Je, Viwanja Vya Zama Hizi Vimehamia Mtandaoni


Leo nimeona nifunguke mambo ya muhimu sana baada ya kuona kwamba dunia inazidi kubadilika kwa Kasi sana wakati Watanzania wenzangu wakiwa wanaendelea kuishi kama vile hakuna kinachotokea.

Zamani ilikuwa kwamba mtu akiwa na mashamba makubwa au viwanja basi alikuwa anahesabika kuwa ana utajiri mkubwa sana. ila siku hizi hali inaonekana kama imebadilika.

Nadhani wewe mwenyewe unaweza kujionea mwenyewe.

Kwenye orodha ya matajiri wakubwa duniani, matajiri wangapi wanamiliki viwanja au majumba.  Ebu kwa mfano tuchukue ile kumi bora ya matajiri duniani, ni wangapi wanamiliki viwanja au majumba.

Utagundua kwamba wengi wanamiliki biashara za mtandaoni/intaneti.

Orodha ya matajiri wakubwa duniani kwa sasa

Hapa siyo kwamba nataka kusema biashara ya uwekezaji kwenye majengo siyo muhimu. Ila pia nataka hiki kitu ukiangalie kwa jicho la pili. Kama bado hujaweka biashara yako mtandaoni,basi ni muda wako wa kufanya hivyo.

Biashara ambazo zilikuwa zinafanya vizuri kabla ya intaneti, zilifanya vibaya pale  ziliposhindwa kuhamia mtandaoni. Mfano mzuri ni  kampuni ya Walmart.

Kuna watu hata hawaijui Walmart ila wanaijua AMAZON. Ujue Amazon ni kampuni ya juzi juzi ila Walmart walikuwepo kabla ya Amazon.

Kitu wanachofanya Amazon leo hii, kilishafanywa na Walmart kwa zaidi ya miaka 30 wakati Amazon inaanza. Kama ulikuwa hujui ni kwamba Amazon ilianzishwa mwaka 1994 wakati Warmart ilianzishwa mwaka 1962.

Kwa kipindi hicho chote sisiti kusema kwamba tayari Walmart walikuwa na uzoefu mkubwa kwenye biashara kuliko Amazon wakati amazon inaanza. Sisiti kusema kwamba Walmart walikuwa na rasilimali za kutosha na hata ushawishi mkubwa.

SOMA ZAIDI: ZAMA ZIMEBADILIKA

Kuna kitu gani sasa kilichotokea?

Walichofanya Amazon ni kudandia teknolojia; wakati Walmart wakiendelea kushikilia njia za zamani Amazoni wakakimbilia mtandaoni. Na huo ndio ulikuwa mwanzo wa Daudi kumpiga Goliath.

Unaifahamu stori ya Daudi na Goliath wewe? Niache kwanza niendelee…

Na hiki ndicho nakiona kwa wabongo na waafrika wengi.  Wanaendelea kushikilia ile dhana kwamba zamani mambo yalikuwa yanafanyika hivi wakati mambo yameshabadilika. Shauri yako.

Leo nataka usanuke na uhamishie biashara yako mtandaoni.

Kwa kukusadia nitaongelea mambo matatu yatayokuwa ya msaada kwako.

Mosi, fungua blogu au tovuti

Pili, andikisha biashara yako kwenye Google my business

Tatu, Tengeneza kurasa za Facebook Instagram na Twitter

Haya Sasa tuone maelekezo ya kila kimoja, lakini kwanza hakikisha umejipatia nakala ya kitabu cha bure hapo chini kishauendelee

Fungua Blogu Au Tovuti.

Hapa hakikisha kwamba umefungua blogu au tovuti. Na hili nalisema kwa aina yoyote ile ya biashara, kipaji au shughuli unayofanya. Kwa biashara yoyote ile uliyonacho hakikisha kwamba umefungua blogu na kwenye hiyo blogu, hakikisha kwamba kuna mawasiliano yako na taarifa zote za muhimu inazohusiana na kile unachofanya.

Na hakikisha kwamba, unaweka taarifa za mara kwa mara kwenye blogu yako ambazo zitawafanya watu wawe wanakuja kuitembelea mara kwa mara.

Blogu na tovuti zimekuwepo kwa muda mrefu na umaarufu wake hauishi, ukilinganisha na mitandao mingine ya kijamii. Mitandao ya kijamii huwa inakuja na kupoteza umaarufu wake ila blogu, zinabaki na umaarufu wake kila wakati. hivyo, zitumie vyema blogu

Hili litakusaidia wewe pale watu watakapokuwa wanatafuta taarifa, uweze kuonekana na hivyo kuiunganisha biashara au kipaji chako na watu wenye uhitaji nayo. Sijui hapo umenielewa au nirudie tena

Unachopaswa kufahamu ni kuwa siku hizi mtu akihitaji kitu sehemu ya kwanza kabisa anapokimblia ni mtandaoni ili kuktafuta hicho kitu. Sasa kama wewe umeweka hicho kwenye mtandao, itakuwa rahisi kwa watu kukutafuta na kukupata. Na eneo la kwanza kwako kuanzia ni kwenye blogu au tovuti.

Kwa wale mtakaojiandisha na darasa maalumu la uandishi kwa mwaka huu, nitawafungulia blogu bure kabisa. kwa maelezo zaidi SOMA HAPA

SOMA ZAIDI: Ninahitaji watu 10 Nami nitawafanya kuwa waandishi wabobevu ndani ya siku 30

Fungua ukurasa wa GOOGLE MYA BUSINESS

Eneo la pili la kuweka biashara au kipaji chako ni GOOGLE MY BUSINESS. Huu ni ukurasa ambao unautengenza bure kabisa. ukiwa na GMAIL Unaweza kutengeneza ukurasa huu na kuorodhesha kipaji chako huko kama biashara.

Google huwa wanaonesha vitu mtandaoni kulingana na umuhimu wake, lakini pia eneo ulipo. Unapoweka kipaji au biashara yako kwenye google my business maana yake, watu watakapokuwa wanatafuta kitu kinachoendana na kile unachofanya, wewe utapewa kipaumbele.

Google my business inaitwa local business directory, yaani inawasaidia kuonesha watu taarifa kwenye maneo yaliyo karibu yao. Kwa hiyo badala ya watu wahangaike kwenda sehemu ya mbali kumtafuta mbunifu wa nguo kama wewe, ukiwa umeweka kipaji au biashara yako huko, wataanza kukuona wewe.

Na wakikuona wewe watakutafuta ili uwasaidie kwenye kuwatengenezea magauni safi ya pasaka! Sijui unanielewa hapo!

Kwa hiyo cha kufanya sasa hivi, pakua app ya google my business, kisha orodhesha kipaji chako huko kama biashara. NI BURE

Sasa kila kitu kipo wazi. Ushindwe wewe tu.

Siku nyingine nitaandaa video inayoonesha nammna ya kujiandikisha google  my business. Ili usipitwe na hili hakikisha umejiunga na mfumo wetu wa kupokea makala kwa njia ya barua pepe. Jiunge sasa hivi kwa kujaza taarifa zako hapo chini.

Mitandao Ya Kijamii

Najua wengi watakwambia fungua ukurasa wa facebook, twitter au instagram, ila kama ulivyoona, mimi kwangu kurasa za mitandao ya kijamii siyo nambari moja wala nambari mbili. bali zinakuja kwenye nafasi ya tatu. Na hapa siwezi kukwambia kwamba fungua ukurasa wa facebook au instagram, badala yake ninchoshauri uchague eneo kulingana na kipaji chako kilivyo.

Instgaram ni mtandao ambao unaendana na picha. Hivyo ukiamua kuwa instagram hakikisha kwamba utakuwa mtu wa kutupia picha mara kwa mara.

Twitter ni mtandao ambao unahitaji ujieleze kwa maneno kidogo tu.

Facebokk picha na maneno vyote vinaenda tu. sasa wewe chagua wapi panakufaa zaidi kulingana kipaji ulichonacho.

Kama wewe kipaji chako ni kinahusisha kurekodi video unaweza kufikiria kuhusu kutengeneza akaunti ya youtube.

Kama wewe unarekodi mafunzo kwa njia ya audio unaweza kuchagua platform za audio kama anchor, spotfy na nyinginezo.

SOMA ZAIDI: Faida Za Kuwa Na Blogu Ambazo Hakuna Mtu Amewahi Kukwambia

umekuwa nami GODIUS RWEYONGEZA

0755848391

[block rendering halted]


2 responses to “Je, Viwanja Vya Zama Hizi Vimehamia Mtandaoni”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X