Amsha Uungu Ulio Ndani Yako: Siri Kuu Ya Mafanikio Kutoka Kwa Socrates


 

Socrates anaaminika kuwa miongoni mwa watu waliokuwa na busara katika ugiriki yote katika nyakati zake.

Kipindi hicho kijana mmoja alimfuata kumwomba ushauri wa namna ya kufanikiwa.

Kwa busara Socrates akamwambia njoo siku fulani. Yule kijana akawa kweli ametokea siku hiyo ili aambiwe siri ya mafanikio. Nadhani yule kijana alikuwa anataka njia ya mkato ya kufanikiwa (kulala maskini-kuamka tajiri)

Alichofanya Baana Socrates ilikuwa ni kumwambia yule kijana amfuate. Waliambatana na yule kijana mpaka kwenye mto, huku Socrates akiendelea kumwambia yule kijana amfuate.

Yule kijana aliendelea kumfuata kwa uoga. Walipofika katikati ya maji, Socrates alimshika yule kijana kwa nguvu na kumzamisha KWENYE maji.

Yule kijna akaanza kuhangaika kuona Kama angetoka, ila akashindwa. Akahangaika akashindwa.

Baada ya kuona hakuna tumaini la kuachiwa, kijana akatumia nguvu zote kujitetea akawa ameweza Kutoka chini ya maji.

Kwa hasira kijana akamwambia mzee Socrates, Mimi nimekuomba uniamboe siri ya kufanikiwa wewe unataka kuniua.

Hivi ungekuwa wewe ninavyokujua ungefanyaje? Nadhani sasa wewe ndio ungemzamisha mzee Socrates mazima…. hahaha, tuendelee….

Socrates akamjibu kwa kusema, ulipokuwa chini ya maji ni kitu gani ulikuwa unakitaka sana. Yule kijana akajibu kwa kusema KUPUMUA

Socrates akiendelea kumwambia kwamba  ulifanya chini juu ili upate hilo.

Sasa kama unataka kufanikiwa unapaswa pia kuyapa kipaumbele mafa kama ambavyo kipaumbele chako kilikuwa kupumua ulipokuwa majini.

Ndani yetu tuna nguvu ya ziada ya kutuwezesha kufanya makubwa. Ila nguvu hii isipotumika inabaki ikiwa imelala tu.

Ni mpaka pale tunapokuwa katika mazingira ya hatari ndipo tunajikuta tunafnya makubwa ambayo hatukutegemea. Inapotokea hatari ndio unakuta mtu anakimbia wakati asku zote huwa anawaambia watu kuwa yeye na kukimbia ni kama maji na mafuta.

Rafiki yangu, usisusubiri hatari itokee.

Anza leo kuutumia uwezo mkubwa. Jisukume wewe mwenyewe

Uaisubiri ufukuzwe na mbwa ndio ujue kwamba unaweza kukimbia mbio za marathon!

Usisubiri nyumba iungue ndio ugundue kwamba unaweza kuokoa watu.

Usisubiri profesa wako akamwambie andika kitu fulani ukilete ndani ya saa 48 ndio ugundue kwamba unaweza kuandika kila siku, tena kitu kinachoeleweka.

Kuna ukuu ndani yako. Utumie… Utumie rafiki yangu

Ni Mimi
Godius Rweyongeza
0755848391
Morogoro-Tz

Kupata mafunzo Zaidi BONYEZA HAPA

Kupata eBooks BONYEZA HAPA


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X