana kwa namna ya kipekee.

 

Chukua hatua sasa lipia kwa 0755848391

 

Kila la kheri

Godius Rweyongeza

Morogoro-Tz

 

 Ninahitaji watu kumi nami nitawafanya kuwa waandishi wabobevu ndani ya siku 30 tu!

 

 

 


One response to “Ninahitaji Watu 10 Nami Nitawafanya Kuwa Waandishi Wabobevu Ndani Ya Siku 30”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X